Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Nami namshukuru Mungu kwa kunipa uwezo leo hii nikasimama hapa kuchangia katika hotuba hii ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nawapongeza sana Mheshimiwa Waziri Comrade Nape Moses Nauye na timu yake kwa jinsi anavyofanya kazi nzuri ya kutoa huduma katika Wizara hii. Kazi yake inapimika, inaonekana na inaeleweka na ipo wazi kabisa kila mtu anaona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuzungumzia kazi kubwa sana iliyoweza kufanywa na mfuko huu wa UCSAF, Mawasiliano kwa Wote. Mfuko huu umefanya kazi kubwa hasa kwa upande wa Zanzibar. Umeweza kusimika minara 42 iliyotiwa mkataba tarehe 20 Januari na mpaka sasa hivi kwa mujibu wa ripoti ya juzi aliyokwenda kufanya ziara Mheshimiwa Waziri, minara 38 imeshakamilika. Hiyo ni muda kama wa miezi minne. Itakapofika mwezi Juni tunategemea minara yote hii itaweza kuwa tayari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, minara hii itaweza kuleta excess kwa sehemu ambazo sisi kwa lugha yetu Kiingereza tunaita very remote places, kama Fundo, Nungwi kule mwisho, Msuka, Kwa Pemba, Chaani, Unguja, kote huko minara hii itakamilika, kwa hiyo, italeta mawasiliano kwa urahisi kwa wananchi wetu na kutuweka Tanzania katika huduma ya endelevu kidijitali. Hapo nawapa kongole sana watu wa mfuko ambao wamefanya kazi nzuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwamba tunategemea hiyo minara hiyo mingine 119 ya huku Bara itakamilika, lakini haya yote pia nitoe pongezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa elekezo lake lililoelekeza kwamba kusiwe na ucheleweshaji katika kutoa vibali vya kukamilisha kazi hizi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Dkt. Hussein amefanya vizuri na nchi yetu inakuwa communicated kidijitali. Namshukuru sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi hii nzuri pia imeweza kufanikishwa kwa juhudi za pamoja za mfuko na pamoja na Zantel na zikifanywa vizuri pia na contractor wetu Helios Tower. Kwa hivyo nawapongeza sana kazi hiyo iliyofanywa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfuko huu pia umeweza kukamilisha vituo vya TEHAMA katika wilaya 10 za Zanzibar na wilaya 11 inakamilika. Na vilevile mafunzo yanatolewa ya matumizi haya ya TEHAMA kwa Masheha wote na watu wote na vituo hivi vipo karibu na watu kwa hivyo vitakuwa access kirahisi na watu. Kwa hiyo, ni kazi nzuri inayofanywa na mfuko huu, kwa sababu hiyo pia naona kwamba mfuko huo uweze kuongezewa fedha ili uweze kufanya vizuri zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo jingine ambalo ni la muhimu vilevile ni hili la kuhakikisha kwamba mfuko huu umeweza kutengeneza kitu cha milio ya dharura ambao unaweza kupiga 190 na Kituo hichi kipo Kiembesamaki na kinafanya vizuri. Mtu unaweza ukapata shida baharini, ukapata ajali, ukapata ugonjwa ukapiga hapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine liliofanywa na Wizara hii ni kuhakikisha kwamba kuunganisha tiba kwa kupitia TEHAMA kwa mtandao, kwa mfano Abdalla Mzee itaunganishwa moja kwa moja na MOI, Jakaya Mrisho na Muhimbili kwa hivyo itapunguza gharama kwa Serikali na wananchi wenyewe kwa kusafiri kwenda kutafuta huduma. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo nchi yetu kila kukicha inakwenda kupaa zaidi kidigitali. Na haya yamesemwa jana pia na Mheshimiwa Rais Mama yetu alipokuwa anasema kwamba katika siku zijazo za mbele tutajikuta Tanzania imepaa zaidi kimaendeleo. Na maendeleo hayawezi kuja kama huna tekonolojia kwenye TEHEMA na kwenye digital na jambo hili limeshikwa vizuri sana Wizara hii, tunatoa hongera sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tunaweza kupata mawasiliano kwa kupitia Televisheni zetu zote ambazo zinafanya vizuri na tunashuhudia na hapo ndiyo tunaweza kupata taarifa ya Habari. Nchi haiwezi kuendelea kama haiwezi kupata taarifa za Habari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu anuani ya makazi.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Asha Juma.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Naam.
MWENYEKITI: Kengele imeshagongwa.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Sijaisikia, samahani; naunga mkono hoja. (Makofi)