Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Nishati

Hon. Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Nishati

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda na kupata nafasi ya kuchangia kwa maandishi. Hii ni kwa sababu sikuweza kupata nafasi ya kuchangia kwa njia ya hotuba Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Wizara iangalie na kukiondoa Kijiji cha Kilolo ambacho ndipo makao makuu ya Wilaya yalipo. Hiki ni kijiji na si mji na kina hati ya Kijiji, kina Serikali ya kijiji na kina vitongoji; kwa hiyo siyo sawa wao kuwekwa kwenye orodha ya miji na kulipa zaidi ya shilingi 27,000. Ifahamike kwamba vipo vijiji vyenye hali bora zaidi kuliko Kilolo na vinalipa shilingi 27,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu umuhimu wa kutengeneza kanuni na taratibu za kusajili vituo vya vijijini; hii itapunguza gharama za mafuta na kufanya biashara halali kuliko sasa ambapo biashara haramu na hatari inaendelea.

Kuhusu Bwawa la Mwalimu Nyerere naiomba Serikali kuweka mkazo katika ujenzi wa bwawa hili na kuondoa vikwazo vyote vinavyochelewesha ujenzi huo.