Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ushetu
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, ahsante nakushukuru sana kwa kweli wewe ni msikivu na unasikiliza sana Wabunge wako.
Mheshimiwa Spika, nilitajka tu nimalizie mchango wangu kwa Mheshimiwa Waziri. Kwanza niendelee kuiomba Wizara ya Maji iangalie visima ambavyo wanachimba nchi nzima waviwekee miundombinu kwa ajili ya kuwafikia wananchi. Kwa mfano ukiangalia kuna Kata ya Masaka ambako ndio kwa mwenyekiti wangu wa kamati, kule kuna visima vizuri kabisa lakini miundombinu haipo.
Mheshimiwa Spika, kuna suala jingine la Mbauti. Miradi mingi ya maji ambayo wanaijenga Wizara ya Maji wanawasahau wafugaji, ningeendelea kuwaomba; ndiyo maana kuna kitu, kama inawezekana hawajagundua Wizara ya Maji, kuna migogoro inakuwa inaibuka kule kwenye miradi mikubwa ya maji. Wafugaji wanazunguka kutafuta maji lakini kwenye kijiji chao kuna miradi mikubwa ya maji.
Mheshimiwa Spika, sasa ningeomba Wizara ya Maji na Wizara ya Mifugo wakae wakubaliane kwenye mradi mkuu wa maji ulipojengwa kuwepo na kitu kinaitwa Mbauti kwa ajili ya kunyweshea wafugaji. Waunganishwe kwenye eneo la mradi wawekewe kama ushirika hivi wawe pamoja halafu wafungiwe na mita yao. Wafugaji hawana shida badala ya kuendelea kuhangaika kuhamahama, wanaondoka kwenye miradi mikubwa ya maji badala yake inaweza kuwasaidia wasiendee kuzunguka kuzurua. Hii kelele wakati mwingine ya wafugaji na wakulima tunaweza tukaipunguza kupitia Wizara ya Maji.
Mheshimiwa Spika, ningeomba Mheshimiwa Waziri aliangalie hili. Tumeliona hata kipindi cha ziara tulipokuwa kwenye kamati, limekuwa ni kero, wafugaji wanalalamika na madhara yake wanaharibu miundombinu ya maji ambayo ni hatari sana.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri aweke mbauti pale wafungue mita, wajikusanye wao wasajiriwe; tena ifike mbali Mheshimiwa Waziri na Waziri wa Mifugo wawasajiri wale wakulima kama wanavyofanya Wizara zingine. Wale wafugaji wakiwasajiri pale wana uhakika kabisa kwamba watafanya kazi vizuri sana.
Mheshimiwa Spika, la mwisho ni uvunaji wa maji ya mvua; ningeomba tuwe na center ya uvunaji wa maji ya mvua kwa sababu maeneo mengi maji ya mvua yanapotea. Wakifanya hivyo kelele nyingi za ndugu zetu wakulima tutaziondoa kwa sababu maji yanapotea yanaenda kwenye mto wananchi wanapata shida.
Mheshimiwa Spika, mimi nikushukuru sana naunga mkono hoja.