Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kuridhia Kufutwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Kigosi ili Kuruhusu Kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu wa Kigosi na Azimio la Bunge la Kuridhia Kurekebisha Mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha

Hon. Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kuridhia Kufutwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Kigosi ili Kuruhusu Kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu wa Kigosi na Azimio la Bunge la Kuridhia Kurekebisha Mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Niendelee kukushukuru sana wewe kwa kazi nzuri ambazo unatuongoza. Leo ni takribani miezi minne ukiendelea kuongoza mhimili huu mkubwa, kazi inafanyika vizuri.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi nzuri anayoifanya, namna anavyoshughulikia migogoro ya hifadhi zetu. Kashughulikia mgogoro wa Ngorongoro, wananchi wamesafirishwa kwa uhakika kabisa na sasa hivi wanafurahia maisha mapya bila kelele yoyote, na Mheshimiwa Rais anashughulikia migogoro ya nchi kwa uhakika kabisa. Tuendelee kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu.

Mheshimiwa Spika, nikupongeze sana Mheshimiwa Waziri, kwa kweli unastahili maua yako, pamoja na Naibu Waziri, Makatibu Wakuu na Wizara yote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwapongeze sana Makamishna wa Uhifadhi wa TANAPA na TFS; kazi nzuri wanaendelea kufanya. Wanatambua nafasi ya kazi ambayo mmewapa.

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba hili suala wananchi walikuwa wamelisubiri kwa kasi kubwa sana, na hatimaye limeweza kufika. Nikupongeze Mheshimiwa Mary Masanja, ulifika kwa wananchi wa Ushetu, uliongea nao, uliwasikiliza na uliwaahidi. Na leo wanaona matunda mazuri ya Mheshimiwa Rais; ni kazi nzuri ambayo imefanyika.

Mheshimiwa Spika, niendelee kukuomba tu Mheshimiwa Mchengerwa, Waziri wetu, kwa sababu sasa tunakwenda kulirudisha pori hili kwenye uhifadhi wa wananchi wetu, kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kigosi sasa inakwenda kuwa Hifadhi ya Kigosi; nikuombe sana Mheshimiwa Waziri, tuna wananchi wetu wafugaji, wanaorina asali, wavuvi pamoja na wachimbaji, sasa wanakwenda kufaidika na rasilimali hizi.

Mheshimiwa Spika, tuna tatizo moja naomba tulifanyie kazi; tuwasajili wafugaji na warina asali, tuweze kuwatambua; wachimbaji wadogo tuweze kuwatambua. Lakini pia na wenzetu ambao wanaingia pale kuvua samaki na wenyewe waweze kutambulika ili tujue kazi hii sasa wanapoingia kwenye kurina asali tuweze kujua, ili tunapojua sasa kwamba idadi yao ni wangapi, inatusaidia sana namna ya usimamizi mzuri kwenye hifadhi.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais kafanya kazi kubwa sana. Ukiangalia leo katika Jimbo la Ushetu peke yake, Kata zinazokwenda kufaidika na eneo hili, kuna Kata kubwa sana ya Ulowa, inakwenda kufaidika; Kata za Ubagwe, Ulewe, Idahina, Nyankende na Bulungwa. Wote hawa wanazungukwa na pori hili ambalo sasa wanakwenda kufaidika wananchi wetu.

Mheshimiwa Spika, lakini bado kuna Wilaya zetu za Bukombe, Kaliua, Mbogwe kwa ndugu yangu, Waziri, Mheshimiwa Doto Biteko. Wananchi hawa wote wanazunguka pori hili. Ni kazi nzuri, kubwa sana Mheshimiwa Rais ameifanya. Mheshimiwa Rais ni msikivu, pamoja na kwamba ametuma Mawaziri wote wamezunguka maeneo haya, lakini anaporudishiwa ripoti anaifanyia kazi hapohapo na kutoa matokeo. Sasa haya ni matokeo ya Mheshimiwa Rais jinsi anavyosimamia rasilimali za nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niendelee kukupongeza sana wewe, lakini niipongeze sana Serikali, niwapongeze sana Kamati, Kamati imefanya kazi kubwa sana; hongereni sana Kamati. Kazi iliyofanyika ni kubwa, imeishauri Serikali kwa uhakika bila upendeleo, na leo wananchi wetu migogoro inakwenda kuondoka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niendelee kuiomba Wizara, endeleeni pia kushughulikia na migogoro ya maeneo mengine, endeleeni pia kushughulikia na mipaka ya maeneo mengine. Ili Mheshimiwa Rais anapoelekea 2025 tuendelee kumpa maua yake, aendelee kubeba kura zake, tuendelee kumtendea haki. Kazi anayoifanya leo Mheshimiwa Rais ni matokeo atakuja kuyapata maua yake 2025, ni kazi kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo niendelee kupongeza kazi nzuri imefanyika, wananchi wa Ushetu sasa wanakwenda kufurahi, kufaidika. Kama Mbunge naahidi kuongeza nguvu kuhakikisha tunaendelea kuwapa elimu ili waendelee kui-support Serikali katika tukio hili.

Mheshimiwa Spika, nikupongeze tena; naunga mkono hoja. (Makofi)