Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Hon. Ghati Zephania Chomete

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa Spika, naipongeza sana Wizara kwa juhudi kubwa iliyoanza nayo tangu imeanzishwa.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Rais wetu Mama Samia kwa kuigawa Wizara hii ili kuwafikia wananchi kwa urahisi.

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuishauri Serikali katika kundi hili la mabinti walemavu na mabinti walemavu wanaofichwa na wazazi wao kwa kudhania kuwa ulemavu ule hawezi kupata elimu wala kufanya kazi yoyote.

Mheshimiwa Spika, niombe tutoe elimu kwa jamii ili itambue kuwa watoto hao wanaweza kusoma na kuisaidia jamii yao. Lakini pia wanawake walemavu watambuliwe kwa idadi yao kupitia Kata, Wilaya mpaka Mkoa ili wawezeshwe kwa kupatiwa miradi rafiki kwao.

Mheshimiwa Spika, kuhusu ndoa za utotoni, kumekuwa na ndoa za utotoni sana katika jamii yetu, naishauri Serikali itenge fedha kwa ajili ya kutoa elimu inayohusu madhara ya ndoa za utotoni na kushirikiana na mashirika yanayotoa elimu na yanayopinga ndoa za utotoni kwa mfano kule Mkoani Mara Shirika kama Masanga, Hope for Girls yamekuwa ni mashirika yanayotoa elimu inayohusu madhara ya ndoa za utotoni ili Taifa letu liwe na vijana wenye elimu na afya njema.

Mwisho naishauri Serikali kuviboresha Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kama vile Chuo cha Buhare kilichopo mkoani Mara na vingine vingi nchini ili viendelee kufanya vizuri zaidi.