Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Hon. Aysharose Ndogholi Mattembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa nafasi na mimi niweze kuchangia hoja hii muhimu kwa mustakabali wa makundi maalum ya wanawake.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri, Dkt. Dorothy Gwajima, Naibu wake, Mheshimiwa Mwanaidi Katibu Mkuu, Dkt. Jingu pamoja na watendaji wote wa Wizara kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kipekee kabisa nimpongeze Mheshimiwa Rais ambaye amekuwa mstari wa mbele kuyajali makudi maalum, lakini pia kwa namna ambavyo ameendelea kuwatumikia Watanzania kwa moyo wa upendo, nampongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile nitumie nafasi hii kukupongeza wewe binafsi kwa kazi nzuri ambayo unaifanya na namna ambavyo unaliendesha Bunge letu, nakupongeza sana. Paada ya pongezi hizo, nijielekeze moja kwa moja kwenye mchango wangu. Kila kukicha tunasikia vitendo vya ukatli vikishamiri katika jamii. Unasikia mtoto amebakwa huku, unasikia mtoto kalawitiwa kule, unasikia mwanafunzi ametoroshwa, unasikia mwanamke amepigwa, vitendo hivi vimezidi kushamiri katika jamii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niiombe sana jamii yangu iweze kubadilisha mtazamo wa masuala haya, pia niiombe Serikali iweze kuangalia kwa kina na kuja na mkakati mahsusi wa mafunzo maalum kwa ajili ya jamii katika ngazi zote kuanzia Kata, Vijiji hadi Vitongoji. Wahakikishe kabisa mafunzo haya yanafika,kwa sababu vitendo hivi vya ukatili wa kijinsia vinatokea katika ngazi ya familia. Utasikia mjomba leo amembaka mtoto wa dada yake, baba mdogo kambaka mtoto wa shemeji yake. Kwa hiyo ni muhimu sana mafunzo yakafanyika katika ngazi zote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niipongeze sana Serikali, pamoja na mikakati mbalimbali ambayo wanaifanya kwa kila siku ya kuelimisha jamii, lakini bado nguvu kubwa inatakiwa kuwaelimisha jamii ili sasa waweze kuepukana na vitendo hivyo.

Mheshimiwa Spika, pia naomba sana sasa kuwepo na haya madawati ya ukatili wa kijinsia katika kila sehemu, kuanzia ngazi ya kata na ngazi ya Kijiji ili yaweze kutoa miongozo mbalimbali na kuwasaidia wananchi kuweza kuepukana na vitendo hivi vya ukatili wa kijinsia.

Mheshimiwa Spika, vile vile katika Mkoa wangu wa Singida kuna changamoto kubwa ya uhaba wa watumishi wa kada ya Maafisa Maendeleo ya Jamii. Hawa ndio wanaobadilisha mitazamo katika jamii, na ndio wanaoisaidia jamii kubadilisha uelekeo wa maisha yao. Kwa hiyo, naiomba sana Serikali iajiri Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kutosha ili sasa kazi nzuri za Maafisa Maendeleo ya Jamii ziweze kufanyika katika kila eneo na katika kila sehemu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala la mikopo. Naipongeza sana Serikali ambayo imeendelea kutoa mikopo kwa makundi maalum ya wanawake, vijana na wenye ulemavu. Natambua kwamba kwa sasa wamesitisha, kwa hiyo, naomba wafanye maboresho haraka ili mikopo hii iweze kutoka kwa makundi haya ya vijana, wanawake na wenye ulemavu, kwa sababu imekuwa ni mkombozi mkubwa sana kwa wao kujikwamua kiuchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kwa haya machache, naunga mkono hoja. (Makofi)