Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Hon. Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Spika, ahsante, sina budi kwanza kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuipongeza na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Waziri wao na watendaji wote ambao leo wamewasili hapa ili kuangalia mwenendo wa bajeti yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nilikuwa nataka nizungumzie ukosefu wa hati miliki katika kambi zetu. Ukosefu wa hati miliki katika kambi zetu ndiyo unaoleta migogoro baina ya jeshi na wananchi. Utawakuta wananchi wanakwenda kuvamia sehemu za jeshi, wakati sehemu zile hazina hati miliki sehemu ni za jeshi lakini hati miliki hawana na hawafuatilii kuzitafuta matokeo yake watu wanalima, wanajenga, migogoro inaanza wanaanza kuvutana baina ya Jeshi na wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mfano; ukija Kambi ya Ubago iliyopo Zanzibar, Unguja Ukuu iliyoko Zanzibar na baadhi ya kambi nyingi hukuhuku Tanzania Bara. Pia nina wasiwasi kama kambi yangu ya Mtoni au Mazizini zimezungukwa na raia/wananchi na bado wanapenya wanaingia. Utakuta hakuna uzio, kuna msitu na ule msitu mtu anaweza akapenya, sasa na hilo waliangalie, watafute mbinu kupatikane hati miliki waweze kudhibiti sehemu zao kuondoa mgogoro baina ya jeshi na wananchi wakaiingize na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nataka kuzungumzia suala la Sera ya Ulinzi wa Taifa. Toka Bunge la Tisa, la Kumi, la Kumi na Moja na la Kumi na mbili kelele ndiyo hizo hizo. Lakini tushukuru hili Bunge la Kumi na Mbili taarifa iliyokuwepo tayari kwa sababu walikuwa wanazungumza kwamba bado kwamba Serikali ya Zanzibar haijatoa maoni yao, wadau hawajatoa maoni yao na sasa hivi tayari wadau wameshatoa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshatoa. Je, itaanza kutekelezwa lini? Maana yake sera ikifanyakazi ndipo jeshi litakapozidi kuimarika, kwa wafanyakazi na jeshi lenyewe. Lakini bila kuwa sera kufanyakazi inamaana ipo ndani vitabu au ndani ya mafaili itakuwa bado utekelezaji wake haujaonekana, bado elimu haijatolewa na bado wananchi watakuwa hawajafahamu nini kinachoendelea. Hatutaki kwamba mambo yao ya siri yatoke, tunataka yale yaliyokuwa ni wajibu ambao kila mmoja ayatambue aweze kuelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikija na hili la mashirika haya, Shirika la NYUMBU na MZINGA. Haya mashirika ni mazuri, yanazalisha lakini kwanza wana upungufu wa wafanyakazi na hao wafanyakazi waliopo pale wawe na utaalam kwa sababu sehemu ile inafanyakazi ya kitaalam; bila ya kuwa na wataalam haitaweza kuzalisha kama anavyofikiria. Ina uhaba wa rasilimali watu na hao watakaoajiriwa wawe wataalam waweze kufanyakazi za kuweza kutambulika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la umwagiliaji maji; wanacho kilimo cha umwagiliaji maji, tulikwenda tukaona Chita, wapo vizuri wanalima, kuna samaki wazuri, watamu maana tulipewa tukala. Lakini tatizo lililopo pale hawana vitendea kazi vya kisasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)