Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja Kuhusu Bei ya Kuuza na Kununulia Mahindi

Hon. Joseph Kasheku Musukuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hoja Kuhusu Bei ya Kuuza na Kununulia Mahindi

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Naomba sisi Wabunge tumwogope Mungu. Nakumbuka mwezi wa Februari na Machi tulipokuwa tunapiga kelele humu kulalamikia mfumuko wa bei, tulipotuma lawama ni Serikalini. Sasa, kama Serikali imeamua kuweka utaratibu ili tukipiga kelele iwe na majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilinde, mimi ni mfanyabiashara na mimi na–export mahindi. Humu kuna wengine hawafanyi biashara hiyo. Mimi najitoa kusema, nafanya hiyo biashara. Hakuna mahali Serikali imezuia kutoa mahindi nje, mpaka leo mimi natoa, lakini nataka niwaulize Wabunge wenzangu, ni nchi gani ambayo inafanya biashara kiholela? Juzi Watanzania zaidi ya 50 waliandamana Zambia. Walikwenda kununua mahindi Zambia, yakakamatwa kwa sababu hawakufuata utaratibu.

Mheshimiwa Spika, masharti yaliyowekwa ni kukata leseni na kufungua Kampuni. Waheshimiwa Wabunge tumwogope Mungu. Mimi nafanya hiyo biashara na Jimbo langu linaongoza Kanda ya Ziwa kwa kulima, Wabunge wanafahamu. Watu wanatoka Uganda na mitumbwi wanakuja kukaa Ziwani wananunua, wanapakia na hela za Uganda na mataka taka bila kufuata utaratibu. Ninyi ni wasomi wa design gani? Tutawezaje ku–control hata hizo dola tunazohangaika? Serikali iweke utaratibu, watu wafuate utaratibu na hela ziwe kwenye system ya Serikali, ndio tutapata hata dola kutoka nje. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tutakaribisha magaidi, wafanyabiashara watakatishaji. Nikuombe masharti ya kufungua kampuni ukianza leo sasa hivi saa ni nne, saa kumi una leseni, wanaogopa nini? (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)