Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Hon. Neema Kichiki Lugangira

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia katika hoja ya hotuba ya bajeti ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum. Kwanza kabisa ningependa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, Dkt. Dorothy Gwajima pamoja na Naibu Waziri, Mwanaidi na viongozi wote wa Wizara hii kwa kazi kubwa ambayo wanaifamnya.

Mheshimiwa Spika, natambua jitihada za Bodi ya Uratibu wa NGOs chini ya uongozi mahiri wa Mama yangu Mheshimiwa Mwantumu Mahiza pamoja na jitihada za Ofisi ya Msajili wa NGOs katika kuhakikisha kwamba NGOs zote ambazo zinasajiriwa hapa nchini zinafanya kazi kwa kile ambacho wamekiombea lakini pia kwa kufuata mila tamaduni na desturi zetu.

Mheshimiwa Spika, aidha, napenda pia kutumia fursa hii kuwasihi sana viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa pamoja na viongozi wa Serikali ngazi ya jamii na katika maeneo yetu yote waweke jitihada ya kuhakikisha kwamba tunazitambua NGOs ambazo zifanya kazi katika maeneo yetu ili nasi tuwe sehemu ya mabalozi wa kuhakikisha ya kwamba NGOs kwenye maeneo yetu wanafanya kazi kulingana na mila tamaduni na desturi, ikiwemo yale ambayo walisajiriwa nato.

Mheshimiwa Spika, kipekee kabisa namshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango mkubwa wa NGOs katika maendeleo ya jamii. Na kipekee nakishukuru tena chama changu Chama Cha Mapinduzi kwa kutambua umuhimu wa mchango wa mchango wa NGOs na hata kupelekea kutenga nafasi zake mbili za viti maalum kwa ajili ya NGOs ndani ya Bunge lako Tukufu. Niko mimi nawakilisha NGOs kwa upande wa Tanzania Bara lakini yupo pia na Dada yangu Mheshimiwa Khadija Aboud ambaye anawakilisha NGOs kwa upande wa Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, katika bajeti hii mimi nitajielekeza kwenye maeneo matatu, eneo la kwanza ni local content kwenye sekta ya NGOs. Lazima tuweke jitihada za makusudi kabisa kuhakikisha kwamba NGOs za ndani zinaweza kunufaika na miradi mbalimbali inayoingia nchini pamoja na ufadhiri. Kwa takwimu za Ofisi ya Msajiri wa NGOs kwa mwaka jana jumla ya tirioni 1.1 zimeingia na kuratibiwa kupitia NGOs hapa nchini; lakini cha kusikitisha asilimia 70 imepita kwenye NGOs za nje kwa maana za kimataifa na ni asilimia 30 tu ambayo imepita kwenye NGOs za ndani kwa maana ya NGOs za Kitanzania.

Mheshimiwa Spika, mimi ningependa kupendekeza kwa Serikali kuputia Wizara hii waone namna ya kuweka mwongozo ambao utaratibu vizuri, kwamba fedha zinapoingia Tanzania kwa ajili ya miradiya maendeleo ngazi ya jamii lazima NGOs za ndani zipewe kipaumbele. Hiyo itasaidia moja, kuhakikisha kwamba NGOs zetu zinafanya kazi kwa kuzingatia mila tamaduni na desturi, lakini pili kuhakikisha kwamba NGOs zetu zinaweza kukua na miradi inakuwa endelevu.

Mheshimiwa Spika, eneo la pili ambalo ningependa kuzungumzia ni kwamba bado kuna sintofahamu kubwa katika sekta ya NGOs na masuala mazima ya kikodi. Natambua kwa upande wa sekta binafsi wanayo kamati ya maboresho ya sera za kodi, yaani wanaita thick tank, ambayo mara nyingi sekta binafsi inakaa na Wizara ya Fedha na Mipango na wanajadili changamoto mbalimbali za kikodi na wanazipatia ufumbuzi.

Mheshimiwa Spika, Mimi ningependa kupendekeza kupitia Wizara hii ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum sekta ya NGOs iweze kupata kamati ya kikodi ambayo itakuwa inakaa inajadiliana na Wizara ya Fedha na Mipango kuhusu changamoto za kikodi na kupata utatuzi wake.

Mheshimiwa Spika, eneo la tatu ambalo ningependa kulichangia katika eneo hili ni kwamba, kuna umuhimu mkubwa sana wa NGOs kushirikishwa katika mipango mbalimbali ya Serikali Wizara hii inagusa masula ya jinsia masuala ya wanawake ambapo masula ya uongozi na ushiriki wa wanawake katika siasa ni moja ya majukumu yao.

Mheshimiwa Spika, kama ambayo tunatambua Serikali inakwenda kufanya maboresho ya Sheria za Vyama vya Siasa, Sheria za Taifa za Uchaguzi na hata pia mchakato wa katiba mpya. Mimi niombe sana Wizara hii kupitia Mheshimiwa Waziri kuhakikisha kwamba katika michakato ya sheria hizo NGOs zinashiriki ipasavyo lakini pia katika mchakato wa katiba mpya NGOs si tu zinashiriki lakini pia zinawakilishwa ipasavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuhitimisha, naomba niwapongeze tena Wizara hii kwa kazi kubwa wanayoifanya lakini niwaombe Waheshimiwa Wabunge wenzangu na Watanzania tutambue mchango mkubwa ambao unafanywa na NGOs ngazi ya jamii kwa sababu NGOS ndizo ambazo zinashirikiana na Serikali kufikisha huduma pale ambapo Serikali haiwezi kufika, kufikisha maendeleo pale ambapo Serikali haiwezi kufikisha, kwa hiyo ni muhimu tufanye kazi kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika, lakini naendelea kusisitiza pia sisi kama viongozi na viongozi wa dini viongozi wa kisiasa viongozi wa kiserikali lazima nasi pia tuwe tunajukumu la kuhakikisha ya kwamba NGOs hizi zinafanya kazi kwa matakwa ya sheria zetu, Katiba yetu mila tamaduni na desturi.

Mheshimiwa Spika, kwa kuhitimisha, nasisitiza tena umuhimu wa kuwa na Kamati ya kikodi baina ya Sekta ya NGOs na Wizara ya Fedha na Mipango ili tuweze kuhakikisha tunatatua changamoto za kikodi zilizopo. Nasisitiza umuhimu wa kuhakikisha kwamba Serikali inakuja na mwongozo ambao utapelekea NGOs za ndani ziweze kupata rasilimali fedha kutoka nje.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja ahsante sana.