Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo

Hon. Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa hii ili na mimi niweze kuchangia katika Wizara ya Kilimo bajeti hii ya mwaka 2022/2023.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiisoma hii bejeti na maudhui yake yote ni bajeti ya kupigiwa mfano toka nimekuwa Mbunge Awamu ya Kwanza na sasa Awamu ya Pili. Kutoka Shilingi Bilioni 274 mpaka kufikia Shilingi Bilioni 751 siyo mchezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, basi niombe sasa, Mheshimiwa Waziri nia yake ni njema, amekuwa akifanyakazi vizuri sana na tunayo matumaini makubwa sana Watanzania kupitia Waziri mwenye dhamana Mheshimiwa Hussein Bashe kwa namna ambavyo amejipata vizuri yeye na timu yake kuhakikisha kwamba analeta mageuzi makubwa sana katika sekta ya kilimo. Sisi tunakutakia kila la kheri Mwenyezi Mungu akupe afya njema wewe pamoja na Naibu wako na Watendaji wako, tunamuomba tu Mheshimiwa Mama yetu Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aendelee kukuacha hapo kwenye nafasi hiyo ili malengo yako na ndoto yako ya kuwatumikia wananchi na kufanya mageuzi yatimie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nizungumze kuhusiana na suala la mbolea. Waheshimiwa Wabunge wengi wamezungumza, kwamba tarehe 4 Aprili, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete hapa Dodoma, Mheshimiwa Rais alizungumza na Watanzania kupitia mkutano ambao ulikuwa umeandaliwa na Waziri wa Kilimo, akaahidi kwamba katika sekta ya kilimo atahakikisha kwamba anaweka ruzuku ya shilingi bilioni 150 ili kuenda kuwasaidia wakulima kupata nafuu na afueni kwenye suala la mbolea. Ninaomba isije ikawa hapa ndani ya Bunge kazi yetu ni kudemka tu na utekelezaji haupo. Niwaombe sana Wizara ya Fedha, pesa hizi ambazo Mheshimiwa Rais amesema ziende kilimo Shilingi Bilioni 150 mkazitoe ziende na Mheshimiwa Rais anamaanisha kama hamzazijua rangi zake basi Wizara ya Fedha safari hii kama hamjapeleka fedha hii bilioni 150 mtaona rangi halisi za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili nataka nizungumzie suala la Benki ya Kilimo. Tunahitaji Benki ya Kilimo katika Mkoa wa Ruvuma. Ninaomba sana leo hii nazungumza hapa kuhusiana na suala la Benki ya Kilimo nataka nitumie lugha ya kudemka, msituchukulie kwamba kazi yetu kudemka, leo nachangia hapa nimeshauliza maswali mengi ni kama siku ya 13 ninachangia suala hili la Benki ya Kilimo, ninaomba Benki ya Kilimo ipelekwe katika Mkoa wa Ruvuma kwa sababu zifuatazo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Ruvuma ni Mkoa ambao ni Benki ya Chakula, tunawahakikishia tutashika nafasi ya tano katika uzalishaji wa mazao ya nafaka. Ni wazi kwamba Mkoa wa Ruvuma unachangia pato kubwa sana katika Pato la Taifa, linachangia fedha nyingi sana kupitia suala la kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine wakulima wangu wanalima kwa kutumia majembe ya mkono mpaka sasa hivi pamoja na kuwa tumekuwa tukiongoza na ni benki ya chakula, kwa nini Wizara ya Kilimo msitupelekee Benki ya Kilimo katika Mkoa wa Ruvuma? Tunahitaji Benki ya Kilimo na niseme Mheshimiwa Bashe kupitia hili suala la Benki ya Kilimo nimechoka kuzungumza ndani ya Bunge hili na ninakuambia kabisa ninakusudia kukamata shilingi ya yako kuzuia bajeti yako isipitishwe, endapo kama utakapokuwa unakuja hapa una-windup, huna maneno mazuri yatakayo-stimulate wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kupata Benki ya Kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo maneno yapita yanasema kwamba ooh! Benki ya Kilimo, tumeshakopesha huko, nenda kaone wapi, tunataka iandikwe pale kama ilivyoandikwa benki nyingine Microfinance Bank tunataka iandikwe pale Benki ya Kilimo, Mkoa wa Ruvuma. Wananchi waingie pale, anayekuwa na shamba dogo la heka tano akakope, mwenye shamba la heka 10 akakope, badala ya hizo blaah! Blaa! za chini ya pazia, tunahitaji Benki ya Kilimo, unahitaji degree ngapi kujua kwamba Mkoa wa Ruvuma kuna umuhimu wa kupeleka Benki ya Kilimo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana nilitaka kupanda juu ya meza...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)