Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nimpongeze Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya. Pia nimpongeze Waziri Mheshimiwa Dorothy Gwajima pamoja na timu yake kwa kazi kubwa wanayoifanya.
Mheshimiwa Spika, uhaba wa wayumshi katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Mandeleo ya Jamii ya Ufundi hususan Mabughai, Lushoto na Misungwi, Mwanza; vyuo vya ufundi na vyuo vya maendeleo ya jamii, Uyole, Buhare na vingine hauoni uhaba huo unapelekea vyuo kutumia fedha nyingi kwa kutumia wakufunzi wa muda na hata kurundikana kwa masomo. Mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi zaidi ya 100 jambo hili linashushia hadhi ya utoaji wa mafunzo.
Mheshimiwa Spika, kwa nini watumishi wengi wanavikimbia vyuo vya maendeleo ya jamii badala ya kuvikimbilia kufanya kazi, sababu watumishi wetu hufuata maslahi vyuo vingine ama taasisi nyingine. Pia miundombinu chakavu na hali duni ya vifaa vya karakana na maabara na hata uchakavu wa vyombo vya usafiri, kwa mfano magari yote ni ya tangu mwaka 2009.
Pia kuna uhaba wa hosteli vyuoni; kwa kuwa vyuo vya maendeleo ya jamii na watoto havina hosteli, niiombe Serikali itenge fedha za kutosha ili vyuo vyetu vijengewe hosteli ili watoto wetu wajisikie kuwepo kwenye vyuo kwa ustawi wao na kuwalinda na unyanyasaji na endapo watakaa mtaani hawatatimiza ndoto zao.
Mheshimiwa Spika, kumekuwa na unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo yetu ya kazi, hii imefikia hatua mbaya zaidi mpaka kupelekea wananchi kuwalinda wahalifu hao. Niishauri Serikali itenge dawati la kutoa elimu ya mambo mabaya kama haya ili kuonesha kabisa tabia hii iliyokithiri hasa mijini. Pia kuna haja ya kuangalia pension za wazee hawa hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kufanya kazi na pia kuna hawa walemavu hasa wanaoishi vijijini kwani walemavu hawa hawafikiwi na huduma yoyote inayowahusu wao, badala yake huduma hii huishia kwa walemavu waishio mijini tu.
Mheshimiwa Spika, niiombe Serikali iwape usafiri Maafisa Ustawi wa Jamii ili waweze kuwafikia walemavu hawa wanaoishi vijijini, kwani nao wana haki kama hawa wenzao wanaoishi mijini.
Mheshimiwa Spika, pia Serikali iongeze fedha kwenye Wizara hii ili iweze kutimiza malengo yake.
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.