Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Hon. Joseph Kasheku Musukuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia Wizara ya Mambo ya Nje. Kwanza nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri tunaona bidii ya kazi yake anayoifanya, aendelee kurudisha mahusiano ambayo yalivurugika.

Mheshimiwa Naibu Spika, asilimia 90 ya Watanzania wa hali ya chini tunategemea sana bidhaa kutoka China na Watanzania wale wa kawaida kabisa na hata humu sisi wenyewe Wabunge asilimia kubwa tunatumia bidhaa ya China. Kwa hiyo, rafiki mkubwa wa Tanzania kiuchumi ni Mchina, sasa na mimi ninazunguka huko China mara nyingi na nimemuona Balozi Kairuki hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeenda hadi ofisini kwake Beijing na labda tuone wapi tumekosea. Kweli kwa Watanzania wa hali ya kawaida ambao ni wafanyabiashara wenye elimu ya kawaida ya darasa la saba kuwapeleka kwenye biashara ya mtandao wewe unakaa Kariakoo wengi sana wamekula hasara, niombe sana Waziri na Balozi mkae na wenzetu kama kuna mahali tuliwakwaza au kuna vigezo hatujafikia waone namna ya kuiachia Tanzania kwa sababu kwanza ni soko lao kubwa kwenye bidhaa zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi watanzania wengi pale kariakoo wamekula hasara kubwa sana na wenzetu wa China ni wajanja kweli, watu wengi wanaoagiza bidhaa mtandaoni mara nyingi inapokuja Tanzania inakuwa tofauti na kitu ulichokiagiza, ulichoonesha ni kingine na kilichokuja kwenye kontena ni kingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na hata ukirudi kwenye address ya kule china unakuta ameshabadilisha na address kwa hiyo watu wengi wanakula hasara biashara nyingine kama za Kariakoo za nguo za urembo zinahitaji choice ya macho sio ya mtandao, leo ukienda Kariakoo inakufa wewe mwenyewe ni shahidi ukienda Uganda na Kenya wenzetu sasa hivi tunatoka Tanzania kwenda kununua bidhaa Uganda na Kenya tuone namna wapi tulikosea turudishe mahusiano. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini lazima na wao wawe fair, leo Wachina wapo kila kata wanachezesha kamari yaani kuja kwetu Tanzania hakuna corona, ila sisi tukienda kwao kule kuna tatizo, mahusiano tuyatafute kotekote kwa sababu na wao wenyewe wanafaidika na Tanzania waone namna ya kulegeza. Mimi nadhani kwenye Afrika ni nchi Tanzania pake yake ambayo leo ukienda kila kata asubuhi saa tatu utamkuta Mchina anakusanya fedha kwenye kamari. Sasa sisi kwenda kule ni kwasababu ya yale mahusiano ambayo tumeyajenga pamoja na wao lakini ukienda kwenye biashara za madini wamejaa Wachina, ukienda kwenye contract za miradi wamejaa Wachina, ukienda kila kazi ambayo ina maslahi makubwa wapo Wachina.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Kwenda huko inakuwa ngumu na mimi mwenyewe ni mfano mzuri na Mheshimiwa Amar hapa tumeagiza mitambo unaoneshwa katapira lakini imekuja mitambo ya Kichina mpaka leo Mheshimiwa Hussein amesimamisha mtambo kwa sababu wataalam hawawezi kuja eti kuna corona ila kuja kuchezesha kamari wapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikuombe sana Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Balozi mtuelewe, mtusaidie Watanzania wengi waliotajirika wametajirika na China, kulikuwa na maonesha tunakwenda kujifunza maonesho ya teknolojia za kisasa ni vizuri waangalie namna ya kuachia yale mahusiano vizuri kabisa ili tuweze kwenda kama tulivyokuwa tunaenda zamani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini lingine ni suala ambalo kila mwaka humu Bungeni huwa linazungumzwa la uraia pacha. Hofu yangu mimi najiuliza ni nini, yaani tunaweka kikwazo kwamba mtu aliyekuwa nje, Mtanzania ambaye nikimsomesha mwanangu akimaliza akasema baba nimepata kazi akafanya maarifa yake akapata uraia, kurudi Tanzania anakuwa ni mgeni, hii ni uonevu mkubwa sana, tunapoteza watoto wetu, tunawanyima fursa kwa sababu ya vitu ambavyo mimi nadhani ni hofu ya kisiasa pia, kwa sababu wanasema eti aruhusiwi kugombea kazi za kisiasa kwanini yaani kwa tatizo gani yaani mtu amesoma, amepata knowledge kubwa akirudi akiwa Waziri hapa ndio watu ambao tunawataka tubadilishe mawazo tofauti. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo niombe sana hili halikwepeki, hata mkilikwepa jaribu kufanya analysis ya wahindi matajiri hapa Tanzania wote wana uraia mbili, utamkuta ni Mtanzania ana passport, lakini ana passport ya Canada na ana ya Uingereza kwa kwetu sisi tuna hofu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo ukienda Uingereza juzi nilikuwa naangalia television tumepata Diwani Msukuma wa Nzela kule Jimboni kwangu kapata Uingereza, tuna Mawaziri wapo sijui Canada, tunaona wivu gani tunasomesha nje ili tupate mawazo mapya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nilikuwa naiomba Wizara hizi hofu tuziondoe turudishe tu hali halisi kwamba watu wapate uraia wa nchi mbili kama anafanya vizuri akirudi hata Jimbo langu agombee, akinishinda basi, ndio vitu tunavyovitaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama Mbunge unajiamini unafanya kazi vizuri hata ukija na degree zako hata ukitoka Marekani unamkuta King kazuia hapo, utapigwa unarudi unajipanga tena. (Makofi)

Kwa hiyo, tuondoe hofu tunapeleka watoto wetu nje ili wapate knowledge ya kuja kulisaidia Taifa na tujifunze hata Asia walipeleka kwanza watoto wao Ulaya wakaiga Ulaya wanafanyaje, waliporudi kwao wakafanya mambo mazuri, tuondoe hofu kazi nzuri Mheshimiwa Waziri, lakini nakusisitiza na kukuomba tena Watanzania wengi wanaitegemea China, hata humu ndani ukiangalia suti nyingi humu ndani ni za Kichina, mnaguna nini wengi tu mmekula (mmevaa) Mchina sasa ukiweka masharti mwisho tutavaa fake ambayo sio choice ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana hata nywele humu nyingi ni za Kichina. (Makofi/Kicheko)