Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza sina budin kumshukuru Mwenyezi Mungu aza wajaalah kwa kunijalia uhai na uzima na leo kuwa mbele ya Bunge hili. Vilevile kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu pamoja na watendaji wao wote wa Wizara. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nilikuwa nataka nizungumzie kidogo kuhusu hii Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ishirikiane na Wizara ya Utalii wakati sisi tuna Balozi ambao Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje waweze kufanikisha kuleta watalii kwa wingi Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kazi aliyoifanya Mheshimiwa Mama Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea vivutio vyote vya kiutalii vya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar hii kazi iwe sio ya bure, ametengeneza filamu ya royal tour na ile filamu inatakiwa itekelezwe na watekelezaji wetu ni mabalozi wetu kwa kuweza kutuletea watalii kwa wingi, kazi ya mama isiwe ya bure iwe kazi ya mama inafaa, yeye kaona maono kutuanzisha sisi nini tufanye. Sasa suala hili Wizara mlikamate, mshirikiane na mabalozi kazi iendelee. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nazungumzia suala la Sera ya Mambo ya Nchi za Nje. Mheshimiwa Waziri ameeleza uzuri katika ukurasa wake wa saba na tunashukuru kwamba, ilikuwa siku nyingi imekaa kwa sababu, hii sera ndio itazidi kuwa chachu ya diplomasia ya kiuchumi. Kwa sababu sera ikifanya kazi sambamba na diplomasia ya kiuchumi ikaenda pamoja ina maana wakulima, wafanyabiashara, bidhaa zetu zinatoka mashambani, usafirishaji wa bidhaa pamoja na masoko ya nje yataweza kupatikana na tutanufaika na tutaondokana na umasikini. Nafikiri na hilo mliangalie, lakini kuliangalia vipi, mtoe elimu kwa wafanyabiashara, mtoe elimu kwa wakulima maana maparachichi yanalimwa, tunalima vitu vingi Tanzania na vina soko nje, lakini bila kumpa mtu elimu atalima na kisha yatajaa Kariakoo tele yamerundikwa pale chini, bila ya kufanya kazi hataweza kufanikiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni ukarabati wa Balozi zetu. Balozi zetu kwa kweli kuzikarabati kama Wizara si rahisi maana yake nyingi chakavu, kwingine hakuna, kwingine hazikaliki, nyumba za mabalozi, nyumba za wafanyakazi na ofisi za ubalozi, lakini jambo lililokuwepo tunaweza tukafanya awamu kwa awamu na tukazishirikisha taasisi za kiuchumi na wanakubali. Kama kuna sheria inapinga leteni Bungeni, tuleteeni ushauri ili hizi ofisi, itakuwa kila siku tunaimba, tunasema, tunapiga kelele, utekelezaji hauonekani. Sasa tubuni mbinu, mbuni mbinu, ili hizi balozi ziweze kujengwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu mfano mimi nilikwenda ziara Congo, Kinshasa, tumeona nyumba ya Balozi haina hadhi ya kibalozi. Ofisi yao haina hadhi, ingawa zimekarabatiwa, lakini itakuwa ndio hapo kwa hapo tu, lakini wamejiongeza kwa sababu ule mtaa waliokuwepo Mtaa wa Gombe, prime area na nafasi wanayo kubwa ambayo plot yao nafikiri namba 912 tatizo lililokuwepo walivyojiongeza, makisio wamefanya tayari, lakini hata wakifanya makisio wakati Wizara hamjawapelekea pesa wafanye nini? Hawawezi kufika kokote. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, na wametuonesha hilo jumba wanalotaka, maana yake la kiuchumi, mtakuwa na ofisi, nyumba, watakodisha watapata wao na itanufaika Tanzania na sifa itakuja Tanzania. Sasa hizi hii awamu kwa awamu lazima hizi ofisi muwe mnaziangalia ili Tanzania nayo iwe katika maajabu katika mabalozi yao. Sio niwe Tanzania Balozi inaonekana ya kizamani, hilo halipo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hizi jumuiya ya kikanda na masoko; hii Mheshimiwa tulipewa semina sisi hivi juzi tukaelezewa kwa kweli, mafanikio tumeyaona, lakini nawaomba hii semina wapewe na Wabunge wote kwa sababu kila mmoja akipata kwa sababu sasa hivi uzalishaji mzuri tu, masoko yako na isitoshe njia zi wazi, Tanzania tunauza sana, lakini watu hawajui. Elimu itolewe na Wabunge pia wafanyiwe semina ili na wao wawe ni mabalozi watakaotoka nje ya Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)