Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio na Mapato ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Hon. Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio na Mapato ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia katika Wizara hii muhimu ya Teknolojia ya Habari kwa ujumla. Kwanza ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Nape pamoja na Mheshimiwa Naibu Waziri Engineer Kundo kwa namna ambavyo Wizara hii wanaisimamia kwa karibu sana, wote tunashuhudia utendaji wao wa kazi kwa karibu na mimi ninawatakia kila la kheri na sisi wa Kishapu tutaendelea kuwaunga mkono kuona kwamba jitihada na juhudi mnazozifanya tunapeana ushirikiano wa karibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ni jambo zima la uanzishwaji wa kitengo cha mawasiliano ambacho kimeanzishwa na Wizara hii na mwezi wa Julai nadhani kinatarajia kuanza rasmi. Kwanza, niwapongeze kwa sababu ni utaratibu mzuri tumeshuhudia kupitia Msemaji wa Serikali Ndugu yetu Msigwa upashanaji na utoaji wa habari kwa umma umekuwa wa hali ya juu na watanzania wamekuwa wakielewa nini Taifa linatekeleza majukumu yake katika masuala mbalimbali Mtambuka. Sasa jambo hili ni jambo la muhimu sana lakini kitu ambacho ninataka nichangie ni kuhusiana na upungufu, ama uhaba wa watumishi hasa katika eneo hili la Kitengo cha Mawasiliano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu katika Halmashauri zetu 185, Halmashauri 100 peke yake ndizo zina Wakuu wa Idara hii ama Wakuu wa Vitengo hivi, Halmashauri zaidi ya 85 mpaka 86 hazina wakuu hawa wa vitengo hivi. Kwa hiyo, hii ni changamoto kubwa, kama Wizara ina dhamira ya dhati kuhakikisha kwamba vitengo hivi vifanye kazi zake vinavyotarajiwa kwa uhakika, haiwezekani kama hatutafanya jitihada za haraka sana kuona kwamba suala la kuhakikisha kwamba watumishi hawa wanajitosheleza katika Halmashauri linafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo. Kwa hiyo, ushauri wangu Wizara ifanye kazi ya ziada na kwa haraka zaidi kuhakikisha kwamba watumishi hawa wanajitosheleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kwamba kwa sababu katika Halmashauri tuna baadhi ya watumishi ambao fani zao ama wamejiendeleza katika eneo hili la Habari, kuna haja ya kufanya recategorization katika Halmashauri zetu kwa haraka zaidi ili Watumishi tulionao katika ngazi za Halmashauri waweze ku-cover maeneo haya ambayo yana matatizo na mapungufu ya aina hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna haja ya kufanya recategorization katika Halmashauri zetu kwa haraka zaidi ili watumishi tulionao katika ngazi za Halmashauri waweze ku-cover maeneo haya ambayo yana matatizo na upungufu wa aina hiyo. Kwa hiyo, nilikuwa naishauri sana Wizara iliangalie hili kwa mapana ilimradi lifanyiwe kazi kwa haraka zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, kwa sababu, tunaye msemaji wetu, kama nilivyozungumza Ndugu Msigwa na amekuwa akifanya kazi kubwa sana, nashauri ifanyike jitihada kubwa ya Wizara kuhakikisha kwamba inatoa mafunzo ya kutosha kwa hawa Maafisa Habari ili nao wawe na uelewa wa kutosha na waweze kuwa wanatoa taarifa hizi katika ngazi za Halmashauri kwa wakati ili Umma wa wananchi katika ngazi za Halmashauri wawe wanaelewa Halmashauri inatenda mambo gani na kwa wakati gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ipo changamoto kubwa ambayo nilikuwa nataka nishauri kuhusu nguvu ya kisheria, kwa sababu katika ngazi za Halmashauri wanaokuwa wasemaji katika ngazi za Halmashauri ni Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi wa Halmashauri. Kwa hiyo, hawa wasemaji wanakuwa wasemaji tu labda katika mitandao ama wakati mwingine wanasimamia tu vitengo vile kwa ajili ya kutafuta Waandishi wa Habari ili waje wachukue habari katika mabaraza yetu. Kwa hiyo, sasa nilikuwa naomba Wizara iweke utaratibu na mpango kabambe wa kuhakikisha kwamba inakuja na nguvu ya kisheria ili kuwapa mamlaka hawa wawe wasemaji katika Halmashauri zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la mawasiliano na hasa simu. Kata ya Mwakipoya, Kata ya Mwasubi, Kata ya Masanga, Kata ya Somagedi, Kata ya Mwamalasa na Kata ya Itilima ni kata ambazo zina changamoto ya mawasiliano. Mheshimiwa Kundo aliwahi kuahidi kufika kwenye jimbo langu na kuja kuona changamoto hiyo. Kwa hiyo, kata hizi sita zina matatizo makubwa. Nilikuwa naomba sana kata hizi zipate huduma ya mawasiliano. Nimeona katika taarifa ambayo moja kati ya maeneo ambayo yanaenda kupata huduma hii, lakini maeneo haya bado yana changamoto. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, usikivu wa TBC bado ni tatizo kubwa katika Wilaya ya Kishapu. Naomba sana Wizara ifanye kazi kubwa kuhakikisha kwamba redio hii iwe inasikika kwa wananchi kwa sababu ni redio mama, na inatoa taarifa muhimu, mtambuka kwa ajili ya Serikali yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Naunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)