Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa Duniani na kupewa Tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu

Hon. Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa Duniani na kupewa Tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa hii. Na mimi kwa niaba yangu binafsi lakini kwa niaba ya Watanzania nipende kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan kwa kweli kwa utekelezaji wa majukumu yake na hasa kwa tuzo kubwa aliyoipata. Tunaweza kuwa na changamoto ndani ya nchi lakini tunavyotoka nje hili ni la kupongeza kwa kweli kwa kupata tuzo hii. Ni sifa kubwa ametuletea Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuzo hiyo ya miundombinu ambayo ameipata; wananchi wengi mnaona changamoto ambazo tunazipata katika usafirishaji hasa wanawake katika kutatua changamo zao. Kwa hiyo tunapongeza sana kwa kupata hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na hiyo amekuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 100. Kwa kweli ni kitu ambacho ni cha kupongeza sana, haijawahi kutokea. Lakini mama huwa anajali familia na anajali nje ya familia. Tunaona kwa vitendo jinsi ambavyo anafanya, tumeona Mheshimiwa Rais amejielekeza katika maendeleo ya watu, na tunaona katika sekta ya afya Rais anakwenda kujenga hata hospitali kubwa kwa ajili ya akina mama na Watoto. Hili ni jambo la kupongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwenye elimu ameangalia kila mkoa kwa kuhakikisha kwamba tunapata shule za wasichana. Hii itasaidia sana wanawake kuwa kuwa katika maamuzi katika maeneo mbalimbali. Tumeona pia kwenye sekta ya maji miradi mingi ya maji imeanzishwa, mingi inalenga kutimiza ile asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini. Lakini pia mama ameleta mapinduzi katika kilimo, tumeona katika bajeti hii jinsi ambavyo amefanya. Cha muhimu ni kwamba fedha zikitoka tutaona matunda yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, licha ya hivyo tumeona mahusiano yake na mataifa ya nje. Ameonesha katika ziara zake anazokwenda ametoa fursa mbalimbali za kiuchumi na tunaona fursa za kiuchumi zinakuja katika nchi yetu. Ameimarisha mahusiano na nchi za nje, kwa mfano tumeshuhudia amehudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa ambako alikwenda kuhutubia kwa umahiri mkubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia tumeona alihudhuria Mkutano wa Glasgow ambako kuna masuala ya mabadiliko ya tabianchi. Huku tunaona ndiko gumzo kubwa sasa linalotokea katika mabadiliko ya tabianchi. Amehudhuria pia katika maonyesho ya kibiashara ya Dubai (Dubai Expo) ambapo wafanyabiashara wakubwa ulimwenguni wanakuja. Hili nalo limeleta umaarufu wa nchi yetu lakini tunajitoa kibiashara ili wananchi waweze kuja kuwekeza nchini kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini alifanya ziara nchi za Ulaya, Ufaransa, na Ubelgiji. Hii yote ni kutanua wigo kuhakikisha wananchi wanaiona hiyo. Vilevile, umaarufu wa Royal Tour; kwa wale ambao wanaangalia sinema, ile tamthilia ya revenge kwenye king’amuzi cha Azam, jana Mellan alimwambia mchumba wake nikufanyie nini? au nikupeleke Tanzania. Kwa maana hiyo inaonyesha jinsi ambavyo ziara hii jinsi ambavyo ziara ya Royal Tour ilivyozaa matunda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi ninadhani kwa miaka ijayo Mheshimiwa Rais pamoja na kwamba alienda Marekani akakutana na Makamu wa Rais, lakini miaka ijayo mwakani labda anaweza akapata tuzo ya watu 20 hivi chini ya hapo, ahsante. (Makofi)