Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. DKT. MEDARD M. KALEMANI: Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani nyingi sana kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi anavyotafuta fedha, kutoa fedha na kuleta maendeleo kwa Watanzania, hongera sana.
Mheshimiwa Spika, tunaona jinsi pesa nyingi za ujenzi wa miradi ya miundombinu ikiwamo barabara, bandari na madaraja zinavyoendelea kumiminika katika maeneo ya wananchi.
Mheshimiwa Spika, miradi ya barabara zilizokamilika na zinazoendelea kujengwa, zilizoorodheshwa katika taarifa ya Wizara ni kielelezo cha kazi kubwa inayoendelea kufanyika kutokana na juhudi za Mheshimiwa Rais. Nashukuru katika Jimbo la Chato pia pesa nyingi zaidi ya shillingi bilioni 5.7 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita zimetolewa. Hii ni hatua ya kupongezwa sana. Naishukuru Serikali kwa niaba ya Wana-Chato kwa kutoa shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya kuanza kujenga barabara kutoka Bandari ya Nyamilembe kuelekea Katoke umbali wa km 50.01, bararara ya SIDO - Ginnery ya Chato na Ginnery hadi Sekondari ya Janet Magufuli. Ombi langu ni kuiomba Wizara kupitia TANROADS kukamilisha haraka taratibu za manunuzi ili ujenzi wa barabara hizi uanze haraka.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wananchi katika eneo hilo hasa katika sehemu ya upanuzi wa eneo la Gati la Nyamilembe wapo wananchi wanadai fidia, naiomba Serikali yetu ikamilishe fidia hiyo ili kundoa kero hiyo kwa wananchi hao.
Mheshimiwa Spika, wananchi wa Jimbo la Chato wamenituma nitoe shukrani kwa Serikali hasa kwa Mheshimiwa Rais kwa kukamilisha ujenzi wa Gati la Bandari ya Nyamilembe, tunaomba bandari hii izinduliwe ikiwezekana na viongozi wa kitaifa ili wananchi wafikishe shukrani na furaha hizo moja kwa moja kwa Serikali yao. Nampongeza Mheshimiwa Waziri na timu nzima ya Wizara na taasisi zake.
Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na naunga mkono hoja.