Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Hon. Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na kukupongeza kwa kazi nzuri. Pia naomba kipekee nimpongeze Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, naomba kwa fursa hii nichangie kwenye hoja ya bajeti ya Wizara hii muhimu ya Ulinzi na Jeshi ya Kujenga Taifa na naomba niongelee unyang'anywaji wa mashamba Kijiji cha Luwa na Jeshi la Kujenga Taifa Kambi ya Luwa.

Mheshimiwa Spika, Jeshi limenyang'anya wananchi mashamba mnamo mwaka 2017 na mpaka kati ya jeshi na wananchi ni Mto Sopa lakini jeshi limevuka hadi kufika barabara ya mkoloni kuelekea Rukwa na kuchukua mashamba ya wananchi wa Kijiji cha Ntendo, Luwa na Fyengelezya.

Mheshimiwa Spika, kipindi mashamba yananyang'anywa, kuna mali ziliharibiwa sana kwani walipewa muda mfupi kuondoka eneo hilo. Kuna mifugo ilikufa (ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku na bata), pia kulikuwa na matanuli yaliyochukuliwa, nyumba tatu, mabanda ya mifugo, mazao ya kudumu ambayo ni matunda aina mbalimbali vipo shambani, majenereta na vifaa vya kilimo.

Mheshimiwa Spika, katika operation hii hakuna maongezi zaidi ya kuondolewa licha ya barua nyingi zilizoandikwa Serikalini bila majibu ya kuridhisha. Ushahidi ni nyumba zilizobaki pale maana hadi leo zipo.

Mheshimiwa Spika, nimuombe Mheshimiwa Waziri atoe majibu na afuatilie suala hii na kutupatia ufumbuzi wa mgogoro huu.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja.