Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa Duniani na kupewa Tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu

Hon. Ummy Hamisi Nderiananga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa Duniani na kupewa Tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA): Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, nilishukuru sana Bunge lako Tukufu kwa kupitisha azimio hili la kumpongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan. Ahsanteni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Serikali napenda nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan. Wabunge waliotangulia wamesema, nami niseme kwa lugha ya wenzetu, a leader is the one who lead the way and show the way. Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, ameyaonesha kwa vitendo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nirejee kipindi fulani nchi ya Marekani walipokumbwa na anguko la uchumi, walimpata Rais Franklin Roosevelt. Rais huyu aliwaonesha namna ya kufufua uchumi wa Marekani, akawaambia kwamba I will show you the new deal. Mheshimiwa Rais Samia ameichukua nchi kipindi ambacho tupo katika janga kubwa la corona. Uchumi wetu umeanguka lakini Mheshimiwa Rais Samia ametuonesha njia, tumepanda kwenye uchumi wetu uliokuwa umeanguka kwa asilimia nne, sasa tuko 5.2 na dhamira yake ni kuupeleka kurudi kwenye 6.8. Nani kama Rais Samia? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais Samia Saluhu tuzo hii aliyopewa ni ya heshima kwake, kwa Watanzania, kwa wanawake na dunia. Nchi yetu tunajivunia sana kwa uwepo wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu kwa kazi zake nyingi na kubwa alizozifanya Waheshimiwa Wabunge wamezieleza hapa, Mheshimiwa Rais kwenye elimu amefanya kazi kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwaalike pia wanaoendelea kutoa tuzo duniani kwenye elimu wamwone Mheshimiwa Rais Samia, kwenye afya wakitaka kutoa tunaye jemedali mpambanaji Mheshimiwa Rais Samia ambaye amefanya kazi kubwa na nzuri sana ya kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais Samia toka amepewa kazi ya Urais halali, anachapa kazi usiku na mchana, Watanzania tumemwona, tumefurahia kazi yake, amefanya kazi kubwa sana kwenye royal tour na watalii wameanza kuja na kuiunga mkono Serikali yetu. Kwa kweli sisi sote tumefurahi tumefarijika sana kwa tuzo hii ya heshima kwa Mheshimiwa Rais, tunamwombea kwa Mwenyezi aendelee kumlinda, ambariki kwenye majukumu yake ili aweze kuendelea kuwaletea Watanzania maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunaendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia, tunamwambia kazi iendelee na sisi tunaoamini katika uongozi wa hoja na kazi, tunasema kazi yake inaendelea vizuri, hongera sana kwa Mama, Mungu ambariki sana, ahsante sana. (Makofi)