Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nitaanza na Serikali kulipa malimbikizo ya madeni ambayo yanatokana na safari za kikazi na uhamisho kwa Askari wetu.

Pili, Serikali ihakikishe inawapa fedha askari kununua uniform. Wamekuwa wakijinunulia uniform wao wenyewe na mtakapoanza kuwapa fedha mhakikishe mnapa na arrears zote za nyuma ambazo wamekuwa wakitoa hela zao kununua uniform maana yake mshahara wao wenyewe ni mdogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni kuhusiana na manyanyaso wanaopata Askari wenye vyeo vya chini kazini. Nimepokea malalamiko mengi sana kwa Askari Magereza na hata Askari wa Jeshi la Polisi, Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Naibu wako nimeshafikisha baadhi ya manyanyaso hayo. Unakuta Askari wengine wananyanyasika wanahamishwa hata zaidi ya mara 10 kisa tu mkubwa wake anamchukua mwenza wa huyu Askari, kitu ambacho siyo haki kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna kesi nyingine ambayo nitaenda kuitoa kama case study ili muweze kufanya kama ni tafiti au muunde Tume kuhakikisha kwamba hawa Askari ambao wanajitoa wasinyanyasike. Kuna Askari ambaye alikuwa ni Askari Magereza wa Gereza la Karanga anaitwa George Mkonda alikuwa ni Koplo by then 2014. Mkuu wake wa Magereza kukawa na mgongano wa kimaslahi akamuundia zengwe, Askari huyo akapeleka malalamiko yake kwenye Ofisi ya Rais, Maadili ya Viongozi wa Umma, wakamuandikia huyu Mkuu wa Gereza onyo. Hakuishia hapo akaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri sana huyu Mkuu wa Gereza akapandishwa cheo kuwa RPO wa Kilimanjaro. Mheshimiwa Waziri Masauni unajua na Naibu Waziri unajua na hata Katibu Mkuu wa Wizara unajua, alivyokuwa hivyo akamuundia zengwe huyu Askari akashushwa cheo akapewa adhabu ya miaka mitatu akahamishwa kuja Dodoma. Kuanzia 2016 adhabu kwa kawaida ni miaka mitatu mitatu, amekaa na adhabu mpaka 2021, miaka mitano ndiyo akarudishiwa cheo chake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hawa Askari wanajitoa, mimi nimeshawahi kwenda gerezani jamani, hawa Askari wana-risk maisha yao sana hasa Askari Gereza. Nimekaa gerezani miezi minne naona jinsi wanavyojitoa, kule gerezani mnapeleka watu wa tabia mbalimbali, yet akitoka hapo apate frustration ya mkubwa wake wa cheo anamnyanyasa katika kazi, is not fair! Huyu Askari amehangaika hebu mtendeeni haki. Msikilizeni, kwanza mmlipe hela yake. Hii adhabu yenyewe amepewa ya magumashi tu, kwamba eti alikuwa anachukua simu za ndugu za mahabusu anawachaji shilingi mia tano, mia tano, hao ndugu wenyewe hawakuwahi kuitwa kuja kutoa testimony, amelalamika mtoto wa watu hamjamsikiliza, mmemshusha cheo miaka mitano, hamjampa malimbikizo. Wenzake sasa hivi ni Staff Sergeant, yeye bado ni Koplo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri msikilizeni, amehangaika sana, Katibu Mkuu wenu ana hii kesi, hebu isikilizeni muifanye kama case study muweze kuwasaidia Askari Magereza, Askari Polisi na wengine wote ambao wananyanyasika kwa sababu vyeo vyao ni vidogo hawawezi wakaongea kwa maadili. Najua kwa maadili yao hawawezi wakaongea, wasaidieni, apewa arrears zake zote, maana yake alitakiwa arudishiwe cheo chake 2019 lakini wamemrudishia 2021, lakini anatakiwa apandishwe kila baada ya miaka mitatu, mkijua kwamba ilikuwa ni zengwa mrudishieni vyeo vyake vyote nae aende kuwa kwenye Staff Sergeant. Nilimsikia Mheshimiwa Rais analalamika kwamba unakuta Askari wanakuwa mpaka wazee wakiwa kwenye Staff Sergeant! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mambo yenyewe ndiyo haya wanatumikia wanabaki na vyeo vidogo kwa sababu wananyanyasika they cannot say anywhere. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kabisa Serikali ichukue hili, iunde kama ni Tume Maalumu wafuatilie watu wanaonyanyaswa..

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Esther.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Wafuatilie watu wanaonyanyaswa Askari hawa wa chini waweze kutendewa haki. Ahsante sana. (Makofi)