Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Hon. Esther Edwin Maleko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Spika, awali ya yote kwanza nichukue nichukue nafasi hii kumpongeza sana Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuitenganisha Wizara hii na Wizara ya Afya, hakika ameitendea haki ili iweze kusimamia maendeleo ya jamii, kwa kuwa Wizara hii imebeba mwanga wa vizazi vyetu kwa maana jinsia wazee, watoto, na makundi maalum ndio ukamilifu wa maisha ya mwanadamu.

Mheshimiwa Spika, tukielekea kupitisha bajeti hii muhimu ni ukweli usiopingika nchi yetu imepitia vipindi kadhaa vya udhalilishaji wa kijinsia hasa kwa na watoto katika maeneo mbalimbali. Kiukweli katika dunia ya sasa watu wameshabadilika kutoka kwenye dhana ya unyanyasaji wa kijinsia, badala yake wanapigania kuyakuza makundi mbalimbali kwa kuyaongezea nguvu na uwezo hasa wanawake na watoto.

Mheshimiwa Spika, tafiti za hivi karibuni zilizotolewa na Jeshi la Polisi nchini ambao ni chombo kinachohusika kupokea matukio mengi ya unyanyasaji wa kijinsia inaeleza kuwa mpaka Juni, 2021 tayari watu 15,131 walikuwa wamefanyiwa ukatili wa kijinsia hasa wanawake waliouawa katika ndoa. Pia ripoti iliyotolewa Septemba, 2021 na Jarida la Afrika kuhusu hali ya ukatili wa kijinsia Tanzania imeonesha kuwa asilimia 46 ya wanandoa hufanyiwa ukatili wa kimwili na asilimia 32 walifanyiwa ukatili wa kisaikolojia na asilimia 13 wanafanyiwa ukatili wa kingono.

Mheshimiwa Spika, Mungu ameliwezesha Taifa letu kwa kulionesha kuwa mwanamke anaweza kufanya mambo makubwa yanayobeba na kuiheshimisha jamii kwa kutupa Rais mwanamke Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye anatupa tafsiri kuwa mwanamke sio kiumbe anayestahili kunyanyaswa, bali anastahili kuungwa mkono na kufunguliwa milango ya fursa. Sasa inasikitisha sana kuona namna Taifa letu linavyojipambanua juu ya kuheshimu nafasi ya mwanamke na haki za Watoto, lakini jamii zetu zimekuwa kimya juu ya ukatili huu unaojitokeza.

Mheshimiwa Spika, sasa Wizara ihakikishe inaimarisha uelewa wa Watanzania juu ya kulinda haki za watoto na wanawake kila mahala sambamba na kuwawezesha wanawake na watoto kuweza kujitambua. Kuwe na madawati katika shule za msingi na sekondari yawepo kusaidia watoto hawa kutoa taarifa kwenye mazingira rafiki maana wengine wanaogopa kwenda polisi kwa hofu.