Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia katika hotuba hii ya bajeti ya Wizara ya ujenzi na uchukuzi. Niseme kweli kwamba, Wizara hii kweli ni kubwa sana na inajitahidi sana kufanya kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaenda straight kwenye shirika letu la ATCL. Kitendo cha kusema tunafufua shirika hili na kununua ndege nyingi kilikuwa ni kitendo kizuri sana. Kwa hiyo, niseme kwamba, Serikali haikufanya makosa kuamua kufanya hivyo. Niseme Shirika hili la ATCL limejitahidi sana kufanya kazi pamoja na kwamba, limefanya katika mazingira magumu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua kwamba, Mheshimiwa Profesa Mbarawa amejitahidi sana kuona shirika hili linasimama, lakini jambo moja ambalo linanifanya nione kwamba, kwa nini hiki kitendo cha kuweka ndege hizi kwenye Shirika la Ndege hili, TGFA kwamba, ndio limiliki ndege zile kwa nia ya kwamba, ndege hizi zisingekamatwa kutokana na madeni ya Serikali, lakini imeshaonekana kwamba, hili halipo. Kama halipo kwa nini ndege hizi hazirudishwi au hazipelekwi ATCL? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mkataba huu wa ndege wa ATCL pamoja na TGF umekuwa ukileta madeni makubwa sana kwa shirika hili na kufanya shirika hili lionekane kwamba, linaweza lisiwe na mwendelezo, yaani tuseme questionable going concern. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba, urari hasi wa kiasi cha shilingi bilioni 157.7 kwa ATCL umeletwa na ukodishaji huo. Kwanza tuangalie Ripoti ya CAG katika mwaka 2021/2022 ilionesha kwamba, ATCL ilitumia shilingi bilioni 29.4 kwa matengenezo ya ndege zake, lakini hapohapo ilitakiwa pia ipeleke shilingi bilioni 25.38 kwenye TGFA kama gharama za matengenezo licha ya kwamba, bado kuna zile gharama za ukodishaji ambazo ni kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika speech ya Waziri, ukurasa wa 267 umesema kwamba, ATCL imeweka mikakati mizuri ya kuweza kupunguza gharama za uendeshaji. Kinachonishangaza ni kwamba, Mheshimiwa Waziri hakutaja hili tatizo la TGFA kuwa bado ndio wamiliki wa ndege hizi ambazo zinafanya kunakuwa na double cost ambazo kwa njia yoyote ile hatuwezi kupunguza deni hili au madeni haya ya Air Tanzania. Commitment iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Ikulu mwaka 2021 alisema kwamba, ifikapo tarehe 30/06/2022 umiliki wa ndege za ATCL utakuwa chini ya ATCL yenyewe kutoka TGFA. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sasa ukiangalia tangu ahadi hii ilipotolewa kwamba, umiliki huu ungehamishwa, mpaka leo ni karibu mwaka mzima na hamna kilichofanyika. Kufuatia malimbikizo ya kukodisha ndege hizo toka TGFA takribani shilingi bilioni 113.5 na deni la Mfuko wa Matengenezo ya Ndege takribani shilingi bilioni 60, haya ni madeni makubwa sana ambayo yatafanya shirika hili lishindwe kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda nieleze tu kwa kifupi kwamba, nini athari kubwa ambayo athari zake zitaletwa na huu uhusiano kati ya TGFA na ATCL. Ni kwamba, ATCL inaweza kufutiwa uanachama wake katika Shirika la Mashirika ya Ndege Duniani (IATA). ATCL inaweza kufutiwa mifumo ya kimataifa ya ufuatiliaji wa mizigo. ATCL inaweza kutolewa katika mfumo wa usuluhishi wa mauzo ya tiketi duniani (IATA Clearing House). Shirika hili linaweza kutolewa katika mfumo wa uuzaji na usambazaji wa tiketi duniani (Global Distribution System), pia ATCL inaweza kushindwa kupata vibali vya kufanya safari katika Mataifa mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia pamoja na mikakati kwamba, ATCL inataka ifanye interlining and code sharing, lakini kwa urari huu ambao ni hasi hili linatia mashaka sana na ukiangalia kwamba, ATCL haiwezi kukopesheka kutokana na hali halisi ilivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa ushauri ufuatao, kwamba, Serikali ifute malimbikizo yote ambayo yamepelekwa katika shirika hili ambayo ni takribani bilioni 113.5 na deni la Mfuko wa Matengenezo ya Ndege ambalo ni takribani shilingi bilioni 6.0 na kwamba, umiliki huu wa ndege upelekwe moja kwa moja kwa ATCL badala ya kuwa TGFA. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida gani tunatarajia kwamba, ATCL ikiwa mmiliki moja kwa moja? Ni kwamba, ndege zote za ATCL kama zile Air Bus, Boeing 77, 787A.8, Dreamliner, kwenda vituo vilivyopangwa kama Johannesburg, London, Nigeria na sehemu nyingine, hivyo kufanya ndege hizo kuweza kufanya kazi zake kikamilifu. CAG ameonesha kwamba, ndege hizi kwa kutokufanya kazi zake kikamilifu kwenye full capacity zimeleta hasara ya shilingi bilioni 45 katika mwaka 2021. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni wazi Waziri hili analiona na ndio maana amekwepa kuweka taarifa hii ya ubia kati ya ndege hizi kwa TGFA. Kwa hiyo, anajua kwamba, tumelisema sana kwenye Kamati yetu ya PAC, lakini hakujachukuliwa hatua yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida gani itapata ATCL pia, kwa kuipa umiliki wa ndege zote? Ina maana kwamba, gharama zake za uendeshaji zitashuka kwa asilimia 30 na hasara kuondolewa kwa asilimia 171 ili ndege hizo ziweze kuonekana kwamba, kweli zina-perform vizuri. Kama ATCL itaweza kumiliki ndege zake zote itaweza kuanzisha auxiliary services zake ambazo ndio zinaleta faida kubwa katika mashirika ya ndege. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri Profesa Mbarawa akija kuhitimisha hotuba yake alieleze Bunge lako Tukufu kwa nini imechukua muda mrefu hivi TGFA kukabidhi ndege hizi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kunaundwa Kamati, tunajiuliza, hivi wakati ndege hizi zikiamuliwa kupelekwa TGFA Kamati ilichukua zaidi ya miaka miwili kuzungumza suala hili? Kwa ajili hiyo, niombe kwamba, Serikali ione athari hizi na ielewe kwamba, hili shirika pamoja na kwamba, tumeweka mikakati mingi, inatumia fedha nyingi za Serikali ambazo ni fedha za umma, lakini bado tumelifunga miguu na mikono halafu tunaliambia likimbie. (Makofi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe Serikali iweze kuweka wazi kwamba, kweli itatoa lini, iwe na commitment ambayo ile ya Katibu Mkuu huyu wa Ikulu ambaye sasa hivi ndiye Katibu Mkuu Kiongozi imeshindikana, mwaka mzima sasa hivi lakini hata hotuba ya Waziri haikuzungumzia suala hili. Kwa hiyo, inasikitisha kwamba, Serikali imechukua muda mrefu sana kuona kwamba, ATCL inatakiwa ifanye kazi, iwe competitive sawa na mashirika mengine duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufikia hapo, nasema kwamba, hayo ndio yangu kwa leo. Ahsante sana. (Makofi)