Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nianze kwa kuipongeza Wizara ikiongozwa na Dkt. Mabula na Mheshimiwa Ridhiwani. Pia niwapongeze watendaji waliopo kwenye hiyo Wizara Katibu Mkuu akiwa ndiye kiongozi. Sasa licha ya changamoto nyingi ambazo zimesemwa bado wanajitahidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajikita sana kwenye vyuo hivi vinavyohusiana na ardhi. Tuna Chuo cha Ardhi Tabora, kuna hiki Chuo kikubwa cha Ardhi hapo Dar es Salaam, kuna Nelson Mandela, kuna chuo kinaitwa UDSM, hivi vyuo vyote vinajihusisha moja kwa moja na ardhi. Sasa niseme hivi Serikali, niliongea wakati fulani, hivi Serikali wanaonaje wavitumie hivi vyuo katika kufanya research na kazi zinazohusiana na ardhi ili kupunguza upungufu huu wa wafanyakazi. Hivi vyuo vipo hapo lakini havitumiwi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilizungumza mwaka jana, ni kiongozi mmoja tu anaitwa Mheshimiwa Sagini wakati akiwa RAS, nami nikiwa RAS Tabora, alikuwa ndiyo anatumia kile Chuo cha Tabora kufanya kazi zake kule Simiyu. Leo hii mikoa ina changamoto nyingi lakini unakuta hivi vyuo hawavitumii; mpaka nikajiuliza au kuna kitu hawakiweki vizuri ndiyo maana hawawatumii hawa watu. Hebu watumie hawa wa Chuo cha Ardhi, MUST, Tabora, UDSM na Nelson Mandela, hasa katika maeneo ya IT kule Nelson. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nije niseme jambo lingine, niiombe Wizara ya Ardhi, wasaidiane au washirikiane na Wizara ya Fedha, Wizara ya Elimu na Ofisi ya Waziri Mkuu, kuona namna gani wataongeza bajeti hasa katika hiki Chuo cha Ardhi kwenye research. Sasa kutokana na idadi ya wanafunzi waliopata mikopo kuwa wengi na lilikuwa ni jambo zuri sana, kwa hiyo fedha za research zikapungua sana, hivyo, unakuta hawa wanafunzi wa Chuo cha Ardhi wanakwenda kwenye research wanafanya research kwa wiki moja; hivi kuna research kweli ya wiki moja kwa mwanafunzi. Kinachotokea ni nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba unisikilize, kinachotokea unajua ni nini? Watoto wale wana-copy au wanagushi researches za kwenye mitandao, hawawezi kufanya research zilizokamilika; kwa hiyo, forgery inaanzia kwenye vyuo; ndiyo maana wakienda field kwenye halmashauri zetu, mahali panahitajika nondo 10, wanaandika nondo mbili. Forgery inaanzia chuoni, tumeshindwa kuwafanya hawa watoto wakafanya researches za uhakika kwa hiyo, wana-copy tunapata degree fake, halafu baadaye tunalaumu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe sana, sasa tuangalie namna gani tunaweza kutumia mifuko katika kuongeza bajeti ya research kwa hao wanafunzi, hivihivi tunapoteana. Hao watu wathaminishaji, tunapata watu wa procurement, Engineers, sijui wengine wanawaita Valuers nasema wote hawa wanahitaji kufanya researches za kutosha. Sasa ardhi kuna hilo tatizo na naomba Mheshimiwa Waziri alichukue hilo. Vijana wanakwenda wanafanya research wiki moja kweli! Hili litatuangusha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo nije kwenye National Housing. National Housing Corporation wanafanya kazi vizuri sana, tulikagua hata wakati ule wamekwenda kufanya marekebisho kwenye sekondari, walijitahidi sana wakati tulilinganisha na lile Shirika lingine, walijitahidi sana. Hata hivyo, niseme, hizi nyumba za National Housing, mimi ni mdau nina nyumba pale Tabora, nikishuka pale nataka kuingia naangalia kushoto na kulia, nani ananiangalia naingia kwenye hii nyumba, yaani unaweza kusema ni magofu. Ukiangalia vijana wanaohusika kwenye National Housing hawafanani na hizo nyumba. Mheshimiwa Msechu, kuna kina Merkio, akina Deo, sijui akina Elias ni vijana ambao ukiwaangalia hawafanani na zile nyumba za National Housing.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa wakaangalie ni namna gani watazifanyia ukarabati na kazi hiyo wanaiweza akina Msechu, hebu wazibadilishe; tunataka wawe na uniqueness ya National Housing na wanaweza kufanya hivyo. Mandhari yake nyingine hapa zipo Iyumbu zinaitwa Satellite, waende wakaziangalie, tunataka zilete mandhari, zioneshe kabisa kwamba hizi nyumba zinasimamiwa na vijana wasomi na wanaoweza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, niende kwa wafanyakazi wa National Housing na hasa vibarua. Wananiambia vijana wale, wanafanya kazi, lakini Mkurugenzi akaangalie wakifanya kazi wapate malipo kwa wakati. Akifanya hivyo kila mtu atasema hivyo sasa kweli tumempata Msechu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nikushukuru sana. (Makofi)