Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kasulu Vijijini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. VUMA A. HOLLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi hii na mimi niweze kuchangia kidogo kwenye Wizara ya Maji.
Kwanza niseme tu Wizara hii imesheheni vichwa sana kuna brain kubwa sana kwenye Wizara ya Maji kuanzia kwa Mheshimiwa Waziri mwenyewe ndugu yangu Mheshimiwa Aweso, msikivu, mchapakazi ana brain ubunifu wa kutosha, usimamizi mzuri lakini Naibu Waziri wake Mheshimiwa Maryprisca, timu Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu wote wako sawa sawa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende moja kwa moja kwenye mchango. Jambo la kwanza nishukuru sana Serikali kupitia kwa Mheshimiwa Rais na Waziri na Wizara kwa ujumla kwa miradi mingi ambayo wameendelea kuniletea jimboni kwangu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipokea mradi kwenye Kata ya Rusesa kata ambayo ilikuwa na shida kubwa sana ya maji mradi ambao kwa ujumla wake zinahitajika milioni 984 lakini nimeishapokea milioni 566 kwa hiyo, bado wakiniongezea milioni 300 namalizia ujenzi wa tank kuweka na sora na pampu ili wananchi wa Kata ya Rusesa wapate maji ya kutosha
Mheshimiwa Mwenyekiti, Nyamnyusi nimepata milioni 977, Kagera Nkanda bilioni 1.300, Mvugwe milioni 353, Chekenya milioni 817, Kaboranzuri milioni 962 hii siyo hatua ya kubeza nashukuru sana sana wananchi wa Kasulu wanashukuru sana sana hata leo asubuhi nimekutana na Mheshimiwa Profesa Ndalichako siyo mbaya kwa sababu ni Waziri mmemfunga mdogo hawezi kuzungumza lakini alikuwa anafurahi sana kwa sababu mradi wake mkubwa wa maji Kasulu Mjini umeanza kutekelezwa angekuwa na yeye anaweza kuzungumza angezungumza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme jambo la kwanza nataka Waziri unisikilize vizuri sana, Kigoma tunahitaji Mradi wa Maji wa Ziwa Tanganyika yaani kama kuna kuna legacy broo utaiacha ukiwa kama waziri ni kuhakikisha kwamba tunapata Mradi wa Maji wa Ziwa Tanganyika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, huu mradi unajua URUWASA unaendelea na uchambuzi wa awali na wanasema chanzo kitakuwa kwenye kitongoji cha Shakachakara kijiji cha Kabwera Kata ya Nsimbo halafu tenki kubwa litajengwa Heru Juu Kasulu hii ukijenga tenki pale kama jina lake linavyosema anavyosema Heru Juu maana yake ni sehemu ambayo ina muinuko mkubwa. Maji unaweza ukayatupa kwenda wilaya yeyote Kakonko, Kibondo, Kasulu yenyewe, Kigoma Vijijini, Uvinza kote itaenda mpaka Kaliua na Sikonge kote. Kwa hiyo, nakuomba brother, is a very very big project hata Katavi watapata mpaka Rukwa. Tunaomba sana utusaidie sana sana, kwa kuanzia angalau mwaka ujao wa bajeti tuone kuna usanifu unaanza please over please. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye Mfuko wa Maji wa Taifa. Kwanza hapa nimpongeze bila kumung’unya maneno CEO wa Mfuko wa Maji tena kwa bahati mbaya anakaimu sijajua nyiye mtajua mnavyofanya lakini tumewaita mara kadhaa kwenye kamati tukaangalia progress zao ni ukweli usiyopingika mfuko wa maji umepeleka fedha nyingi sana kwenye kila kona ya nchi hii na kama haitoshi miradi ile hasa ambayo ilikuwa ni kichefuchefu wewe unafahamu umekuwa Waziri. Mfuko wa maji umekusaidia kuikwamua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nisema la kupongezwa kubwa sana kwenye mfuko wa maji ni hili la ubunifu wao wa kukopeshwa mamlaka kubwa za maji zile ambazo zinajiendesha kwa faida. Aingii akilini eti Waziri uumize kichwa eti kutafuta hela ukawape DAWASA no thank you, DAWASA database yao ya walaji wa maji kubwa purchasing power watu wa Dar es Salaam ni kubwa iko wazi huwezi kuwapelekea hela za ruzuku wale. Wale wanajiendesha kwa faida kubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanakopeshwa na mfuko wa maji zile hela ambazo mnazipeleka za ruzuku zile zipeleke Kasulu, zipeleke Kibondo, zipeleke Uvinza, zipeleke Kigoma Vijijini yes lakini haya ma–giants hawa wakopeshwe kwa sababu wanajiendesha kwa faida. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatutegemei kuona unawapelekea kama kwa ndugu yangu pale Mwanza na RUWASA inajiendesha kwa faida kubwa sana naamini wanaweza kukopeshwa na mfuko wa maji wakawa wanalipa. Kwa hiyo, nipongeze sana ubunifu huo lakini tuongezewe pesa sasa mfuko wa maji ili uendelee kukwamua miradi mingi ambayo haijakamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wengi wameguswa kuhusu DUWASA. DUWASA sisi tumewasimamia kama Kamati ya PIC. DUWASA tutawapiga tu madongo bure tunataka Wizara iwasaidie kuongeza miradi ili production ya maji iwe kubwa. Kwa sababu baada ya ile ongezeko la watu Serikali ilivyohamia Dodoma wanasema production yao nusu ya mahitaji ya Mji wa Dodoma sasa unawezaje?
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo nadhani wanajitahidi angalau tunakuja hapa tumeoga, tunakuja tumefua suti zinakaa vizuri I am telling you. Lakini katika hali ya kawaida production fifty percent ya mahitaji. Mradi kama huu ambao nimekuona Mheshimiwa Aweso juzi unaenda kuzindua Nzuguni ya vile midogo midogo ya dharula ifanyike wakati tunasubiri mradi mkubwa wa maji kutoka wapi? Ziwa Victoria kwa hiyo, nimuombe Mheshimiwa Aweso jitahidi sana kuhakikisha kwamba unawasaidia watu hawa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Aweso pale ninae Kaimu Manager wa RUWASA wa Wilaya ya Kasulu Kijana kama wewe, anachapa kazi vizuri japo ana gari bovu kweli kweli kuliko watumishi wa Serikali wote Wilaya ya Kasulu. Kijana anajitahidi sana kweli kweli lakini bado anakaimu, nimekwambia mara mbili mara tatu moja ya jambo la kufanya watu wafanye kazi kwa ufanisi mkubwa ni kuwapa haki yao wanayostahili, yule kijana anatusaidia sana, sana Kasulu sana sana Kasulu hebu mpeni haki yake anatusaidia sana Kasulu, Madiwani wanampenda, Mbunge nampenda, Watumishi wanampenda anasaidia sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii miradi ameisimamia kwa nguvu kubwa ni mbunifu anashirikisha sasa anakaimu leo mwaka wa pili hata yenyewe ile sheria ya kukaimu si miezi sita peke yake Mheshimiwa Aweso.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja ahsante sana. (Makofi)