Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo

Hon. Deo Kasenyenda Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makambako

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga na Wabunge wenzangu kwamba aijawahi kutokea, nampongeza sana Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ambayo haijawahi kutokea mwaka jana bajeti iliongezwa nyingi, mwaka huu yaani ndiyo yameongezwa ma-bi na ma-bi na ma-bi. Kwa hiyo, tunampongeza sana Mama. Vilevile tunampongeza Bashe pamoja na Naibu wake na Katibu Mkuu na watendaji wake wote kwa kazi nzuri wanayoitendea haki Wizara hii ya Kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka huu uliyopita tulipopata fedha za ruzuku kule Njombe na najua na wenzangu wengine, Wabunge wenzangu tunakupongeza sana. Mpango huu ndiyo umeongeza mazao ya kilimo mbalimbali kwa sababu baadhi ya wakulima walikuwa wanashindwa kununua mbolea kwa sababu ilikuwa bei juu kutoka shilingi 140,000, shilingi 150,000 leo shilingi 70,000, shilingi 60,000 mfumo ulio uweka tunakupongeza sana. Ombi letu sisi watu wa Njombe mfumo huu uboreshwe, uongezwe mawakala zaidi kwa sababu baadhi ya mawakala walikuwa wachache kwa hiyo hawakufikisha sawa sawa foleni ya wananchi ilikuwa ni kubwa. Kwa hiyo tunakuomba uboreshe mfumo, uongeze zaidi mawakala ili waweze kusambaza mbolea za ruzuku kwa wakati unaostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekitiki, vilevile lakini kwa Njombe nimpongeze sana Mkuu wa Mkoa Anthony Mtaka kwa namna alivyoungana na wewe kuhakikisha watu wote waliyojaribu kuchanganya mbolea na michanga walikamatwa. Waliyochanganya mbolea feki walikamatwa kwa hiyo tunampongeza sana Anthony Mtaka kwa kushirikiana na wewe kuhakikisha kwamba watu wanaofanya ujanja pamoja na Mkuu wetu wa Wilaya Kisa Gwakisa waliweza kusimamia vizuri zoezi hili la Njombe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile lakini nitaendelea kumpongeza pia Anthony Mtaka sisi Njombe katika Mkoa wetu Wilaya na Makete ndiyo inayozalisha sana ngano. Kwa hiyo tuna washukuru kwa kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa, kwamba sasa Wilaya ya Makete ndiyo kuwe habu ya kulisha Tanzania na nchi ya Tanzania zao la ngano kwa hiyo tunakupongeza sana Waziri kwa kukubali wazo hili na tunampongeza Mama lakini pia Mheshimiwa Waziri Bashe, mtulie vizuri. Wenzangu wamesema hapa wewe ni kijana, wewe ni kijana kweli ubunifu huo unaoendelea nao ndani ya Wizara yako wako watu wengine wanakubeza. Hao wewe songa mbele ndiyo unapatia. Kwa hiyo sisi tunakitakia kila la kheri uweze kufanikisha vizuri katika mpango huu ambao Mama amekutengea fedha nilizosema hapa ma bi na ma bi sasa yanakwenda kuwa na ma ti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho hili siyo liko kwenye Wizara yako Mwigulu Waziri wa Fedha nilimuona hapa. Nikuombe sana Mwigulu mwaka jana mwezi wa nane Rais alipokuja ulikuepo na wewe Bashe ulikuwepo mkumbushane wananchi wa eneo la kituo cha polisi cha Makambako Mjini fidia ambayo unagharimu shilingi milioni 235 na Rais alihaidi pale kwamba fedha hizi zitolewe. Nimuombe Mwigulu sasa muda umefika aweze kutoa fedha hizi ili wananchi hawa waishi kwa amani kwa sababu wanaishi kwa tabu sana nyumba zao zimebomoka, hawawezi kufanya kitu chochote wanategemea uwalipe fidia ili wakaweze kuishi mahala pengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna zao la parachichi Njombe. Mheshimiwa Bashe tukuombe utakapokuwa unamaliza hapa kutoa majibu ya haya Wabunge tuliyochangia unipe na majibu haya sisi Njombe ndiyo wakulima wakubwa wa parachichi Mkoani Njombe. Zao hili kama nyinyi Serikali maana watu wanao nunua wanatoka sehemu mbalimbali muwe na tamko la Serikali kwamba soko lake liko wapi? maana wananchi sasa wamejikita sana kuvunja mashamba yao ya miti na kulima maparachichi sasa isije ikatokea kama Mbunge mwenzangu mmoja amechangia hapa kwamba nchi nzima sasa wamesema walime korosho na sisi hapa isije ikatokea tukalima zaidi parachichi wakati soko kamili hatujapata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwahiyo akija hapa utuambie soko kamili la parachichi liko wapi? na uhakikishe kinajengwa kiwanda cha parachichi katika Mkoa wetu wa Njombe, cha parachichi ili wananchi wawe na kizazi na kiza kwamba wataendelea kulima parachichi lakini vinginevyo Bashe na timu yako leo nisingependa sana nichangie nakupongeza sana wewe pamoja na Naibu wako pamoja na Katibu Mkuu pamoja na Wizara yote kwa ujumla mshikamane. Sasa kwa mwaka huu wa Kilimo wa 2023/2024 mtakapokuwa mnatuletea mbolea Njombe mtuletee kwa wakati lakini la pili muongeze mawakala kama nilivyosema. Vinginevyo Bashe nakushukuru, endelea na kazi nzuri unaifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.