Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Nishati

Hon. Joseph Kasheku Musukuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Nishati

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia. Naipongeza Wizara kwa kazi nzuri inazofanya pamoja na mambo madogo madogo yanayoendelea kutokea lakini hizo ndizo changamoto lazima ukabiliane nazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitachangia kuhusiana na suala la umeme, jana kuna mchangiaji nilimsikia anazungumza kuhusu sub-station ya Geita. Ni kweli tulimuona hata Mtendaji Mkuu wa TANESCO Ndugu Maharage kwenye vyombo vya habari anatangaza kufunga mkataba na GGM ambayo tunategemea kupata karibu Bilioni Tano kwa mwezi na utekelezaji wake ulitakiwa uwe umekamilika mwezi wa 12.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshauri Waziri kuwanyang’anya biashara ya mafuta ya exemption GGM siyo kazi ndogo, ubovu mwingine Serikali ukishajitangaza kwenye tv hamna ufuatiliaji, nilijaribu kufuatilia kule GGM hakuna kitu kinaendelea ndiyo kwanza wako kwenye manunuzi na wakati ujenzi wa sub-station ulitakiwa uwe umekamilika mwezi wa 12, kama leo ni mwezi wa Sita ndiyo kwanza wanaanza manunuzi, maana yake kuna miaka miwili ijayo.

Mheshmiwa Mwenyekiti, tunajua sisi tunaoishi pale kwamba wanatumia zaidi mafuta karibia zaidi ya lita Milioni Tatu kwa mwezi, siyo kazi ndogo na kuna deal za watu pale, siyo kazi ndogo ni lazima TANESCO muwe na mkakati mzuri maana ya kujenga ile sub-station ya Geita ilikuwa ni pamoja kulilenga lile soko la mgodi mkubwa wa GGM sasa naona kama tuna mizaha mizaha ambayo ninaimani wenzetu ndiyo wanatumia kama nafasi. Kwa hiyo, ni vizuri Mheshimiwa Waziri fanya ufuatiliaji uone wamefikia wapi usikae kuletewa tu taarifa za makaratasi, naamini hazitakusaidia na sisi wengine tulioko kule tunaona hali siyo nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili mimi kwenye Jimbo langu nimepata Ofisi ya TANESCO ambayo Meneja wetu pale anaenda mpaka kilometa 100 mpaka kilometa 90 kwenda kutoa huduma, tulikuwa hatuna gari anatumia pikipiki tena bodaboda, hapa amebeba viatu vya kukwea kwenye nguzo amebeba na vifaa vya kwenda kutengenezea. Nilipozungumza humu mmetuletea gari ambayo kiukweli ni kama dharau bora angebaki tu kwenye bodaboda. Gari inasukumwa kilomita moja ndiyo inawaka! Sasa nikuombe Mheshimiwa Waziri mimi ni Mjumbe wako wa Kamati najua mipango uliyonayo, toka akiwa Waziri Kalemani mnasema mna magari 100 yamefikia wapi? Au yamekuja yameenda wapi? Huko Mjini watu wana vitendea kazi sehemu ambazo mmepeleka huduma vijijini pelekeni magari ili watu waweze kufurahia huduma ya Tanesco vizuri pale wanapokuwa wamepata matatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la tatu nazungumza kwenye suala la mafuta. Nilizungumza hapa tunaishukuru Serikali imechukua hatua kupunguza kuweka bei, kuweka ile Bilioni 100 imepunguza lakini imepunguza wapi? Mimi naiona tu kwenye karatasi mpaka leo, yaani imepunguza kwa mletaji imepunguza kwa watu wa Dar es Salaam mimi ninayetoka Nzela Vijijini na Wabunge wenzangu mafuta ya vituo vyetu almaarufu madumu bado bei ni ile ile na imeongezeka sehemu zingine. Sasa Mheshimiwa Waziri mtusaidie maana tukitoa ushauri saa nyingine huwa hamtusikii tunawaeleza kila siku legezeni masharti ya vituo vya vijijini ili watu wakafungue vituo. Unawekage sharti kituo cha kijijini kinachouza lita 200 unaweka masharti sawa na kituo cha Kariakoo kinauza lita 15,000? Kwa hiyo, utakapokuwa umelegeza masharti nikuhakikishie kwamba madumu kule yatapungua na bei zitakuwa zinafuata utaratibu kwa sababu watu watakuwa na reserve ya kutosha. Kwa hiyo nikushauri narudia kushauri na kwenye Kamati nimezungumza ni vizuri tukabadilika mwaka wa pili hii tunazungumza karibia wa tatu tulegeze masharti ya kituo cha mafuta cha kijijini kisifanane na vituo vya mjini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Nne Mheshimiwa Waziri ni kuhusiana na suala la biashara kwenye hili naungana na Prof. Muhongo. Unajua biashara inataka vitu vingi sana, siyo tu degree kuipeleka TPDC kwenda kufanya biashara ya mafuta nakuambia ukweli mimi naungana na Mheshimiwa Profesa Muhongo hatutafika popote ni suala la muda tu. Tulikuwa na kampuni inaitwa COPEC iliingia kwenye hizi biashara ilienda wapi? Ilikufa sasa hivi tumeibuka tena na TAN OIL tunasema ni shirika, kampuni tanzu lakini bosi ni huyo huyo Mataragio na hii nawapa labda mwaka mmoja tu na yenyewe mnapotea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, biashara ya mafuta ina akili nyingi, kwa mfano watu kama MOIL na wengine wenye vituo vya mafuta wanawakopesha wateja wakauze kwenye madumu walete haya huko kwenye TANOIL unamkopeshaje mteja? inaweza ikaharibika tu pump ya kutengeneza kwa 15,000, 20,000 unaanza procurement siku tatu mpaka mafuta yanakupandia bei. kwa hiyo niombe sana mimi nakubaliana na Muhongo TPDC ibaki kwenye kazi yake ya taaluma ya kutafuta mafuta na kutafuta gesi kwenye biashara tuwaachie private sector mimi nakuhakikishia Mheshimiwa Waziri hii pesa kwa mfano ungempa private sector akafanya na huu mtaji baada ya miezi zita tungekuwa na faida kubwa sana lakini leo pamoja na kwamba ni Kampuni ya Serikali nakuhakikishia Mheshimiwa Waziri huko tuendako bado tuko Bungeni kuna mzinga ambao najua tu utakuja wala siyo muda mrefu tutakuja kuujadili tena humu. Tuziache private sector zifanye kazi za biashara sisi tufanye kazi ya taaluma kuwaonyesha watu wafanye kama walivyosomea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine kuhusu mafuta ninataka kumuuliza Waziri na wataalam wake mimi ni mfanyabiashara kama sifanyi biashara ya mafuta lakini nina biashara zingine zina-attach na mafuta. Katika hii biashara ya kushusha bei jana Tarehe Mosi nataka mnipe majibu kwenye ku-wind up aliyepata faida ni mwagizaji au muuzaji? Kwa sababu kuna watu wana vituo huko vijijini wamefumaniwa na lita 20,000 jana na wao wameshazinunua cash na hizi pesa tunakopa benki kwa asilimia 22, amekutwa na labda lita 100,000, 200,000 bei imeshuka hakuna utaratibu wa ku-return hela zao, sasa hiyo hasara inabebwa na nani? Kwa sababu mlikuwa mnafanya tathmini ya kushusha mafuta Tarehe Mosi mlifanya utafiti kwa Watanzania ambao wana vituo huko mijini na vijijini kwamba tutakaposhusha watakula hasara gani, kama ni hapana lazima tukae chini tuangalie tumewatia umaskini watu wetu hawa wanaouza vituo vya vijijini na Mikoani kwa sababu pengine hatukufanya utafiti mzuri na haya ndiyo mambo ambayo bado ninasema Mheshimiwa Waziri tuiache TPDC ifanye kazi ya taaluma, hii kazi ya biashara tuwaachie private sector hii zimamoto Mheshimiwa Waziri wewe bado ni wa kwetu tutakuja kukaa tena na wewe bajeti ijayo bahati nzuri watu wengine computer inawezekana hawatunzi vizuri vile vipaumbele vyako ulivyovigawa jana usubiri mwakani vinakuja kukusulubu tena humu ndani. Nakueleza ukweli kwa sababu watu wametunza zile wanakusubiria mwakani, tunajua ni bajeti yako ya kwanza hii ya mkakati wako lakini mwakani tunakung’ang’ania tuko na wewe tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine Mheshimiwa Waziri Mkoa wa Geita tumepata bahati mbaya sana, tumepata Mkandarasi ambaye wenzetu tayari miradi inaendelea akaonekana hana uwezo, tumepata mwingine nikuombe Mheshimiwa Waziri hakuna siasa nzuri Tanzania kwa wanasiasa kama umeme tukuombe hawa Wakandarasi uwasimamie vizuri na Mheshimiwa Waziri imetosha muda wa kukaa ofisini wa mipango, umemaliza karibia miezi sita zunguka! Watanzania tunataka kukuona huko kwenye nguzo huko tunakueleza nguzo zinaanguka unaona, tukizungumza nguzo zinatengenezwa ni fupi unaona zunguka usiletewe makaratasi, mimi nakukaribisha sana kwenye Mkoa wangu wa Geita lakini na Jimbo langu uje uone na hayo matatizo ninayo kuambia, tunayo ofisi lakini bado watu wakitaka kwenda kulipa labda bili au nini wanatakiwa watembee kilometa 57 na ofisi ya TANESCO iko pale, tunashindwa nini gharama ya kufunga mfumo na kufanya zile correction na kuwahudumia watu tatizo liko wapi Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana Mheshimiwa Waziri haya matatizo yako kila mahala kwa Wabunge ambako vimepelekwa vituo vidogo bado mtu anaona bango la ofisi ya TANESCO lakini unaambiwa tembea kilometa 100 kwenda kulipia bili au kutatuliwa tatizo la kimsingi. Nikuombe sana Mheshimiwa Waziri uwe makini na uzunguke kwa ajili ya kuona matatizo ambayo tuko nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine Mheshimiwa Waziri la bwawa la umeme, nazungumza tena ninakuomba Mheshimiwa Waziri.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Musukuma muda wako umekwisha.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru na ninaunga mkono hoja. Ahsante. (Makofi)