Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Hon. Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, nashukuru kunipa fursa ya kuchangia kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, ushauri kuhusu uanzishaji wa Madawati ya Jinsia katika Taasisi za Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati, niipongeza Serikali kwa kuanzisha madawati haya. Mwongozo huu utasaidia wanafunzi kupata ushauri na pia inaweza ikawanusuru changamoto za msongo wa mawazo, kuua na kujiua, rushwa ya ngono na masuala mengine ya ukatili. Ushauri wangu mwongozo huu uwe popularized katika vyuo vyote. Pia wanavyuo wote wafahamishwe kuhusu mwongozo huu. Pia Serikali iongeze bajeti ya maendeleo Fungu 53 katika pesa ya maendeleo ili kuleta ufanisi.

Mheshimiwa Spika, ushauri kuhusu ukatili kwa watoto; watoto wafundishwe kutoa taarifa na wasiogope vitisho wanapofanyiwa ukatili watoe taarifa, pia wazazi/walezi wawe wanakagua watoto wao kuona kama wamefanyiwa ukatili na kuchukua hatua za mapema.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na naunga mkono hoja.