Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa Duniani na kupewa Tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu

Hon. Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa Duniani na kupewa Tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Spika, awali ya yote ningependa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu ambaye ametufikisha siku ya leo, ambapo kwa ujumla wote tunaona Bunge bila kujali itikadi zetu za Vyama vya Siasa. Sote tunajadili ajenda kubwa ya kitaifa kuhusu suala hili la Mheshimiwa Rais. Hili jambo ni kubwa sana, Watanzania tuna kila sababu ya kujivunia. Heshima hii iliyotolewa kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watu waliipima. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukumbuke kwamba Rais alipopata majukumu haya ya kuiongoza Jamhuri ya Muungano Tanzania, Taifa lilikuwa limekabiliwa na ujenzi wa miundombinu mingi iliyokuwa inaendelea, ukiangalia ujenzi wa reli standard gauge, barabara zinazofunganisha mikoa katika maeneo mbalimbali, endapo kipindi kile Rais asingekuwa Rais mwenye msimamo, mwenye kujali watu, mwenye kujali mustakabali wa Taifa hili, Taifa lingeenda mahali pabaya sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki tunaona ujenzi wa reli ulivyoshika hatamu katika maeneo yote. Tukumbuke tulikuwa na kipande cha kwanza tu kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro na kipande cha pili toka Morogoro mpaka Makutupola, lakini tunaona jinsi gani hii kazi inavyoendelea kuiunganisha nchi yetu katika standard gauge. Pia kuna suala zima la ujenzi wa miundombinu hii tunayozungumza, leo hii tumeshuhudia suala zima la mkataba mkubwa wa ujenzi wa barabara ya ring road katika Mkoa huu na Jiji la Dodoma, tuna kila sababu ya kumpongeza sana Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, yapata wiki moja sasa imepita, tumemshuhudia Rais akiunganisha suala zima akizindua mradi mkubwa wa barabara unaounganisha Mkoa wa Singida na Mkoa wa Tabora, lakini Mkoa wa Tabora na Katavi, nani kama Mama Samia? Kungekosa udhibiti wa usimamizi wa maeneo hayo, hayo mambo tusingeyaona, lakini ukiangalia leo hii, watani zangu kule Wasukuma ukienda angalia lile Daraja la Busisi linavyojengwa kwa nguvu kubwa, hii yote ni kazi kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati Rais anashika majukumu haya, tunafahamu ujenzi wa Tanzanite Bridge pale Dar es Salaam ulikuwa unaendelea, bila yeye kusimama kidete tungeona wakandarasi wale wanaondoka site. Tumeshuhudia daraja limekamilika daraja limefunguliwa, nani kama Mama Samia? Tukumbuke barabara zinazotuunganisha katika maeneo mbalimbali ya barabara za TARURA ambayo bajeti yetu tumehama kutoka bilioni 280 mpaka leo hii kuzungumzia bilioni 803, nani kama Mama Samia? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii hata ukienda kule Mbuchi kwa ndugu zangu kule Kibiti watu waliokuwa wanahangaika nenda kaangalie daraja kubwa zaidi ya Shilingi bilioni sita, nani kama Mama Samia? Watu walikata tamaa, Rais asingekuwa na msimamo wa kusimamia miundombinu katika nchi yetu hii, hali yetu ingekuwa mbaya. Kwa kweli naomba niwaambie, hili jambo Mama ametuvisha nguo Watanzania, amefanya kazi nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kazi iliyoanzishwa na viongozi wa awali mpaka yeye alipoipokea, wakati ujenzi wa miundombinu hii ukishika hatamu kipindi cha Mkapa, wakati wa Kikwete, wakati wa Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli, yeye akaiendeleza kwa kasi, leo hii Watanzania tumevishwa nguo, tunaenda vizuri zaidi. Tuna kila sababu ya kuliombea Taifa letu, lakini tuna kila sababu ya kumwombea Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, ndugu zangu kuna kauli Wazaramo wanasema kanoga afile, watu hawasifiwi mpaka siku wametoka duniani. Leo hii tumeona dunia imemsifia Rais wetu akiwa hai, jamani! Katika hili niwaombeni Watanzania, jambo kubwa tuendelee kumuenzi na kumpa moyo Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kazi kubwa anayofanya, sidhani kama huyu mama analala, kwa hii kazi kubwa analiyoifanya tuna kila sababu kwa umoja wetu na kwa mapenzi yetu, tumwombee sana Rais Mama Samia Suluhu Hassan aendelee kuwatumikia Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii tunaona faraja kubwa aliyopata mpaka hata kwa watoto wadogo, hapa tumezungumzia miundombinu ya barabara lakini leo ukiangalia mradi wa Shilingi trilioni 6.5 ujenzi wa Bwawa la Nyerere linaloendelea, zaidi ya megawatts 2,115 itazalishwa, nani kama Mama Samia? Leo hii ukiangalia manunuzi ya ndege hata bajeti iliyopita jana hapa, tumepitisha bajeti ya ununuzi ya ndege mpya lengo ni kwamba ajenda ya utalii iendelee kutamalaki katika Taifa letu. Katika hili hata kama tuna upungufu wetu wa hapa na pale, lazima Taifa tuungane kwa pamoja kuliombea Taifa letu na kumwombea Rais wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukifanya hivi na kuondoa chuki zisizokuwa na sababu yoyote, tutalifikisha Taifa letu mbele. Hivyo, tusijiharibie sisi wenyewe, tunafanya vizuri. (Makofi)

SPIKA: Haya, ahsante sana.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na hongera sana dada yangu Katimba. (Makofi)