Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

Hon. Geoffrey Idelphonce Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Masasi Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

MHE. GEOFFREY I. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Kwanza kwa niaba ya watu wa Masasi ningependa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha siku ya leo. Pia nikishukuru sana Chama changu Cha Mapinduzi kinachoongozwa na Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupigania Watanzania lakini kipekee kwa kunipigania mimi Mbunge wao kule Masasi kwa kuhakikisha kwamba changamoto za Masasi zinaondoka. Na Masasi sasa hivi ni mpya, na kila mmoja anaiona kwamba Masasi inang’ara. Hiyo yote ni juhudi za Mheshimiwa Rais kuniunga mkono mimi kama Mbunge wake tukishirikiana na Mheshimiwa Madiwani ambao niko nao kule Masasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuyasema hayo ningetamani nichangie kwenye bajeti hii ambayo imewasilishwa na Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango. Tunafahamu kwamba bajeti ni makadirio ya mapato na matumizi, ni makadirio tu. Kwa hiyo nina michango kwenye maeneo haya mawili; mapato na matumizi. Ningeomba sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha anisikilize, najua itamsaidia. Na kwa sababu muda ni mdogo nitajitahidi kwenda haraka haraka. Yeye ni mchumi mwenzangu, anajua, kwamba nikizungumza kitu basi ajue namna ya kuki-pick.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, na hii naendelea kusisitiza sana; any sense to the government, the first concern ni employment ya vijana wake. Tukitengeneza fursa pana za ajira kwa vijana tafsiri yake tunaongeza direct tax payment. Kwa upande wa wale vijana wanalipa kama pay as you earn, ambayo ni personal income tax kutoka kwenye mishahara yao lakini pia makampuni na shughuli watakazokuwa wanazifanya nazo zinalipia cooperate income tax, ambayo ni direct tax ambayo ni ya uhakika kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tukifanya hivyo tunaweza tukahakikisha kwamba tunatoa fursa pana zaidi kwa Serikali kukusanya kodi ambayo inaweza ikasaidia kwenye upande wa matumizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inaendana na adhma ya kupanua tax base. Amezungumza Mheshimiwa Kihenzile hapa inasumbua kidogo; na bahati nzuri nilihudumu kidogo kwenye Bodi ya TRA. Tunaolipa kodi ni wachache sana kwenye nchi hii. Sensa imeonesha kwamba tuna watu milioni 61 lakini walipa kodi hapa ni kama milioni tatu tu wale wenye active TIN Number, wako milioni tatu tu; na hiyo ni watu binafsi pamoja na kampuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kwa hiyo ni watu wachache sana wanaolipa kodi, matokeo yake concentration inakuwa kubwa kwa sababu wachache wanaolipa kodi wanalazimika kulipa kodi sana na wanalazimika kukamuliwa sana ili kufikia malengo ya kitaifa, lakini tungetanua tax base tungerahisisha na kufuata zile rules tano za usimamizi wa kodi. Kwamba kodi lazima kuwe na fairness, kodi lazima kuwe na adequacy, kodi itoshe kuitosheleza Serikali lakini kuwe na simplicity, kuwe na urahisi wa ulipaji kwa yule mlipa kodi kwa sababu ya compliance iko juu lakini lazima kuwe na transparency la mwisho lazima administratively kuwe na easiness, kuwe na urahisi wa kukusanya hizo kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa natamani nigusie kwenye maeneo ambayo tunaweza tukasaidia hawa vijana kupata ajira nyingi pia tupate kodi za kutosha. Eneo la kwanza; tunafahamu kuna ule mradi wa Mkurabita nchi yetu sisi structure ya uchumi wetu asilimia 60 mpaka 70 ni informal sector, kule kodi huwa hazipatikani kirahisi kwa sababu si sekta rasmi. Kwa hiyo Mkurabita nafikiri imeshakufa. Lengo kubwa lilikuwa ni kuweza kutengeneza utaratibu wa kampuni mbalimbali na watu binafsi shughuli zao ziweze kurasimishwa ili waingie kwenye tax net waweze kulipa taxes kwa kuwa tax payers. Kwa hiyo nilikuwa nafikiri Mheshimiwa Waziri arudi kwenye ku-reform informal sector ili ziwe formal kupitia mikakati mbaliambali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine, mwaka wa jana Bunge lako Tukufu Mheshimiwa Mwenyekiti lilipitisha azimio kutoka kwenye Kamati yetu ya PAC la ku-undertake a comprehensive tax system regime of view ambayo ilifanyika mwaka 1992 ambayo ndiyo iliyotengeneza mifumo ya kuanzishwa kwa TRA. Kwamba ni structure ya aina gani ya kodi tulipe, nani alipe, aina gani ya shughuli zitozwe na viwanda vikoje. Yaani tupitie upya huo wigo mzima wa kikodi ili tuhakikishe kwamba tunapata walipa kodi sahihi aina ya kodi sahihi pia na mfumo wa ukusanyaji ambao uko wezeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni uwajibikaji wa wizara zingine zote za kisekta kumsaidia Waziri wa Fedha kukusanya mapato, kumsaidia kutengeneza mapato. Kazi ya wizara hizo ni kutengeneza vyanzo vya mapato kwa ajili ya Wizara ya Fedha. Kwa hiyo kila Wizara ingetakiwa kuwa na lengo inayopewa iwe ni four trillioni, wewe five 5 trillion, wewe three trillion. Wakae na kuona; yale maeneo ambayo Waziri wa kisekta ana changamoto nayo anamwambia Waziri wa Fedha ili nikuletee four trillion naomba labda 10 billion kwenye eneo hili. kwa mfano Mheshimiwa Waziri Bashe anaweza kabisa kuweka mkakati wa kufufua viwanda vya korosho kule Masasi, Tunduru, Lindi na kwingineko; ili ajira zikiwa nyingi pamoja na kuongeza thamani kodi inakuwa ni kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tunafahamu kwamba tuna mradi mkubwa wa Mtwara Development Corridor ambao unatakiwa kuchochea kule ikiwemo Liganga na Mchuchuma pamoja na ujenzi wa ile reli ya kule Kusini. Tukifanya hayo na matumizi sahihi ya Bandari ya Mtwara tutakuwa na trilioni ya fedha ambazo tutazikimbia. Lakini…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. GEOFFREY I. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kwa kusema naunga mkono hoja asilimia 100 na sisi watu wa Masasi tuko Imara kuweza kuhakikisha kwamba tuna-support Chama cha Mapinduzi kiweze kupata maendeleo, ahsante sana. (Makofi)