Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja ya Kuazimia Kuwahamisha Maafisa Ushirika katika Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Maafisa Ugani chini ya Wizara ya Kilimo

Hon. Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hoja ya Kuazimia Kuwahamisha Maafisa Ushirika katika Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Maafisa Ugani chini ya Wizara ya Kilimo

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi nichangie hoja iliyoletwa mbele yako.

Mheshimiwa Spika, kwanza nianze outright kwa kusema kwamba siungi mkono hoja iliyotolewa. Naomba wenzangu watanikumbusha katika mahojiano ambayo Hayati Baba wa Taifa aliwahi kufanya na kujutia kati ya maamuzi ambayo aliyafanya katika uongozi wake alisema kwamba ni kitendo cha kuua Halmashauri na kurudisha Serikali Kuu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa katika hoja ambayo imeletwa ni kama vile tunataka turudie makosa, ile sense of ownership ya watu wetu tuanze kuinyang’anya kwa style ambayo inaonekana kwamba hakuna performance nzuri, kwa hiyo, tuanze kuinyofoa. Maana yake itafika mahali hata vikao vya WDC ambavyo vinaketi vitakuwa havina maana yoyote na watu wetu kwa ushiriki…

MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, muda mchache sana.

TAARIFA

SPIKA: Inatokea wapi taarifa? Mheshimiwa Kandege kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Kasalali Mageni. (Kicheko)

MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Spika, nataka nimpe taarifa mzungumzaji ya kwamba ili halmashauri zetu ziendelee kuwepo na kutekeleza majutio na kauli ya Baba wa Taifa, kinachopaswa kufanyika sasa ni kuimarisha mfumo wa halmashauri zetu na kurudisha vitu vyote ambavyo viliondolewa halmashauri ikiwemo maji, barabara na ardhi na siyo kuondoa kilimo. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Kandege, unapokea Taarifa hiyo? (Kicheko)

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, naipokea taarifa kwa maana ya kuboresha. Hii inaonesha jinsi ambavyo sisi kama Taifa tulivyoamua kwamba D by D iwepo tulikuwa tunamaanisha kwamba wananchi lazima wakiri na wamiliki Serikali yao ili wawe sehemu ya maamuzi ambayo yanaenda kufanyika kule Central Government. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa hii style ambayo imeanza kuja, hiwezekani tukachukua labda udhaifu wa Halmashauri X then tuka-conclude kwamba halmashauri zote hazifanyi vizuri. Kwa hiyo, tuhangaike case by case; hata hizi taasisi ambazo zimeanzishwa, cha kwanza kulikuwa na budget constraint ambayo inatibiwa, ndiyo maana TARURA inafanya vizuri kwa sababu ina bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni vizuri Serikali mtuambie: Je, ni kweli mmeshindwa? Katika hizi taasisi ambazo wanataka zihame, mmeshindwa kiasi kwamba kwenye halmashauri haiwezekani, mmefanya michakato yote imeshindikana mpaka mnasema mna give in ili watu wetu wasipate nafasi ya kushiriki na liwe linatoka Central Government kushuka kule chini? Hakika naamini inahitaji research ya kutosha. Namwomba Mheshimiwa Mbunge aliyekuja na hoja…

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: …kwa research ambayo amefanya upande wake tu...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Mheshimiwa Kandege kuna taarifa na kengele imegonga. Sasa acha niwape dakika moja mmalizie. Mheshimiwa Getere, taarifa.

TAARIFA

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Tuko kwenye mapinduzi makubwa sana ya kilimo. Mimi sidhani kama kuwatoa ushirika na kujipanga vizuri katika kutafuta mazao ambayo washirika watajipanga vizuri na wakapata utaratibu mzuri ili waweze kuongeza mapato ya halmashauri kwa mazao hayo, eti itakuwa ni kosa. Tuwe nao na mazao hayap. Wakisimamia vizuri pamba, wakisimamia vizuri kahawa na tunahitaji ushirika, mimi naomba hiyo iondoke, irudi kwenye Wizara ya Kilimo mapato yapatikane. (Makofi)

SPIKA: Haya, Mheshimiwa Kandege unaipokea taarifa hiyo? Muda wako ulikuwa umeisha, kwa hiyo, sekunde 30.

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, taarifa iko against na mtazamo wangu. Kwa hiyo, kwa vyovyote vile hakuna namna ambavyo naweza nikaipokea ikanisaidia. Sana sana imsaidie yeye kwa upande wake. (Makofi)