Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hoja ya Kuazimia Kuwahamisha Maafisa Ushirika katika Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Maafisa Ugani chini ya Wizara ya Kilimo

Hon. George Boniface Simbachawene

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibakwe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hoja ya Kuazimia Kuwahamisha Maafisa Ushirika katika Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Maafisa Ugani chini ya Wizara ya Kilimo

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, kwanza nakushukuru kwa kuruhusu hoja hii ijadiliwe na pengine fursa hii inaweza ikawa imetokea katika wakati ambao imechelewa kutokea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu kinachoelezwa hapa juu ya namna ambavyo ugatuzi umekuwa ukiathiri dhana ya D by D ni jambo ambalo limekuwa likiendelea kwamba tumeondoa barabara, tumeondoa maji na tunaendelea, na pengine tunafikiri utaratibu huo uendelee na mwisho wake itakuwa tumeondoa vitu vyote. Kwa hiyo, kwanza tutakuwa tunaenda kinyume na Katiba. Ibara ya nane ya Katiba inaweka msingi wa madaraka ya umma, madaraka kwa wananchi, lakini ibara ya 145 na ibara ya 146 zitakuwa zinakiukwa, kama Mheshimiwa Ole-Sendeka alivyosoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni tofauti sana miradi ya maji, ni tofauti sana miradi ya barabara na jambo linaloitwa ushirika. Ushirika ni zao la wajamaa. Ushirika ni jambo la wananchi wenyewe.

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Condester Sichalwe.

TAARIFA

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, nataka kumpa taarifa Mheshimiwa Waziri kwamba, pamoja kwamba tunarejesha madaraka kwa wananchi, mbona hata kule kwenye Serikali za Mitaa kwenye vikundi vya 10% kama lengo ni kurudisha madaraka kwa wananchi, kwa nini wale wanaiba pesa za wananchi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, sisi tunaomba jambo hili lirudi kwa Waziri mwenye dhamana ili aweze kuwasimamia Maafisa Ugani na Maafisa Ushirika ili kumsaidia mkulima wa nchi hii maana anateseka sana, na ndiyo huko tutakuwa tumemsaidia mwananchi, ahsante. (Kicheko)

SPIKA: Mheshimiwa Simbachawene, unaipokea taarifa hiyo?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, naipokea taarifa ya mwanangu. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilitaka kusema hivi, kwa maneno machache, kwamba ushirika ni mali ya watu wenyewe. Yaani hata ushiriki wa Serikali ni kwa sehemu sana kwa sababu washirika wanakubaliana wao, wanapanga mambo yao wao. Ndiyo msingi. Huwezi ukauondoa ushirika kwa wananchi wenyewe. Kwa hiyo, mahali sahihi unapotakiwa kukaa ushirika ni Mamlaka ya Serikali za Mitaa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kazi ya Serikali na Wizara za Kisekta ni ku-facilitate, ni kupeleka rasilimali kule chini. Kinachokosekana hata tukafikia hapa, ni kwamba Tume kwa mujibu wa Sheria hii tuliyoipitisha, Sheria Na. 6 ya mwaka 2013, Tume wajitahidi kufika kule chini kupeleka fedha, kupeleka ujuzi, kupeleka wataalamu, wapeleke kule wataona matokeo yanaendelea, lakini siyo kunyang’anya uwa-centralize washirika ushirika huo uta…

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Simbachawene kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Mwanaisha Ulenge.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, taarifa.

TAARIFA

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, naomba kumpa taarifa mzungumzaji kwamba kweli dhamira ya ushirika ni kupeleka tija na ni ushirika wa watu wenyewe kule chini, lakini kinachohitajika ni maendeleo yao kule chini. Maafisa Ugani pamoja na Maafisa Ushirika, iwapo hakutakuwa na mpango wa kuwaendeleza kitaaluma (on job training) kule halmashauri, hakuna, hakuna kitu chochote kinacholeta umuhimu wa kuwafanya wawe bora zaidi ili kuwahudumia wale watu wa chini; je, tunapelekaje tija kwenye jamii? (Makofi/Kicheko)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mkiuliza maswali kwenye taarifa ni kama unataka sasa aanze kujibu swali lako badala ya kuendelea na mchango wake.

Mheshimiwa Simbachawene, unaipokea taarifa hiyo? Ile sehemu ya taarifa ili usilazimike kujibu swali lake.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa ni sehemu ya swali, nitamjibu tukitoka hapa, lakini kwa hapa nataka niendelee hivi... (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, ninachotaka kusema ni kwamba tutafute nchi zenye mfumo mzuri wa utawala na uongozi kama nchi yetu ni vigumu sana kuipata. Huu mfumo ambao tunauona una upungufu huu mdogo, umeifikisha nchi yetu hapa, na pengine hata sababu ya amani na utulivu wa nchi yetu unatokana na mfumo huu tulionao. Tuulee vizuri, tuutunze vizuri mfumo huu wa kuhakikisha kwamba Mamlaka ya Serikali za Mitaa zinaendelea kuwa na nguvu kama zilivyotakiwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuendelea kutohoa na kuondoa nguvu zake kule tunadhoofisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Sekta zetu zote zijiulize kabla ya kuamua kuchukua kitu chochote kutoka kule chini kama je, wametimiza wajibu wao sawa sawa?

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, taarifa.