Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio na Mapato ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Hon. David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio na Mapato ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa hotuba nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha kwako maombi ya Wanamufindi kukuomba upatikanaji minara kwenye maeneo yenye kero kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kuomba minara ya simu maeneo yafuatayo; Kata ya Maduma, Kata ya Kasanga Makao Makuu ya Kata, Kata ya Kiyowela, Kata ya Makungu sehemu za Kitasengwa, Kata ya Igowole sehemu za Kisasa na Ibatu na Kata ya Nyololo katika baadhi ya sehemu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna maombi ya kompyuta ili kuunga mkono sera yetu ya Make Mufindi Digital. Niombe kompyuta 500 kwa ajili ya shule 10 za kuanzia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.