Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa Duniani na kupewa Tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu

Hon. Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa Duniani na kupewa Tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia hoja hii iliyopo mbele yetu. Kwanza kabisa kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Nyang’wale, tunaungana na Wabunge pamoja na wananchi wote kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan kwa tuzo ambayo ameipata na kuiletea heshima kubwa nchi yetu ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kweli Mama anaupiga mwingi na anaupiga mwingi kweli kweli. Hapa sasa kwa lugha ya Kisukuma kama naruhusiwa kusema, wanasema “shirikalewa mnzengo hatina mangaka.” Maana yake ni kwamba, Askari wa Kijijini kwenu huwa hatishi, lakini Mama ametisha Kimataifa mpaka kupata tuzo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tuendelee kumuunga mkono kwa mambo mengi aliyoyafanya kwenye miundombinu mbalimbali mfano ujenzi wa reli ya SGR, ujenzi wa bwawa la umeme, ujenzi wa madaraja, ujenzi wa miundombinu ya afya, ujenzi wa miundombinu ya kilimo na mambo mengine mengi. Mama ameupiga mwingi ndiyo maana amepata tuzo, nasi kama Watanzania tuendelee kumuunga mkono mama yetu kwa kazi nzuri anazozifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sina mengi yakusema, kwa niaba ya sauti ya wananchi wa Nyang’wale na Wabunge na Watanzania wote tuendelee kumuuga mkono Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anazozifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)