Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Afya

Hon. Mwantum Dau Haji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Afya

MHE. MWANTUMU DAU. HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza nichukue fursa hii ya kuwashukuru Mawaziri wangu Mheshimiwa Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake kwa kufanya kazi nzuri sana. Wanafanya kazi usiku na mchana kupumzika hawajui kupumzika kama kazi iwe tu kazi iendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nimshukuru Mheshimiwa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake anazochukua katika Serikali yetu hii ya Muungano jinsi anavyoifanya kazi kubwa na yeye kwa kila pembe, kwa kila rika anafanya kazi. Kila sekta ukija sekta ya afya hapa hayasemeki sasa hivi, anafanya kazi vizuri, vituo vimeimarika viko vizuri, havina wasiwasi kama vile zamani unaingia kwenye kituo, kituo ukitambua lakini hivi sasa hivi tunashukuru sana kwamba vituo vimeimarika na vinafanya kazi vizuri. Kwa hilo tuhongere kwa sote jamani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuendelea pia nishukuru Wizara hii ya Afya ya huku Tanzania, vilevile inafanya kazi vizuri katika nchi yetu hii na hasa inasaidia mpaka na Zanzibar pia inasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niombe kwamba wizara yako inafanya kazi kutusaidia katika Wizara yetu ya Zanzibar ya Afya kule Mnazi mmoja. Hususani ukija kwenye magonjwa ya moyo, magonjwa ya figo na magonjwa ya kupandikiza pia tunakuja kule yanasadia na wanafanya kambi ya kukaa baina ya madaktari wa kule na madaktari wa huku wanazifanya hizi kazi kwa pamoja kwa mashirikiano ili wale wagonjwa na wao wanajisikia na wanajua wanafanya nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa ule muda wa kusema wachukuliwe wagonjwa wapelekwe India au wapelekwe nchi nyingine angalabu sana madaktari wanakuja zao Zanzibar wanawasaidia wagonjwa wa moyo pamoja na figo pamoja na wale ambao wanaopandikizwa kizazi cha kinamama, ahsante sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuendelea naomba sekta hii isituchoke iwe pamoja na sisi, wawe na mashirikiano na madaktari wetu kwa kila mara, kila wakati wawe wanakwenda kutupa mashirikiano kule kwetu Zanzibar ili kufanya kazi zao vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakwenda kwenye mada yangu ya pili kuhusu habari ya saratani. Saratani inatibika tena inatibika sana saratani, zamani ilikuwa ukipata Saratani hofu inakuingia, wasiwasi, mashaka unajua mie hapa tena nishakwenda. Lakini kwa hivi sasa ukiingundua saratani na ukienda uko kwenye Hospitali ya Ocean Road ukitibiwa mapema basi unapona na unakuwa mzima. Kama ujaolewa, unaolewa kama hutaki unafanya kazi zako salama salimini kwa hili gonjwa la saratani hivi sasa hivi la kizazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niombe sasa izidi kufanya kazi kuhusu suala hili la saratani, wagongwa wanapotoka kule kwetu Zanzibar wakija huku Bara kuja kutibiwa Ocea Road wanatoka kule hali zinakuwa taabani lakini wanakuwa hawajambo na pia kule kuna kitengo mmekiweka nyie cha kwamba wale wagonjwa wakiwa wamepata muda mkubwa huku basi wanakwenda kufanyiwa vipimo pale Mnazi mmoja. Kwa hiyo, nikushukuri kwa hilo pia, mnafanyakazi vizuri si haba tunashukuru. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuendelea nazungumzia kuhusu habari ya suala la Afya ya Akili. Suala la afya ya akili haliko kwenye suala la kuwa ndiyo afya ya akili huyu mgonjwa kapata akili, kapelekwa mentally au kapelekwa Milembe ahaa afya ya akili inakuja hata mgonjwa wa sukari, shindikizo la damu pia anapata afya ya akili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu mgonjwa wa sukari akienda akifurahi sana basi kaisha zidisha kila kitu katika kiwiliwili chake, akisema afanye kitu cha ukali kaishazidisha kila kitu wewe unatakiwa uwe standard katika kukaa yako na suala hili la ugonjwa wa sukari. Usifurahi sana, usiwe mkali sana wala usiwe na hamaki sana, ukihamaki basi tayari afya ya akili imeshakuingia ujijui, hujitambui saa yeyote unaweza ukapelekwa mentally. Kwa sababu tayari pale ushaichanganya ile sukari na ile afya ya akili kwa hivyo hii afya ya akili Mheshimiwa Waziri inaingilizana mpaka na magonjwa hayo yapo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ugonjwa huu wa sukari hivi karibuni nilikwenda mie kuhangaika kuhusu dawa za sukari kidogo dawa zilipungua kukawa hakuna kidogo. Kwa hiyo, niombe hizi dawa zinapokuwa tayari basi tuzipate kwa wingi ili zile afya zetu ziimarike na tuweze kufanya kazi ili kazi iendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme hivi sasa hivi naunga mkono hoja asilimia mia moja haya niliyoyasema yanatosha na ninashukuru wizara hii ifanye kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa ruksa yako. (Makofi)