Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Hon. Conchesta Leonce Rwamlaza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangia machache katika hii bajeti ya Ustawi wa Maendeleo ya Wanawake Jinsia na nini na nini lina neno refu mimi sijaielewa vizuri. (Kicheko)

SPIKA: Haya ngoja nikusaidie, inaitwa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, nimefuatilia kwa karibu sana hotuba ya Waziri, lakini pia nimefuatilia kwa kwa karibu sana maoni ya Kamati, hotuba hiyo na maoni ya Kamati hakuna mahali wameongelea Mfuko wa Maendeleo wa Wanawake yaani ile Women Development Fund. Waziri hakusema popote na hata kamati haikusema popote. Mfuko huu upo katika Wizara hii na unatoa mikopo katika halmashauri, je, naomba niulize mfuko huu upo au mfuko umekufa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, CAG ametuambia mwaka 2020/2021 mfuko huu ulipanga kutoa mikopo ya shilingi milioni 450 lakini Serikali haikutoa chochote katika mfuko yaani one hundred percent na kama Serikali haitoi fedha katika mfuko huu, huu mfuko ukoje na unaendaje? Maana yake tutaongea mikopo ndani ya Halmashauri ile ya ten percent lakini huu mfuko naona Wizara imekaa kimya na hata Kamati imekaa kimya. Tungependa kupata ufafanuzi kwamba je mfuko huu upo au umekufa. Mfuko huu ulipanga kutoa mikopo, lakini mfuko huu licha ya kupanga mikopo, lakini sekretarieti yake ilikuwa inapaswa kukusanya madeni ya shilingi milioni 300 lakini amekusanya shilingi milioni 20.6 ambayo ni asilimia saba tu. Kwa hiyo inaonekana hata sekretarieti yake haifanyi kazi vizuri, kwa hiyo, kuja haja ya Serikali kurudia kuupanga upya mfuko huu ili na wenyewe uweze kusaidia katika kutoa mikopo kama halmashauri zinavyofanya.

Mheshimiwa Spika, siwezi kuchangia bila kwenda kwa wazee, yamesemwa mengi katika wazee na tumechangia sana kuhusu mambo yao, nashukuru kila mtu anawaona wazee jinsi anavyowaona. Kitu cha kwanza ninachokiona perception ya Watanzania au raia na wananchi kwa ujumla juu ya wazee ni kama imefifia katika miaka fulani, lakini mimi napenda kusema Serikali imejitahidi kusaidia wazee kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kuwapa tiba bure, lakini watu ambao wana uhakika wa kuweza kutunza wazee ili waweze kupata matunzo yao ni watoto wao pia wanapaswa kufanya hiyo kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi napendekeza Serikali hii ije na muswada, baada ya kufanya need assessment tunaweza kuangalia mahitaji ya wazee, baadaye ukaja muswada ambao unawa-task watoto kuweza kutunza wazazi wao, na wanaweza kutunga sheria ambayo kwa wale watoto wanapata kazi sehemu ya mishahara yao inaweza ikakatwa ikapelekwa moja kwa moja kwenye akaunti za wazazi wao. Kwa hiyo mimi naona kwamba twende na hiyo muda ni mchache. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naona niongee kuhusu TASAF; TASAF ni Mfuko wa Maendeleo ya Jamii ambao upo chini ya Wizara ya Utumishi na kadhalika, lakini mfuko huu kwa sababu ni wa maendeleo ya jamii uangalie namna ya kurudishwa katika Wizara hii, kwa sababu huu mfuko unaangalia wanawake vijana yaani wale young women pamoja na wale wasichana wanaopevuka yaani adolescent ambao wanaweza kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza mambo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini mfuko huu hautoi fedha kwa ajili ya wanawake hawa kwa sababu hata ukiwapa hakuna mtu wa kuusimamia, utasimamia vizuri kama huu Mfuko wa TASAF ambao unahusu haya makundi maalum, wazee, wanawake, vijana pamoja na hawa wasichana wanaopevuka wakipewa fedha kwa ajili ya miradi yao midogo wanayotengeneza, basi mtu wa kusimamia vizuri mfuko huu ni Wizara hii ambayo kwa kweli na mimi ninapenda kumshukuru Rais ambaye amerudisha Wizara hii ambayo kutokuwepo kwake kwa kweli kulichagiza mambo machafu sana kufanyika ndani ya nchi pamoja na ubakaji na mambo mengine ya udhalilishaji.

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)