Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi niweze kutoa mapendekezo ya mpango ambao Serikali inaenda kutuandalia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema kwa kunijalia afya njema. Kipekee naomba niwapongeze Mawaziri wote wawili, walionesha ushirikiano mkubwa sana walipokuja kwenye Kamati yetu ya Bajeti. Mengi ya mapendekezo waliweza kuchukua, ninawapongeza sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee naomba nimpongeze Mheshimiwa Rais na Serikali yake kwa ujumla kwa uamuzi wa busara ambao unaenda kusaidia Taifa hili na hasa kwa kuingia makataba na DP World, naomba nimpongeze sana. Makubaliano ambayo yamefanyika na DP World yatakuwa na maana pale ambapo sisi kama Taifa tunaenda kufanya kazi kwa haraka na kuhakikisha kwamba bandari yetu inakwenda kuwa na ufanisi mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hali ya kawaida kwa takwimu nilizonazo za kuonesha shehena ambazo zimekuwa zikienda nchi jirani kwa mwaka 2018 mpaka 2020/2023, naomba nisome kwa mwaka 2020/2023, shehena ambayo ilienda nchini Zambia ni 1,963,718, lakini ambayo imeenda Nchini DRC - Congo ni 3,495,195, Burundi ni 487,811, Rwanda 1,550,443, Malawi 610,506, Uganda 183,280 nchi nyingine 62,768 ambazo nchi hizi zinajumuisha Mozambique, Sudan, Kenya, Comoro pamoja na Zimbabwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hii shehena kubwa ambayo inakwenda Congo ya DRC, kwa wastani nitakupeleka shehena kama tani laki mbili na nusu, yaani katika tani laki mbili na nusu ile ambayo inaenda Eastern Congo ni tani elfu 50 peke yake, kwa hiyo Southern Congo ambayo ndio iko na Lubumbash ni wastani wa tani laki mbili kwa mwezi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo unaona jinsi ambavyo ni eneo gani sisi kama Taifa, tunatakiwa tuchangamkie kama fursa ili kuhakikisha kwamba shehena kubwa ambayo inaenda huku ambayo kimsingi ndio uchumi tunatumia kama fursa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wastani wa malori ambayo yanapita eneo linaitwa Kasumbalesa kwa siku on average ukenda kila muda unakuta malori kati ya mia nane mpaka 1000, na pale lori likienda linatumia kati ya siku 21 mpaka siku 30 likiwa limepaki linasubiri kwenda upande wa pili. Kwa hiyo, ni kwamba tunafikisha malori yanakaa siku 21 mpaka 30 hayafanyi shughuli yoyote zaidi ya kulipa parking fee na kunakuwa na taratibu za kuvusha mpaka ambapo kunakuwa na usumbufu mkubwa sana, na nchi ambazo zinatumia eneo hili ni pamoja na Afrika Kusini, Namibia, Mozambique, Tanzania na Zambia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, najenga hiyo hoja ili niweze kuikumbusha Serikali huu mzigo ambao tunasema laki mbili unapita kwa mwezi, njia ambayo ni rahisi kabisa tukitaka kwenda Lubumbash, naomba kipekee nipongeze Serikali imefanya uwekezaji mkubwa na imejenga barabara kiwango cha lami mpaka kufika Kasanga na tayari imejenga bandari ambayo inasubiri kuanza kutumika. Hivi tunavyoongea hakuna meli hata moja ya mizigo ambayo iko Kasanga pamoja na uwekezaji mkubwa ambao umewekwa na Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nini kifanyike? Upande wa Tanzania tumefanya kazi nzuri sana, na ili tuweze kutoka Kasanga Port kwenda upande wa pili kuna eneo ambalo linajulikana kama Mlilo, hilo ndilo ambalo Wabelgiji walisema kuna natural hub, kwa hiyo, ni vizuri Serikali yetu kama kuna mahusiano mazuri sana ya kidplomasia, tuweze kutumia eneo lile kujenga bandari hata kama ni kwa kushirikiana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, muda utakaotumika badala ya siku 21 ambayo malori yanakaa unahitaji masaa matatau hadi manne umeshaenda upande wa pili, na kama Taifa, maana yake hata mizigo ambayo imekua ikipakuliwa pale Bandari ya Dar es Salaam kwa sababu ya congestion, kwa sababu movement iko so slow, ukiwepo uwezekano wa kuchachusha eneo hili likatumika vizuri zaidi, hakika kama Taifa tutaanza ku-benefit.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huo Serikali iendelee kufikiria namna ya kuboresha reli yetu ya TAZARA. Ili mzigo mwingi ambao unapatikana katika Bandari ya Dar es Salaam, uchukuliwe na TAZARA na ukifika Tunduma ni rahisi kutoka Tunduma kwenda Kasanga na wakati mwingine mbele ya safari wafikirie namna gani tutaweza kuboresha ili tuwe na kipande cha reli kutoka Tunduma kwenda Kasanga. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa uharaka kabisa, low hanging fruit ndio kama hizo ambazo nasema kama Taifa tuchangamkie fursa ya kwenda DRC bila kukanyaga nchi nyingine yoyote. Tutoke Tanzania twende DRC na twende Southern Congo balada ya Eastern Congo, mzigo wake kama nilivyosema ni elfu hamsini tu lakini laki mbili as we speak inaenda Southern part of Congo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini Mheshimiwa Waziri wa Fedha ukiwa na Mheshimiwa Rais Zambia, uliahidi kwamba utakuja ili haya ambayo ninayasema uje usadiki kwa kuona jinsi ambavyo it’s so easy sisi kama Taifa kuweza ku-access kwenda upande wa pili ule. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti,eneo lingine ambalo ninaomba kuchangia ni katika suala zima la utalii; kama Taifa, utalii unaonekana kwamba kasi yake inaongezeka lakini kasi hii inaweza ikaongezeka zaidi kwa kufungua circuit ya Southern Highland ili Mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma na Rukwa, kuna vivutio ambavyo hakika bado viko very virgin, watu bado wanahitaji kwenda huko. Tuna kazi moja tu ya kuhakikisha kwamba tunaweka miundombinu ikiwepo Maporomoko ya Kalambo, linatakiwa jambo moja tu kuwa na airstrip kwa sababu mtalii anakuja huku na fedha yake asingependa asafiri umbali mrefu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama Kalambo tuko tayari. Wizara ya Utalii wameshatuomba tuoneshe sehemu ambayo inafaa kujenga airstrip na sisi tuko tayari na tulishalitenga eneo. Kwa hiyo, tunaomba tu Serikali mfanye jitihada za haraka kuhakikisha kwamba uwekezaji huo uliofanyika na hasa kwa kutumia ECF ambayo for sure nadhani mwakani pesa hii itapatikana kwa ajili ya mkopo ili tuweze kuendeleza suala zima la utalii, hakika tuifungue nchi yetu pande zote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kule kaskazini inafanya vizuri lakini ni vizuri kukawa na sehemu nyingine ambazo itakuwa ni kama sehemu ya kupumulia ili kama Taifa tutumie nchi yetu ambayo tuna potentials nyingi sana ambazo hatujaweza kuzitumia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya michango hiyo miwili naomba niunge mkono hoja ahsante sana. (Makofi)