Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio na Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Hon. Salim Alaudin Hasham

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ulanga

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio na Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

MHE. SALIM A. HASHAM: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwenye Bunge lako lakini pia namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya ya kuweza kusimama tena kwenye Bunge lako Tukufu kuchangia kwenye Wizara ya Ujenzi.

Mheshimiwa Spika, pia niwashukuru sana nani wapongeze, nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa kazi kubwa anayoifanya lakini pamoja na kwamba anafanyakazi kubwa sisi Wabunge humu ndani hatutaacha kusema kwasababu changamoto bado ni nyingi na sisi humu wote tunawawakilisha wananchi zaidi ya milioni 60. Kwa hiyo, tupo kwaajili ya kuwasemea wao kwa hiyo, tutaendelea kusema. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, barabara yangu ya Ifakara kwenda Mahenge yenye urefu wa kilometa 68 ilifanyiwa upembuzi yakinifu mwaka 2013 na ikaingizwa kwenye Ilani ya Chama mwaka 2015 miaka mitano ile ilipita bila mafanikio yoyote na mwaka 2020 pia ikaingizwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi tunaangalia ndani ya miaka mitano hii Mheshimiwa Mbarawa utakuja kutufanyia nini.

Mheshimiwa Spika, kiukweli kilio cha barabara ya Mahenge – Ifakara yenye kilometa 67 ni kilio kikubwa sana kwa wananchi wa Ulanga sisi tunaokaa jimboni kwa muda mrefu ndiyo tunajua adha yake ikifika masika ukisikia barabara sehemu imekatika watu hawapiti inamaana na wewe Mheshimiwa Mbunge hata kama unasafari zako huwezi kupita kwasababu huna cha kuwaambia wananchi wako. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukifika pale cha kwanza wao wataanza matusi yao watasema tu Mheshimiwa Mbunge yupo tumemchagua analala tu Bungeni. Sisi kila siku kazi yetu ni kuwasemea wananchi hawa tunaomba Mheshimiwa Waziri mtuangalie barabara ile kama mwaka huu kwenye hotuba yako utakuja kututaja na sisi tutakushukuru sana Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Morogoro ni Mkoa wa kimkakati na kila kiongozi mkubwa wazee wetu wangekuwa mzee wangu Kabudi hapa angesimama angeweza kuuelezea Mkoa wa Morogoro kwa upana sana. Mkoa wa Morogoro ni Mkoa wa kimkakati, Mkoa wa Morogoro umeme unaotumika Dar es Salaam unatoka Mkoa wa Morogoro lakini Mkoa wa Morogoro ndipo ambapo kuna kiwanda kikubwa cha sukari, Mkoa wa Morogoro watu wanalima kwelikweli lakini Mheshimiwa Kabudi anaujua sana Mkoa wa Morogoro lakini Mkoa wa Morogoro bado tumesahaulika sana. Sisi mpaka leo wilaya zetu hazijaunganishwa kwa lami wala mikoa yetu haijaunganishwa kwa lami kuna barabara tatu tu Mheshimiwa Waziri za kimkakati kwenye Mkoa wa Morogoro. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, barabara ya kwanza ni ya Mahenge kwenda kutokea Liwale ambayo inaunganisha mikoa ya kusini kwa maana tutakuwa na uwezo wa kufika haifiki kilometa 100 Mheshimiwa Waziri tunao uwezo wa kufika Lindi, Mtwara na sehemu zingine huko lakini barabara ya pili ni barabara Malinyi kwenda kutokea Songea ambayo tutakuwa tumeutoboa Mkoa wa Morogoro ambayo imeanza kujengwa tangu enzi ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ndiyo alikuwa ameizindua barabara ile lakini mpaka leo hatujui muendelezo wake ni nini. Barabara ya tatu Mheshimiwa Waziri ni barabara ya Mlimba kwenda Njombe ni barabara za kimkakati mkitusaidia barabara hizi mtakuwa mmetusaidia sana Mkoa wa Morogoro. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wilaya zetu zote hazina lami kwa hiyo, tunawaomba sana Mheshimiwa Waziri na Mama yetu anatusikiliza Mkoa wa Morogoro ni Mkoa wa Kimkakati mkoa ule una mambo mengi sana ni muhimu katika Taifa hili kwa hiyo, tunawaomba sana mtujengee barabara yetu tunashukuru barabara ya Kilombero kwenda Ifakara inaendelea kwa kasi na inaendelea kujengwa mkituunganisha na zile 67 pale sisi tutakuwa tumepona sana.

Mheshimiwa Spika, pia wewe ni shahidi mwaka jana Serikali ilisaini mkataba na kampuni moja kubwa sana ya uchimbaji inaenda kufanya uchimbaji kwenye jimbo langu imeenda kuwekeza zaidi ya dola milioni 200 kwenye lile jimbo ile kazi inaenda kufanyika pale kama barabara haitatengenezwa ule mradi hauwezi kufanikiwa kwasababu magari yatakayokuwa yanapita pale ni magari makubwa tunawaomba sana muende mtusimamie hilo muweze kwenda kulifanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, baada ya hayo naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)