Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo

Hon. Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, suala la kutumia jembe la mkono halitaweza kuwasaidia wakulima wadogo wadogo. Ni muhimu sana Serikali sasa ipeleke matrekta kwenye vijiji kwa kuanzia na matatu kila kijiji. Tukiendelea kulima kwa mkono bado wakulima wadogo ambao ni wengi hawatafaidika na umaskini utabaki pale pale.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa vituo vya usambazaji mbolea tafadhali sana viwepo vijijini. Wakulima wanatapeliwa sana na wajanja ambao hutumia pikipiki kutoa kituo kikuu na kuongeza bei.