Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

Hon. Bakar Hamad Bakar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024

MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii nami niwe mchangiaji kwenye Hotuba yetu hii ya Bajeti ya Serikali. Nimpongeze Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo anaendelea kutenda mema kwa Watanzania, lakini nimshukuru na nimpongeze kwa bajeti hii ambayo jumla ya zaidi ya trilioni 44 ambayo ametuletea mwaka huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru pia na nimpongeze kwa utendaji kazi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo afya, ikiwemo elimu, ikiwemo ujenzi wa Barabara, lakini reli ya kisasa ambayo inaendelea kujengwa, lakini nimpongeze kwa mambo mbalimbali ambayo yanaendelea kwenye nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sitatenda haki kama sikumpongeza Waziri na Naibu Waziri wa Wizara hii kwa namna ambavyo wanaendelea kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza majukumu ambayo Watanzania wamewakabidhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwapongeze na niwashukuru sana kwa namna ambavyo wanaendelea kushirikiana na Wizara inayohusika na Fedha na Mipango ya Zanzibar. Kwa kweli kulikuwa changamoto nyingi ambazo ziko kwenye maeneo yao, walipoingia wao wamekwenda kushirikiana katika utatuzi na leo hii tunazungumzia mambo mengi ambayo yamefanywa mazuri kwenye ushirikiano huu wa Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwatie moyo na niwaombe Wizara hii waendelee kupiga kazi. Sisi tuko pamoja nao na tunawaunga mkono, tunawaombea sana Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa afya bora, lakini pia hekima iendelee kuwatawala. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la uwekezaji. Hatuwezi kuongeza idadi ya walipakodi, hatuwezi kupiga hatua ya kuongeza watu wenye ajira kwenye nchi yetu kama hatukuhamasisha, kama hatukuendelea kujenga mazingira rafiki, kujenga mazingira mazuri kwa wawekezaji ambao wanakuja kuwekeza ndani ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la uwekezaji haliepukiki, ni lazima nchi yeyote kwanza iangalie wananchi wake na hususani kundi kubwa la vijana. Vijana hawa lazima tuwaangalie kwenye suala la ajira na kwenye suala la ajira hatuwezi kwenda kwenye ajira kama hatukuweza kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali ambayo yanazalisha ili kuweza kuwapa vijana wetu ajira. Tunapoongeza ajira maana yake tayari tunaongeza walipakodi na hapo ndipo tunapokwenda kuzungumzia suala la upunguzwaji wa viwango vya kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumza sana kwamba viwango vya kodi bado viko juu, lakini tutafanyaje kwa idadi hii ya walipakodi ambao wanahudumia Watanzania walio wengi? Hatuwezi kupunguza viwango hivi, lakini nadhani dawa ya jambo hili ni kuongeza walipakodi hasa wa kuwekeza maeneo mbambali ili kuweza kupunguza rate ya kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima ifike mahali Tanzania tuache, tubadilike na tubadilishe mindset zetu, tukiona tu hatuwezi kumwona tu Mzungu yeyote au mtu mweupe yeyote tu hapa nchini halafu tukawa tunadhania amekuja kutuibia. Dhana hizi potofu ni lazima tuzipige vita, ni lazima wananchi wa Tanzania wabadilike, hakuna, haiwezekana kwamba nchi yetu sisi tuwe sisi tu wenyewe tu tumejifungia, haiwezekani. Tuna-lack of experience katika mambo mengi sana, tuna-lack mitaji kwa mambo mengi sana lakini tuna-lack teknolojia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu wana fedha, wenzetu wana teknolojia nzuri, wenzetu wana uwezo wa kuweza kutekeleza mambo mbalimbali, lazima tuweke mazingira rafiki na lazima tuwavutie. Nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wetu kwa hakika anaendelea kufanya kazi kubwa kwenye kuwavutia wawekezaji kuja nchini kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna eneo moja ambalo mchango wake mpaka sasa ni mdogo kama vile limesahauliwa. Suala la uvuvi, bado rasilimali tuliyonayo kwenye bahari ni kubwa sana, lakini ukiangalia mchango unaochangiwa kwenye sekta ya uvuvi ni asilimia 1.8. Kwa kweli katika eneo hili ni lazima tuendelee kuwekeza ili kuweza kuongeza, kuweza kutumia bandari yetu au kuweza kuitumia bahari yetu katika kuongeza pato la Tanzania, kuongeza ajira, lakini pia kuweza kupunguza ile rate ambayo nimezungumza pale mwanzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)