Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Hon Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote nikushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia hoja iliyoko mbele yetu asubuhi hii.

Kwanza niungane na Waheshimiwa Wabunge wote ambao tumeona walio wengi kwa kweli wamechangia very positively kuhusu kazi nzuri ya ulinzi wa Taifa letu unaofanya na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na kwa kweli, hii kama alivyomaliza mzungumzaji wa mwisho, ni kazi nzuri na miongozo mizuri inayofanywa na Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri wangu wa Ulinzi Dkt. Tax, lakini Katibu Mkuu, Wakurugenzi, Wakuu wa Majeshi na wasaidizi wake wote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja nyingi zimezungumzwa hapa na Waheshimiwa Wabunge, katika kuchangia naomba na mimi niseme machache yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, moja kuhusu umuhimu wa barabara za mpakani; hili kweli Serikali inajua umuhimu wake. Wizara ya Ulinzi na JKT itawasiliana na wenzetu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa madhumuni ya kuimarisha barabara hizi za mpakani. Hoja imezungumzwa ya kuweka lami, lakini nadhani jambo la msingi hizi barabara zote zianze kupitika halafu ziimarishwe kuwa barabara za lami. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja iliyoibuliwa na Mheshimiwa Ng’enda, tunashukuru moja umeisema, lakini nilitaka nichangie hii ya doria katika Ziwa Tanganyika, lakini pia tuseme na maziwa mengine hata na bahari yetu.

Mheshimiwa Spika, kwenye hili jeshi letu liko imara, lakini litaimarisha ushirikiano na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ikiwemo polisi na vyombo vingine, ili kuimarisha doria kwenye maeneo hayo. Tusingependa kuona wananchi wetu wanadhalilishwa na wahalifu au kama alivyowaita majambazi au maharamia kutoka nchi za jirani, lakini pia nikiri wapo hata miongoni mwa wananchi wa Tanzania wanaofanya vitendo hivi vya uhalifu, wote hawa wanahitajika kudhibitiwa.

Mheshimiwa Spika, hili la nyimbo za kizalendo majeshini; tunaimarisha hilo sana. Zinaimbwa nyingi ila nyingine akiziona ni za hamasa tu. Na tunashukuru umetusaidia kwamba kuna mazingira fulani fulani ili waweze kufanya mazoezi hayo kwa ufanisi wanahitaji nyimbo zinazogusa hisia kama hizo ambazo Mheshimiwa Ng’enda alitaka kama vile kuzinyanyapaa.

Mheshimiwa Spika, mwisho ni hili la ajira; naomba nichangie kwenye hili la ajira; imeelezwa hapa, lakini nataka niseme kwa kweli, ajira si kwamba iko restricted kwa Jeshi la Wananchi tu, wale wanaopitia JKT. Hiki ni kigezo muhimu kwa sababu, tunazungumzia uzalendo, utayari, uchapakazi na JKT ndio hutoa mafunzo ya namna hiyo. Kwa hiyo, sio Jeshi la Wananchi tu wanaolazimisha waajiriwa wao wapite huko, bali hata Polisi mmeona tumesema juzi hapa, Magereza pia, Uhamiaji, wote wanakuwa wamepitia huko, lakini hata taasisi za kiraia pia wanapitia huko.

Mheshimiwa Spika, baada ya maneno hayo sasa naomba niunge mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)