Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa Duniani na kupewa Tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu

Hon. Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa Duniani na kupewa Tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, na mimi nichukue nafasi hii kuwaomba Wabunge wote kabisa tumpongeze Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwanza kabisa ametuheshimisha sana wanawake wa Tanzania na wanawake wa Afrika. (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Spika, kwanza hata katika teuzi ametuheshimisha, yaani ni kiongozi ambaye amesimama na kuona kwamba binadamu wote, wanaume na wanawake tunaweza tukafanyakazi. Pia tuangalie katika suala la miundombinu, miundombinu hii itawasaidia sana wanawake katika suala la uchumi. Kwa hiyo, ametuheshimisha kuona kwamba miundombinu yetu sasa inaendelea kukua vizuri na inaendelea kuboreshwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine ambao Mheshimiwa Rais anastahili pongezi ni suala linalohusiana na eneo la afya. Mheshimiwa Rais amejipambanua sana kuona kwamba katika hospitali zetu, hasa maeneo ya wanawake kujifungua na watoto wadogo kupata huduma, amehakikisha kwamba zanahati zetu na vituo vya afya sasa hivi maeneo yote ukienda lazima yawe na sehemu ya wanawake kujifungua salama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mimi nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri sana anayoifanya upande wa miundombinu, afya na hata elimu. Kwa hiyo, anastahili pongezi na niwaombe Wabunge wote tuendelee kumtia moyo Mheshimiwa Rais, tumpongeze ili aendele kuboresha maeneo haya yote kwa manufaa ya wanawake na wanaume wote wa Tanzania, ahsante sana. (Makofi)