Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Hon. Zuena Athumani Bushiri

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inavyoongozwa na Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan; nimpongeze Waziri, Naibu Waziri na watendaji wote.

Mheshimiwa Spika, nianze kuchangia kuhusu wanawake wanaovyonyanyasika kwa kutelekezwa na waume wao; kumekuwa na tabia ya wanaume kutelekeza wake zao na watoto na kusababisha watoto kukosa haki zao za msingi kama elimu, chakula, malazi na mapenzi ya wazazi wao wote. Wanawake wanaotelekezwa kwanza wanaathirika kisaikolojia na kusababisha hata kukosa malezi bora. Niishauri Serikali kutunga sheria kali ili kudhibiti hali hii.

Mheshimiwa Spika, nichangie pia kuhusu suala la nyumba za kulelea wazee nchini. Tunao wazee wengi sana ombaomba ambao hawana uwezo katika Taifa letu, wazee hawa wengine hawana nyumba bora za kuishi wengine hawana chakula, nguo na kadhalika. Niiombe Serikali kwanza ihakikishe kila mkoa kunakuwa na nyumba za kulelea wazee za kutosha kulingana na idadi ya wazee waliopo katika mkoa husika ili kuwasaidia wazee ambao wanahitaji kulelewa.

Mheshimiwa Spika, nimalize kwa kuchangia suala la ukatili kwa wanawake na watoto. Kumekuwa na wimbi kubwa la wanaume kupiga wake zao na watoto hata kupelekea kupata ulemavu, niiombe Serikali itunge sheria kali ili kudhibiti ukatili huu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja.