Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio na Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Hon. Capt. Abbas Ali Mwinyi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Fuoni

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio na Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

MHE. CAPT. ABBAS ALI MWINYI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ni muda mchache sana yaani si rahisi kumaliza hoja ambazo ninazo kwenye meza.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili nami nichangie katika hoja iliyopo usoni kwetu. Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujaalia afya na uzima na kwa wale ambao wana changamoto ya maradhi, basi Mwenyezi Mungu awaponye. Amina.

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu kwa siku ya leo nitajielekeza katika taasisi ambazo ziko chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi. Zipo nyingi sana na Taasisi zote hizo nina jambo la kusema juu yake, lakini kwa kuwa muda ni mfupi sana nitafikia pale ambapo…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Abbas maelekezo ya kiti yameletwa kwa wote ni kumi kumi. (Makofi)

MHE. CAPT. ABBAS ALI MWINYI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Basi kwa kuwa ni dakika 10 nami nichukue fursa hii adhimu na adimu kabisa ya kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza vyema yote yale ambayo mtangulizi wake aliishia. Vile vile niwashukuru viongozi wote wengine wa kitaifa Makamu, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri Mkuu na wote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa usafiri wa majini na baharini siyo jambo la Muungano, kwa hiyo hapa kwetu Tanzania kuna mamlaka mbili ambazo zimepewa majukumu za kuendesha mamlaka hizo. Kuna mamlaka ya ZMA (Zanzibar Maritime Authority) ambayo iko Zanzibar, lakini vile vile kuna TASAC ambayo iko Tanzania Bara. Kwa hiyo maeneo haya mawili, Mashirika haya mawili au mamlaka haya mawili yanafuata sheria tofauti, kwa upande wa Tanzania Bara kuna Match & Shipping Act. lakini kwa Zanzibar kuna Maritime Transport Act. Sasa katika maeneo haya au mashirika haya mawili au wadhibiti hawa kila mmojawapo amepewa majukumu maalum na yameainishwa katika sheria. Kwa hiyo mipaka inajulikana na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa katika suala zima la uendeshaji wa mamlaka hizi, masuala haya yote ya baharini yanapaswa kuendeshwa na mamlaka kama nilivyosema awali. Kuna wakaguzi ambao wamekuja kutoka Shirika la Bahari la Ulimwengu ambao wamekuja kufanya utafiti na kutukagua katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hilo Shirika la Umoja wa Kimataifa la Mabaharia walitupa majukumu ya kwenda kukagua flag state obligation (majukumu ya nchi yaliyopewa usajili wa meli ambayo ndiyo ZMA) lakini na vile vile kulikuwa na Flag State Obligation ambayo majukumu haya yalipaswa kufanywa na nchi ambayo imesajili meli zenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna coastal voyage obligation ambayo anapewa nchi ambayo ina maeneo ya mwambao. Kwa hiyo majukumu haya yamekuwa haya ya mwambao walikuwa wamepewa hawa watu wetu wa upande wa Tanzania Bara kwa maana ya TASAC. Sasa kinachoelekea ni kwamba hii IMO (Umoja wa Ukaguzi wa hayo Mashirika) umetuelekeza ya kwamba lazima ukaguzi uendane na matakwa ambayo wao wanayataka.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kulikuwa na mapungufu yafuatayo na mapungufu hayo ambayo tumeelekezwa tuyafanye na hiyo Kamati ya IMO – International Maritime Organization ni mengi na tunatakiwa kwamba tuyatafutie suluhu. Yapo maeneo ambayo inabidi tuyatekeleze kwa pamoja yaani kati ya TASAC na ZMA lakini yako ambayo ZMA inatakiwa ifanye kivyake, na TASAC inaweza kufanya kivyake kwa hiyo hayo ndiyo maeneo ambayo yanatakiwa kuzingatiwa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Abbas wewe ni Captain wa Boeing, Captain wa Dreamliner, Captain wa Air Bus, tusaidie mengine viwanja vilivyo, matatizo ya ILS, matatizo ya vertical approach, slope indicators…

MHE. CAPT. ABBAS ALI MWINYI: Mheshimiwa Naibu Spika, hapana! Katika kutekeleza hayo ambayo nimeyasema nataka nimuulize Mheshimiwa Waziri yafuatayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Je, ameunda Kamati ya Kitaifa ambayo inatakiwa ilete majibu kwa yale yote ambayo tumeelekezwa na IMO waweze kuyatekeleza? Tunataka kujua hayo kwa sababu Kamati hiyo ya kitaifa ndiyo ambayo ina majukumu ya kuweza kutusaidia kwa pande hizi mbili za Muungano. Hali kadhalika, Tanzania Bara katika yale mambo ambayo tumeambiwa tuyafanyie marekebisho na IMO - Shirika la Bahari Duniani, kuna maeneo ambayo tumeambiwa lazima tuyafanyie marekebisho, lazima tuwe na pande mbili za Bara na Visiwani ambavyo wafanye hayo mambo kwa umoja wao. Sasa Je, kuna Kamati ya Kitaifa ambayo imeundwa na Mheshimiwa Waziri katika kuhakikisha yanatatuliwa hayo?

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ambalo napenda kusema ni kwamba kwa upande wa Zanzibar mamlaka zote hizo imekuwaje na kwamba zinasaidiana vipi, hilo tunataka kujua kwamba je, kuna action plan yoyote ambayo Mheshimiwa Waziri ameunda kwa lengo la kuhakikisha kwamba yale mapungufu tuliyokutana nayo yamepata suluhisho, kwa sababu findings kwa maana ya kwamba mapungufu yameonekana 20 na maangalizo matatu, kuna utaratibu gani wa kuhakikisha ya kwamba tunapata majibu ya hayo ambayo tumeambiwa tuyafanye kwa sababu tumepewa miaka minne ya kuyarekebisha hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hawa Wakaguzi watarudi mwaka 2023.

NAIBU SPIKA: Ahsante Captain Mheshimiwa Dkt. Abbas kwa mchango mzuri.

MHE. CAPT. ABBAS ALI MWINYI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naunga mkono hoja ahsante.