Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Hon. Mwantum Dau Haji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Spika, kwa nafasi hii niliyoipata hivi sasa hivi na kuichangia wizara hii iliyombele yangu na kwa mara yangu ya pili Bunge hili lako tukufu kuendelea kuchangia hii leo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, awali ya yote kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kunijalia kuwa na hali ya uzima na afya na kunijalia kwamba hivi sasa nimesimama niweze kuichangia Wizara hii ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto na mambo mengine.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Rais Mheshimiwa wangu Samia Suluhu Hassan kwa kuupiga mwingi. Hii Wizara nasema ilikuwa ina Wizara ambayo imo pamoja na Wizara ya Afya, lakini Rais wetu akaamua kuitenga baina ya Wizara ya Afya na Wizara hii ya Maendeleo ya Jamii makusudi ili iweze kufanya kazi vizuri. Kwa hiyo mama nampongeza sana na hao watu ambao aliwaweka hapa Mheshimiwa Waziri na Naibu wake wanafanya kazi vizuri ili waweze kufika hapo mbele tunapopataka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuendelea kuchangia, mimi niendelee kuchangia kwanza kuhusu suala la wanawake; wengi Wabunge wenzangu wamechangia mambo mengi mambo mazuri tu ambayo wamechangia na kila atakayesimama hapa anachangia masuala ya wanawake na watoto kuhusu unyanyasaji pamoja na ubakaji.

Mheshimiwa Spika, sisi wanawake tuliokuwemo humu ndani ya nchi au ndani ya Tanzania hii kwa kweli tunapata matatizo makubwa sana na kuna wanawake waliokuwemo ndani ya majumba wanaangaika usiku na mchana na hali zao duni na masikini wengine wameolewa, lakini na wengine wanakuwa wajane.

Mheshimiwa Spika, mwanamke mwenye mume hivi sasa amekaa kwa mumewe kusema kwamba mimi naomba stara ili nisitirike, nitazame hatma yangu inapokwenda. Mwanamke huyu anakwenda zake kuuza machungwa au mboga au anakwenda kwenye ujasiriamali wake kujitafuta riziki, mwanamke huyo akirudi pengine maji hana ndani akayatafute, mwanamke huyo hana chakula cha kula ameshanunua huko alikokwenda kuuza matunda yake, anakuja anapika mboga yake, anaupika ubwabwa wake anamaliza shughuli zake na anategemea mume wangu hapa akija nije nimfurahishe.

Mheshimiwa Spika, mwanamke akishapika chakula kile na jinsi wanawake sisi tunavyowapenda wanaume basi Mwenyezi Mungu alivyotujalia sisi wanawake tunawapenda wanaume, nisifiche hili neno lipo mwanamke anapika chakula anaiweka sahani nzuri kaipamba wali, ule wali anaupika kule kwetu kule kwetu linaweka tandu juu, analichukua tandu anamwekea mumewe pale kaipika mboga yake vizuri kaiweka pale kila kitu chake ile kitu kimetokana na mwanamke. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, anakuja mume anakamkaribisha vizuri mumewe wanakuja wanakula pale ila wenyewe wanaendelea kuzungumza mazungumzo yao baina ya mwanamke na mwanaume ndani ya nyumba, lakini bado wanawake wananyanyasika yote hayo anayoyafanya haonekani kama yeye yule mwanamke si lolote si chochote. Mwanaume anaweza akatafuta nyumba ya pili au ya tatu mkewe aliye ndani aliyemuwekea lile tandu akaona si lolote si chochote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wizara hii naiomba, hii Wizara yako leo au wizara yetu naiyomba hiki kitu kiwasimamie wanawake vizuri kiwajengee uwezo wanawake na kama kuna uwezekano mimi nazungumza siku zote wapate mafunzo ili hawa wanawake wajue jinsi ya kukaa ndani na kuhusu familia zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili hilo nalizungumzia kuhusu watoto wetu jinsi wanavyonyanyasika ndani ya nyumba, ndani ya maeneo, ndani ya shughuli zao wanakokwenda.

Mheshimiwa Spika, kuna wengine watoto wananyanyasiwa kwenye shule au vyuoni. Walimu wao wenyewe wanawanyanyasa watoto lakini mbaya zaidi inayosikitisha baba yake mtu aliyemzaa kashawekea tandu na mkewe, jioni yake anakwenda kumfanyia kitendo kibaya mwanae mweyewe aliyemzaa. Kweli hii haki? Hii inakuwa si haki anafanya kitendo kilichokuwa si kizuri kwa yule mwanae au watoto wake anawafanyia mambo yasiyokuwa na maana na anamfanyia yule mwanamke kwa juu ya mapenzi aliyonayo haoni hasikii kwamba mimi huku mume wangu ataingia ubavu wa pili aende akawadhuru wale watoto kwa vitendo vibaya. Kalala buheri kwa masaa ishirini mwanamke hana habari baba mtu anakula vitu kwa mtoto.

Mheshimiwa Spika, kweli hili suala ni haki hii Mwenyezi Mungu kweli yupo radhi kufanya vitendo kama hivi? Kwa hiyo, jamani Wizara itusaidie kwa sababu akienda akisema mtoto anatishwa.

Mheshimiwa Spika, juzi tu hapa mtoto kalawitiwa na baba yake mbele na nyuma, akamwambia huna ruhusa ya kusema na ukimwambia mama yako basi sikununulii dhahabu wala sikupi herein, wala sikupi nyumba mtoto kashindwa kusema anamwambia nitakuchinja au nitakuua ukisema kafanya tendo hilo mwanamke kuja kugundua kaenda kusema kwa mama kamwambia wewe mama kampiga mwanamke kapigwa mpaka kasema hiki nini! Mtoto yule keshamuhangaikia na baba kutambulika kakimbia dunia hii unakimbia unaenda wapi? Ameshakamatwa na sasa hivi yupo kwenye mikono ya sheria.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, sheria ya watoto ambao wananyanyasika ingawa imewekwa kwa mtu mbakaji atiwe ndani kwa muda wa miaka 30, mimi naiona hii kidogo na kama atapewa hii miaka 30 huyu mbakaji huyu kama atapewa hii miaka 30 basi ahasiwe kwa ile sindano, akishahasiwa kwa ile sindano yule atakuwa hana nguvu na atakapotoka huku nje adabu atakuwa kaipata kwa muda wa miaka 30, kahasiwa hana nguvu, hana kitu chochote amekaa yeye kama boya, mtu kama huyo anakuwa anaitwa chapa upunga ulale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja asilimia mia moja. Ahsante sana kwa ruhusa yako, ahsante. (Makofi)