Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nami niweze kuchangia machache kuhusu hoja zilizopo hapa za Taarifa za Kamati zetu za kusimamia fedha. Mimi ni Mjumbe wa LAAC, kwa hiyo, nitajaribu kusema machache tu niliyonayo ambayo tumeyaona wakati tunachambua Taarifa ya CAG. Nikuhakikishie kwamba Kamati yako tunafanya kazi mpaka wakati mwingine mpaka saa sita usiku. Tulikuwa tunakuunga mkono wakati tulikuwa tunajua na wewe unakesha huko kutafuta kura, nasi LAAC tukasema mpaka saa sita, saba usiku, ili wewe ukipata usingizi naisi tumalize kazi yetu. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mwenyekiti wetu Mheshimiwa Halima Mdee ametuambia akasema tutafika, lakini tutafika tumechoka sana. Nina uhakika nchi yetu tutafika, lakini tutafika tumekuwa wachovu kweli kweli. Nianzie nyuma kidogo; wakati Bunge hili linaanzisha Kamati ya LAAC nilipata nafasi ya kuwa mwanzilishi wa Kamati hii. By then, Mwenyekiti wetu alikuwa Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla. Baada ya kupitia mambo mbalimbali, tukagundua kwamba Halmashauri zinakusanya mapato lakini zinatumia pesa ovyo ovyo, hazichangii miradi, hazi-support chochote. Kwa hiyo, tukapendekeza kwamba Halmashauri hizi zitoe percentage kwa ajili ya ku-support miradi ndani ya Halmashauri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuwepo kwa Halmashauri ni kutoa services, kuhakikisha zinasaidia wananchi wake ambao wanachangia katika mapato haya kuweza kufaidi sehemu ya kodi zao. Kwa hiyo, ikakubalika ndani ya Bunge hapa, kwamba zipo Halmashauri ambazo zina mapato kidogo, zitachangia asilimia 40 kwenye mapato yake kusaidia maendeleo katika Halmashuri zao, nyingine zitatoa asilimia 60. Kwa kweli sera hii, sijui niite sera, ilifanikiwa kwa sababu Halmashauri zilianza kuwajibika. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa hii sera Serikali imeenda kuibadilisha kimya kimya. Wamerudisha Halmashauri kwa 20 percent and 30 percent katika kuchangia Halimashauri. Jambo hili halikubaliki, hakuna Halmashauri maskini, ni ule uzembe wa kutokuwa na ubunifu kwa Wakurugenzi. ( Makofi)
Mheshimiwa Spika, mimi natumikia katika Halmashauri ya Bukoba DC. Tulikuwa tunakusanya mapato ya shilingi milioni 800, sasa hivi tumekwenda kwenye three billion. Tumechambua, tumeangalia sehemu kubwa ya Halmashauri za Mkoa wa Kigoma, wanakusanya shilingi milioni 700, shilingi milioni 600, wanaendeshaje Halmashauri hizi? Ukiangalia ni uzembe na ukosefu wa ubunifu wa Wakurugenzi. (Makofi)
MBUNGE FULANI: Yes!
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Serikali Kuu haiwezi kubeba mzigo wote. Kuwepo kwa Halmashauri hizi, zinapaswa kusaidia maana yake hatuwezi kuendesha Serikali hii kutoka Central Government. Nchi hii ni kubwa, ni lazima Halmashauri ziwepo, lazima ziwezeshwe na zijiwezeshe zenyewe, zisimamiwe ili kuweza kusaidia maendeleo.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, kama Kamati hatukukubaliana na jambo hili. Najua na wengine mpo, mtuunge mkono, hakuna Halmashauri maskini. Halmashauri ziendelee na ile 30 percent, hatuwezi kufanya Wakurugenzi kubweteka. Lazima wawe wabunifu, watengeneze vyanzo vipya. Vyanzo vipo; kilimo, biashara na kadhalika. Najua Watanzania wanapenda ile copy and paste. Ukitengeneza stendi na Halmashauri nyingine stendi, na nyingine stendi; ukitengeneza soko na nyingine soko, na nyingine soko; kwa sababu watu they can’t think beyond the box. (Makofi)
MBUNGE FULANI: Yes!
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, hatuwezi. Ni lazima kusaidia nchi hii, tuhakikishe Halmashauri zinafanya kazi, zinasaidia ku-support Serikali Kuu katika kuleta maendeleo. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Spika, kingine nitakachoongelea ni ceilling, yaani ule Ukomo wa Bajeti. Ceiling hizi namwambia Waziri wa Fedha, asitumie ceiiling hivyo kuleta umaskini na kufanya watu wabweteke. Kwa mfano, Halmashauri ya Temeke, (natoa mfano wa Halmashauri moja, lakini zipo nyingi) ilisema itakusanya shilingi bilioni 60 na zaidi. Halafu Wizara ya Fedha ikawaambia mkusanye shilingi bilioni 42. Wapi na wapi? Wao ndio unakusanya? Sasa kinachotokea, wanakwenda wanakusanya fedha zaidi ya ile ceilling, wanaanza kutafuta mafungu namna ya kuzitumia. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Spika, tulipowauliza, kwa nini mnafanya hivyo? Wakasema kuna miongozo ya IMF (International Monetary Fund). Sasa nikawauliza, What is this International Monetary Fund? Yaani inakuja kuchungulia mpaka kwenye vyungu vyetu. Wanatufanya tuendelee kukopa na kukopa mpaka tufe. Wanafurahia nini? Wanachofurahia, ni kwamba sisi tukusanye mapato, tuendeleze nchi yetu, tupunguze mikopo! Hawatakubali na Wizara ya Fedha msikubaliane na hayo. Mhakikishe ceilling zinaenda kwenye Halmashauri kwa Halmashauri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, zipo Halmashauri ambazo zina uwezo hasa zile za Majiji. Zile sasa zikusanye zi-support zile za Buhigwe. Kule Halmashauri ya Buhigwe wanakusanya shilingi milioni 600, halafu hawana mradi hata mmoja, yaani wana Mradi wa Lishe tu. Kwa hiyo, zile tuwape uwezo wa kukusanya na kuhakikisha yale makusanyo yanasaidia zile Halmashauri nyingine ambazo zimekaa; Kigoma DC, Buhigwe sijui na nyingine zipi?
MBUNGE FULANI: Kasulu
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Kasulu, zote hizo zinakusanya shilingi milioni 700, shilingi milioni 800. Afadhali Uvinza wanajitaji huko. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Spika, yaani hata Serikali inahangaika na mawese kutengeneza mafuta, yenyewe yote hiyo haina chochote! Mimi nashanga sana! Mheshimiwa Ndalichako Halmashauri yako, mwende mwangalie. Waheshimiwa Wabunge, muwe mnakuja kwenye Kamati ya LAAC mnasikiliza mambo yaliyopo huko. Muhudhurie kwenye Kamati ya LAAC ndiyo mtajua kinachoendelea ndani ya Halmashauri zetu kule, kuna mambo siyo mazuri. Nanyi msaidie kutoa mchango, siyo kudumaza kwamba mrudi kwenye 20 percent. Yaani badala ya kwenda mbele, tunarudi nyuma!
MBUNGE FULANI: Haiwezekani. (Kicheko/ Makofi)
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Haiwezekani.
Mheshimiwa Spika, baada ya kumaliza habari ya cealing, sasa niongee kidogo kuhusu kulipa pesa za Makandarasi na Wazabuni. Kwa Kiswahili wanaita Wazabauni, ndio suppliers, lakini ukitaka kufa maskini katika nchi hii, fanya kazi na Halmashauri. Yaani kama ukitaka kufa maskini na kufilisika, fanya kazi na Halmashauri, unatembea kudai mpaka visigino vikatike. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa taarifa ambazo siyo rasmi, huko chini (underground) wanasema kama hujatoa chochote hulipwi.
WABUNGE FULANI: Hulipwi, ndiyo! (Makofi)
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, tunaomba, acheni kuziambia Halimashauri hizi hazitakuwa na roho mbaya. Lipeni Wazabuni wenu, lipeni Wakandarasi walio katika uwezo wao ili mwaokoe. Serikali iliyokuwa ikisema kwamba wanalea wakandarasi na wazabuni ili kuwainua kiuchumi, hawa watu wanakopa mikopo, lakini mtu ana-supply, anadai mpaka anakufa. This is too bad. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Spika, lingine ni kuhusu usimamizi. Namshukuru sana Naibu Waziri, kwa kweli tunafanyanaye kazi mpaka saa sita na yeye. Amekaa huyu, amekomaa kweli kweli. Amekomaa, tusingekomaa tusingeweza kupitia Halmashauri zote hizo sabini na kitu. Kwa kweli it was a big job. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Spika, usimamizi wa hapa kwenye Sekretatrieti za Mikoa ambazo zipo nchi ya TAMISEMI, hazisimamii. Wana kitu kinaitwa M & E (Monitoring and Evaluation), sasa hivi wameajiri watu mkoani siyo chini ya wawili na wana bajeti, bado hawatoki Ofisini. Miradi yote ya Force Account inakufa, na yenyewe labda ingekuwa inakwenda vizuri kama ingekuwa inapata usimamizi unaotakiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, TAMISEMI watoke Ofisini, Sekretarieti za Mikoa zitoke Ofisini. Wanatufanyisha kazi kubwa; LAAC tunafanya kazi kama ya Waziri wakati mwingine na kama Wakurugenzi. Yaani tunajiuliza, sasa tumekuwa Wakurugenzi sisi mwenyewe! Haiwezekani. Tuwajibike. Serikali za Mkoa chini ya hicho Kitengo mlichoweka, mnawawekea wafanyakazi wako wawili, wanalipwa pesa nzuri, wana mafungu, ni kwa nini hawatoki Ofisini? Watoke waende kuangalia hii miradi ili fedha za wananchi ziweze kutumika ipasavyo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nisiseme mengi leo, niwachie na wengine, ila naunga mkono hoja.