Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naomba kwanza niseme kwamba nimetumika kwenye sekta ya TAMISEMI miaka 12 nimetumika Serikali Kuu miaka 18 na kote tuliona changamoto. Wakati niko miaka 18 kwenye Wizara ya Elimu tulibaini kwamba elimu inaweza ikasimamiwa kwa ufanisi kama kila kitu kitafanyika makao makuu lakini ilikuja kuthibitika vinginevyo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baadae tulifanya utafiti mdogo wakati ule Wizara ya Utumishi. Tulikuta mwalimu ameacha kazi miezi sita au zaidi Wizara haina habari inamlipa mshahara kwa sababu usimamizi wake ulikuwa unafanywa na Katibu Mkuu wa Wizara wakati ule Dar es Salaam kwa shule zilizotapakaa nchi nzima lakini achia mbali utoro na kadhalika.
Mheshimiwa Spika, haya maamuzi ya D by D nadhani Tanzania hayajaeleweka vizuri. Kama itakupendeza najitolea kuwa mwalimu katika kipindi kimoja tujielimishe D by D kule kulikofanikiwa walinya nini. Kwetu hapa tutazilaumu sana halmashauri lakini ule uwezeshaji haujafanyika ipasavyo. Nitoe elimu kidogo kwenye nchi zilizofanya vizuri sana kwenye ugatuaji wa madaraka kuna principle moja wanayoi-apply inasema “The principle of subsidiarity” maana yake pale ambapo shughuli zinafanyika…
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, taarifa.
SPIKA: Taarifa inatokea wapi?
MJUMBE FULANI: Kwa Sophia.
SPIKA: Mheshimiwa Jumanne Sagini kuna taarifa kutoka kwa Sophia Hebron Mwakagenda.
TAARIFA
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, naomba nimpe taarifa mzungumzaji kwanza amesema kwamba amefanya kazi miaka 12 ya uzoefu na 18 ya uzoefu. Bado ni Waziri wa Serikali hii, kwa nini hajafanya hili suala? Kwa sababu mtoa hoja baada ya kuleta hiyo hoja yake ni baada ya mambo kutokwenda sawa. Kwa hiyo, nampa taarifa ni vema wakatengeneza kutumia uzoefu alionao na vitu ambavyo amevifanya ni labda itasaidia Taifa hili, ahsante.
SPIKA: Mheshimiwa Jumanne Sagini unaipokea taarifa hiyo?
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naipokea kwa sababu tu hana ufahamu na nilichofanya, nimefanya mengi sana kwenye sekta hii. Hata ukatibu mkuu pale miaka saba, minne ya unaibu na mitatu ya Ukatibu Mkuu nilifanya haya. Sasa nasema hivi principle ile inasema hivi, unaposimamia jambo ambalo linafanyika pale ulipo, ufanisi wake unakuwa mkubwa zaidi kuliko ukisimamiwa kutoka mbali. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa tabia ya ubinadamu naomba niseme kwa Kingereza kwa sababu nimeitoa huko normally people do what you inspect not what you expect. Ukiwa makao makuu ya Wizara ukamsimamia mwananchi aliye kwenye kijiji ufanisi wake uko ndugu wapi ndugu zangu. (Makofi)
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, taarifa.
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kilichokosekana kwenye mfumo wetu wa ugatuaji…
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, taarifa.
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: …kilichopungua kwenye mfumo wetu wa ugatuaji ni nafasi…
SPIKA: Mheshimiwa Sagini kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Kunti.
TAARIFA
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, leo maafisa ushirika na maafisa ugani wako TAMISEMI na wako hapo kwenye miguu na ndiyo wanafanya vibaya kuliko kitu kingine chochote.
SPIKA: Mheshimiwa Sagini unaipokea taarifa hiyo?
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naipokea anakosa Subira tu, nilikuwa nataka nimwambie ni kwa nini tunaona huo udhaifu. Moja, baada ya uamuzi huu wa kupeleka madaraka karibu na wananchi, wizara za sekta na watendaji kwenye local government walipaswa wafanye realignment moja kwenye attitude na perception kwa sababu wizara hizi zilizoea kutekeleza. Leo ukiwaambia washiriki kwenye sera wafanye M and E, mentoring and evaluation wafanye capacity development ya watu kule hayo hayafanyiki. Peleka resources, peleka vifaa… (Makofi)
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, taarifa.
SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kengele imeshagongwa Mheshimiwa Sagini ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru.