Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Nishati

Hon. Augustine Vuma Holle

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kasulu Vijijini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Nishati

MHE. VUMA A. HOLLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa fursa hii na mimi kuchangia hoja hii ya Bajeti ya Nishati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nipende kumpongeza Mheshimiwa Rais lakini na Waziri mwenyewe. Leo tarehe 01 Juni, waliahidi kwamba watashusha bei ya mafuta, kweli tumeona tangu jana usiku mafuta yameshuka imepunguza angalau makali ambayo yale ambayo Watanzania walikuwa wanayapata. Hongera sana Serikali yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwana nataka nizungumzie grid ya Taifa Mkoa wa Kigoma, ni matamanio ya wananchi wote wa Mkoa wa Kigoma kupata umeme wa uhakika kama ambavyo watanzania wengine wanapata. Kwa bahati mbaya sana hatujawahi kupata grid ya Taifa tangu tupate uhuru Mkoa wa Kigoma. Tumekuwa tunasema muda mrefu humu ndani na kwenye platform tofautitofauti lakini bado utekelezaji wake unasuasua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa nimeona kwenye bajeti ya Mheshimiwa Waziri, kwanza nishukuru kwamba kuna mawazo hayo ya kupeleka grid ya Taifa lakini nimeangalia figures bado is not convincing, ina maana huu mradi wa Urambo kwenda Kigoma ambao ni Bilioni 69.7 zimetengwa Bilioni 2.0. Nimeangalia huu wa Nyakanazi kwenda Kigoma ambao ni zaidi ya dola Milioni 35 ambao ni zaidi Bilioni 80 huko lakini tumetengewa Bilioni 7.4. Chondechonde Mheshimiwa Waziri unanisikia vizuri, wewe ni Kaka yangu, unajua hilo tunaheshimiana sana. Mkoa wa Kigoma tunaomba wakati tukiwa Waziri wa Nishati tuachie zawadi, tuachie legacy, Kigoma itakukumbuka wewe, itamkumbuka Mama Samia katika suala la umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naweza kusema mengi lakini mengi wewe unajua tumeshazungumza, nakuomba sana Kigoma tunataka grid ya Taifa, tumesubiri mno, Mikoa yote grid ya Taifa imeunganishwa bado Kigoma tu, kuna nini? Tunahitaji tutengewe fedha za kutosha siyo Bilioni Mbili hizi, tupewe fedha za kutosha ili miradi hii iende kwa kasi kubwa, ikamilike na wananchi waweze kupata grid ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la REA nashukuru vipo Vijiji ambavyo vimepata umeme lakini yapo maeneo makubwa hasa sisi Wabunge wa Vijiji, Kasulu Vijijini, kutokana na ile jiografia ya kule umbali wa kutoka Kijiji mpaka Kijiji yako maeneo mengi ambayo umeme kwa kweli haujafika. Ziko Kata kama saba Nyamwusi, Titie, Ungwempya, Kurugongo, ahsante Nyerere, Kitanga, Herushingo, Shunguriba hizi ni Kata kabisa ambazo umeme haujafika. Ningependa kasi ya kupeleka umeme Vijijini hasa Jimbo la Kasulu Vijijini yaongezeke kwa kasi kubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, liko suala la kukatikatika kwa umeme. Kama kuna jambo ambalo limekuwa linachafua Serikali ni la kukatikatika kwa umeme, tunaweza tukafanya mambo makubwa na mazuri sana lakini lazima tudhibiti jambo hili. Na nikupongeze Mheshimiwa Waziri kwa kuja na mawazo haya ya kuimarisha grid ya Taifa. Umekuja kuomba Bilioni 500 hapa nimeona na Inshallah tutakupatia lakini nenda ukasimamie vizuri suala la kukatikakatika kwa umeme linachangia, linachafua mno Serikali kuliko kawaida. Umeme ukikatika tu watu wanatukanwa mno huko chini. Lazima tujitahidi sana hizi fedha ambazo utapatiwa uende ukafanye usimamizi mzuri sina mashaka na Mheshimiwa Waziri, naamini usimamizi utakuwa mzuri na hatimae suala la kukatikakatika umeme lilikuwa ni nchi nzima lakini sasa Kigoma lilikuwa ni balaa zaidi, ili kuhakikisha kwamba tunaweza kumaliza jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa nataka nishauri jambo moja hii shilingi bilioni 500 nadhani kuna viwanda siku hizi vya kutengeneza vifaa mbalimbali vya umeme. Ningependa sana hii fedha sehemu kubwa ya fedha hii au chochote ambacho mnataka kununua ambacho kinapatikana hapa kwetu Tanzania vinunuliwe hapa hapa ili angalau kuweza kuongeza fedha kwenye mzunguko wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yangu ni hayo tu naunga mkono hoja all the best Mheshimiwa Waziri, ahsante sana. (Makofi)