Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja Kuhusu Bei ya Kuuza na Kununulia Mahindi

Hon. Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Hoja Kuhusu Bei ya Kuuza na Kununulia Mahindi

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kwanza, naomba ni–admit jambo moja ambalo linaleta masikitiko. Wakulima wa mahindi wamekuwa wakipitia misukosuko mikubwa sana. Mwezi Mei na Juni huu ambao upo, mwanzoni bei ilikuwa imefika shilingi 80,000 shilingi 90,000 hadi shilingi 100,000. Ghafla tu ni kama Serikali hawakuwepo na hawakujua kama kutakuwa na jambo hili. Ghafla bei zilipokuwa hapo ndio wana–impose mambo mengi yanayojitokeza, documentation na nini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii imekuwa ni tendency kwa wakulima wa zao la mahindi yaani kila mwaka kuna jambo. Vile vile, kuna mtu mmoja anajaribu ku–admit kwamba ule mchakato ni rahisi na nini. Ungekuwa rahisi ungesababisha wanunuzi waje kirahisi. Hii inatokana kwa sababu hakuna competition. Mheshimiwa Waziri, jana amesema kwamba bei elekezi ni shilingi 800. Mahindi sio kama mafuta anayopanga bei elekezi. Bei ya mahindi inakuwa determined na competition kwa maana ya demand na supply. Kwa nini imeshuka? Ni kwa sababu supply ya mahindi ni kubwa na demand imepungua kwa sababu wanunuzi hawapo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tuache soko huru. NFRA najua watanunua lakini hata baadaye hawawezi wakanunua mahindi, najua sasa hivi hawanunui. Hata wakija hawana uwezo wa kununua mahindi yote. Turuhusu competition, wafanyabiashara wanunue. Hizi restriction tunakubaliana na jambo Serikali ililokuja nalo. Waahirishe mpaka mwakani ndiyo wajipange, lakini kwa mwaka huu tuache amani kwa wakulima wauze, nao wanataka wainue uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niombe tu, Mheshimiwa Bashe, aahirishe jambo hilo. Kwa sasa, hizo restrictions kama tutaendelea kwa namna tunavyoenda hivi, tunakwenda kumuumiza mkulima wa mahindi. (Makofi)