Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

Hon. Ummy Ally Mwalimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tanga Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii. Vile vile nakupongeza kwa kuongoza vema Bunge letu. Pili, nawapongeza sana Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati zote tatu, PAC, LAAC na PIC kwa taarifa zao nzuri ambazo sisi kama Sekta ya Afya kupitia Wizara ya Afya tunazipokea na mapendekezo yao yote tunayapokea na tunawaahidi kwamba tutayafanyia kazi. Kipekee nampongeza sana CAG kwa kufanya kazi yake ya kikatiba ya kudhibiti na kukagua fedha za Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kipekee tunataka kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge wote kwamba kila senti inayotolewa na Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kuboresha huduma za afya tutaisimamia kikamilifu. Katika kipindi cha miaka miwili tunamshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Sekta ya Afya tumepokea shilingi trilioni 6.7, haijapata kutokea katika historia ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya muda, niruhusu sasa nijielekeze kwenye hoja kama tatu ambazo zimeletwa kwenye Bunge lako tukufu. Kamati ya PAC, PIC na LAAC, walileta hoja kuhusu MSD. Suala la kwanza la MSD ni suala la ukiukwaji wa sheria katika ununuzi wa vifaatiba kutoka kampuni ya Misri ya Alhandasya, shilingi bilioni 3.4. (Makofi)

Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge, tunazingatia sheria, kanuni na taratibu. Sisi kama Serikali tumeanza kuchukua hatua za kiutawala ambapo Mtendaji Mkuu wa MSD tulimwondoa tarehe 12 Aprili, 2022. Hatukuishia hapo, tumeondoa Wakurugenzi sita wote wa MSD, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, Mkurugenzi wa Ununuzi, Mkurugenzi wa Utawala, Mkurugenzi wa Usambaaji wa Huduma za Kanda, Meneja wa Sheria na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa MSD. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, unaweza ukaona dhamira ya dhati ya Serikali katika kuwashughulikia watu wanaotuhumiwa kutenda ubadhirifu katika fedha za Umma. Kama haitoshi…

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Ummy Mwalimu, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Anatropia.

TAARIFA

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa mchango anaoendelea nao, amekiri kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na waliohusika waliondolewa. Moja kati ya kilio cha Wabunge na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, ni watu kuondolewa kutoka kwenye eneo moja kwenda eneo lingine. Aliyekuwa sasa Msimamizi ambaye alikuwa Mwanajeshi, ameondolea amepelekwa Jeshini. Yuko hai, alihusika katika hiii mikataba na fedha kupotea. Tunataka sasa tujue ni hatua gani zilichukuliwa, pamoja na kumkamata yeye ili tusaidie kurudisha hichi kiasi? (Makofi)

SPIKA: Haya, ahsante sana. Mheshimiwa, Ummy Mwalimu.

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, tumeapa mbele ya Bunge lako tukufu kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo, lazima tufuate Sheria na Kanuni za Kiserikali. Mheshimiwa Simbachawene, ameeleza vizuri, vyombo vyenye mamlaka ya kufanya uchunguzi wanaendelea na kazi. Kwa sababu, sheria yetu inazungumzia presumption of innocent, ndiyo maana tumechukua maamuzi ya kiutawala, tuache vyombo vifanye kazi yao ya taratibu nyingine za kijinai. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninachotaka kuwahakikishia, hatukuishia tu kwenye Wakurugenzi sita wa MSD, tumebadilisha Mameneja wa Kanda wote nane wa MSD. Kwanza, sisi Wizara ya Afya hatukusubiri hata Taarifa ya CAG. Tulifanya special audit wenyewe, tukaleta humu na baadhi yetu sisi tulituhumiwa na baadhi ya Wabunge kwamba sisi tunawaweka pembeni baadhi yao, lakini tulikuwa tunajua tunachokifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba niseme, kila senti ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inayopelekwa kwenye Sekta ya Afya tutaisimamia. Nitume salamu kwa watendaji wote wa MSD na wengine katika Sekta ya Afya, hatutawavumilia. Tutachukua hatua mara moja ili kulinda fedha za Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la pili ambalo kwa sababu ya muda ni suala ya Bohari ya Dawa. Hii ni hoja ya LAAC kutopeleka dawa na vifaa tiba shilingi bilioni 8.6.

Mheshimiwa Spika, suala hili tayari tumeshalifanyia kazi, kwa mfano Halmashauri ya Mbinga walikuwa wanadai milioni 577 vifaa tiba wamepokea vifaa tiba vya milioni 846. Maswa walikuwa wanadai milioni 558 wameshapelekewa bidhaa za milioni 810. Pia Dar es Saalam walikuwa wanadai bilioni 2.9 wamepelekewa vifaa vyenye thamani ya bilioni 2.8.

Mheshimiwa Spika, kubwa ambalo nataka kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge, yapo mabadiliko makubwa ndani ya MSD. Tukiangalia thamani ya bidhaa zilizosambazwa na MSD mwaka wa fedha 2021/2022 wamesambaza vifaa vyenye thamani ya bilioni 315, mwaka 2023 375 kwa hiyo ongezeko la bilioni 58. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunaangalia pia mapato revenue. Mwaka jana quarter ya kwanza MSD alipata mapato ya bilioni 77.9 quarter ya 2024 MSD imepata mapato ya bilioni 113. Hii inaonyesha maoni na ushauri wa Wabunge tumeufanyia kazi na niwaambie Waheshimiwa Wabunge tutaendelea kufanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala la MSD kupokea dawa ambazo zinakaribia kuisha muda limeletwa na Kamati ya PIC ni kweeli mwongozo ambao unatutaka tupokee bidhaa za dawa zinatakiwa zisiwe chini ya miezi 28 au 80% lakini pia kama Wanasheria wanavyojua kwenye general rule lazima kuwe na exceptions kwa hiyo, ipo sheria inayoturuhusu.

Mheshimiwa Spika, kuna baadhi ya bidhaa mnaweza mkazipokea chini ya wiki, chini ya shelf life ya wiki 24 pale ambapo bidhaa hiyo inaweza kutumika kwa ajili ya kutibu magonjwa mahususi. Kuna vitu vitendanishi vinaitwa control, hivyo vinazalishwa ndani ya miezi mitatu kwa hiyo miezi sita ni lazima pia uvipokee chini ya muda huo.

Mheshimiwa Spika, naenda haraka haraka suala la Njombe kwamba MSD alinunua mashine ya bilioni 6.3 haijafungwa. Zipo changamoto tunaendela kuzifanyia kazi lakini pia lazima tuongozwe na Taarifa za Kitaalamu. Jambo hili naomba niseme Kamati ya PAC tumelipokea na tutakuja kuleta ufafanuzi zaidi juu ya suala hili.

Mheshimiwa Spika, nimalize suala la PAC kuhusu NHIF. Hili ni suala la madeni kwamba NHIF wanaidai Serikali bilioni 228. Waheshimiwa Wabunge tumemsikia Waziri wa Fedha katika budget speech hapa wamehaidi kwamba wataanza kurejesha deni hili Wizara ya Mambo ya Ndani bilioni 45, Taasisi ya Mifupa MOI bilioni 18.2 NIDA bilioni 17.3 na Hospitali ya Benjamini Mkapa bilioni 129 wenzetu Wizara ya Fedha tayari wameshalihakiki deni hili na wameahidi kulilipa ili kulinda uhai na uendelevu wa NHIF. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa kengele ya pili ilishagonga.

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika naunga mkono hoja. (Makofi)