Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo

Hon. Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kumalizia nyongeza ya mchango wangu kwa Wizara ya Kilimo kwa kuwa wakati ninachangia ndani ya Bunge kwa kuwa muda ulikuwa hautoshi sikumaliza kuwasilisha mchango wangu.

Mheshimiwa Spika, ninashauri suala la BBT liwekezwe zaidi kwenye mikoa na ukanda wenye uhakika wa mvua ili kuepuka gharama za ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kwenye maeneo ambayo hayana nvua kabisa. Ninaomba pia kwa kuwa Mkoa wa Ruvuma umekuwa na uhakika wa mvua za kutosha, BBT ipelekwe huko mapema sana nina imani itafanya vizuri sana.

Mheshimiwa Spika, kuhusu miundombinu; Mheshimiwa Waziri Hussein Bashe ameweka mpango mzuri sana wa kuweka miundombinu mizuri kwenye suala la utekelezaji na nitataja baadhi tu ya vifaa ambavyo ni pikipiki, vinasaba, nyumba, magari ambayo ametaja kuwa magari hayo yatawahusu Maafisa Kilimo wa Wilaya.

Mheshimiwa Spika, hoja yangu sijasikia maboresho ya miundombinu kama magari yakitajwa kwa Wakurugenzi wa Taasisi za Wizara ya Kilimo kwa maana ya maslahi yao. Hawa wakurugenzi wanafanya kazi nzuri sana na ndiyo maana Wizara hii imeonesha matokeo chanya katika utendaji wake.

Mheshimiwa Spika, iko haja na ni jambo muhimu sana kwa wakurugenzi hawa kuboreshewa maslahi yao ikiwa ni pamoja na kuwapa magari mazuri yenye uhakika na yatakayokidhi mazingira halisi ya utendaji wao maana hawa viumbe wanazunguka nchi nzima kuhakikisha ustawi wa Wizara, wananchi na uchumi wa nchi unakuwa kama ilivyo sasa. Aidha kwa kuwa hawa wakurugenzi wamekuwa wakifanya kazi na makampuni makubwa yaani matajiri wakubwa ambao wana fedha nyingi ambazo zinaweza kuwaweka katika hali ya majaribu makubwa sana, ni imani yangu kuwa endapo maslahi yao yataboreshwa itasaidia sana kuwaongezea ari ya utendaji wa majukumu yao.

Mheshimiwa Spika, nipende kuliambia Bunge lako tukufu kuwa katika hali ya kawaida nimeona gari la mmoja wa wakurugenzi akiwa ziarani Mkoani Ruvuma katika kufuatilia majukumu yake kwa zao la tumbaku kwa kweli lile gari linaonekana kuchakaa kabisa, nikajiuliza ndio gari analotumia Mkurugenzi kuzungukia nchi nzima? Kimsingi magari kama hayo ni hatari sana kwa usalama wa watendaji hao, hata hivyo viumbe hawa ni rasilimali ya Taifa na inapotokea wanapata ajali na kupoteza maisha mara nyingi tunakuwa tunasema maneno rahisi kabisa kwamba "Taifa limepoteza kiongozi muhimu sana na kwamba pengo lake halitazibika" so what?

Mheshimiwa Spika, hii ni hatari sana na ni hasara kubwa kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mbolea ya ruzuku mfumo uboreshwe kwani inaonesha kuwa mfumo wa mbolea ya ruzuku ina tundu. Aidha, mbolea sasa ipelekwe mpaka vijijini ili kumpunguzia mkulima gharama na adha mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo wafadhila endapo nitamaliza mchango wangu bila kuwataja watu wafuatao na ninaomba majina yao yaingie kwenye Hansard.

Mheshimiwa Spika, Watendaji Wakuu hawa wa taasisi ndani ya Wizara ya Kilimo wanastahili pongezi, wanafanya kazi nzuri sana hakika wanazitendea haki nafasi zao walizopewa nao ni hawa wafuatao; NFRA ni CPA Milton Lupa; Kahawa ni Ndugu Primus Kimaro; Korosho ni Ndugu Francis Alfred; Tumbaku ni Ndugu Stanley Mnozya; TFRA ni Dkt. Stephan Ngailo na CPB ni Ndugu John Maige.

Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa nafasi hii ninaunga mkono hoja na ninaomba kuwasilisha.