Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpendae
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. TOUFIQ SALIM TURKY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Mwaka uliopita Rais wa African Development Bank alihutubia akasema kuwa, katika jambo rasilimali ambayo itakuja kuwa ghali basi itakuwa ni chakula. Tumeshafika asilimia, sasa hivi nimetizama dunia inapoelekea inaenda katika exhaustion na ukitizama watu tumeshazidi Milioni Saba.
Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru sana Serikali kupitia kwa Mama yetu Rais mpendwa kuona uono huo na kuja na mapinduzi makubwa sana ya kilimo Tanzania. Ukitizama katika historia ya Tanzania basi hii tumeupiga tena tumeupiga mwingi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba kumshukuru sana Waziri husika kuja na taswira tofauti, kuna kitu kinaitwa agriculture na agro-business. Agriculture tunaenda katika tamaduni, lakini safari hii tukasema hatutaki kilimo cha utamaduni, tunataka kilimo cha biashara. Kwa hivyo, nampongeza sana Waziri Bashe kuja na mfumo mpya. Pia lazima nimshukuru Bwana Mzee wa Mayele kuhakikisha katenga bajeti. Kaka yangu Mheshimiwa Mwigulu pale akasema aah! safari hii nitachumba huku, nitachumba huku, uono wa Mama hii agro-business na tunapoelekea dunia inayohitajika kilimo kuweza kupatikana kwa hivyo, hongereni sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jamani jana nilipata fursa ya kuonana na wanafunzi kutoka UDOM, wanamaliza research zao na tulikuwa tunabadilishana mawazo tu, wakawa wanazungumza kuna mmoja kamaliza uchumi, ananiambia Mheshimiwa tunamaliza sisi uchumi tayari, sasa a tunataka kuja huko utusaidie tutafanikiwa vipi? Tutapata fursa gani katika biashara au katika ajira?
Mheshimiwa Naibu Spika, nikamwambia sasa wewe umekuwa mchumi, sisi kawaida yetu kule watu wenzetu wanapomaliza vyuo wanakuwa wameshakuwa wachumi wanakuja na maarifa. Sasa hebu nikuulize mwenzangu, wewe sasa hivi umeshakuwa mchumi, unaona katika hali halisi sasa hivi ya nchi yetu, kitu gani kinaweza kutusaidia sisi katika nchi yetu?
Mheshimiwa Naibu Spika, kanambia mambo mengi tu. Nikamwambia mambo mengi gani, niambie? Akaniambia unajua kama sera zetu. Sera kama zipi? Akasema unajua kuna sera nyingine haziko sawa, lakini ukienda huku, vipi, tunaweza tukaziweka sawa. Kama zipi? Akawa hakamati sehemu. Nikamwambia inawezekana tuambie pengine tuambie Fiscal Policy, Investment Policy au Policy ya aina gani?
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ukitizama akawa ameganda. Baada ya hapo tukaitizama sasa tulilokuwa tunaongelea suala zima la hapa tunapozungumzia kabla ya hapa katika michango yangu ya kabla kuwa, wanafunzi wengi tunamaliza University, lakini wanakuwa hawana mchango katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mama juzi karibuni kati hapa alikuja Zanzibar katika organization ya MIF, (Mwanamke Initiative Foundation), akawa anaongelea suala zima la kubadilisha curriculum. Namshukuru sana Mama kwa kuja na uono wa kuona sasa elimu yetu nafikiri umefika wakati wa kuja na mageuzi na hilo ni muhimu sana kwa Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimekaa na vijana wanamaliza, wenzetu mataifa mengine wanatumia fursa hizi wanakuwa wanakaa na makampuni. Wanaenda katika Universities wanafanya interview kwa sababu tunajua umuhimu wao kuwa sasahivi tunawahitaji wao wanakuja na maarifa mapya, lakini wanafunzi wetu bado wanategemea maarifa yaleyale yaliyopita na siyo maarifa mapya.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kupitia huko wakaja pia wakaniambia kabisa sisi bwana Walimu wetu wanatuambia, ukitaka kufaulu au kuendelea kimaisha lazima unatakiwa mtu akukamate mkono uwe nae hivi ndiyo maisha utapiga, lakini siyo kwa elimu yetu tuliyo nayo. Hao ni Maprofesa wetu wanaongea lugha hizo, sasa hawa wanafunzi wetu watakuwa na dira gani? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jamani watu wengi sana pengine au mtakuwa mnajua, hamfahamu, lakini tajiri wa dunia wa sasa hivi anaitwa Elon Mask, watu wengi labda wanaweza wakafikiri kuwa huyu ni Mmarekani, lakini huyu ni mwana Afrika, kazaliwa Pretoria, South Africa. Kuna wakati mmoja akaulizwa kwa nini ulitoka zako Afrika unaendazako Marekani? Akasema unanua mimi nilitengeneza instrument ya kulipa inaitwa PayPal, alianzisha yeye na mwenzake, lakini baada ya hapo wakaiuza, baada ya hapo akaenda zake Marakeni. Akaulizwa kwa nini ulienda zako Marekani? Akasema nimeona Afrika hakuna mtu anaewekeza katika ndoto.
Mheshimiwa Naibu Spika, Afrika tunabonyezwa tunabakia huku, nimekuja Marekani nikasema mimi nataka nianzishe gari lisilokuwa na dereva, nitaanzisha battery ambayo haitaki mafuta haitaki chochote itakuwa inafanya kazi. Afrika hakuna mtu kanisikiliza. Nimeenda Marekani watu wamenisikiliza na leo ile kampuni inaitwa Tesla ni namba moja duniani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tukitizama jamani duniani kwetu huku Afrika, imekuwa ni jambo la ajabu sana kwamba hatutaki kuwekeza katika suala zima la ndoto ya research. Katika Bara linaloongoza sasa hivi kwa kukua katika masuala ya teknolojia ni South Korea. Waliulizwa ilikuwaje wewe ghafla umekua kwa haraka katika Bara hili la Asia? Akasema tumetenga asilimia Nne ya GDP yetu katika research and development, na leo wao ni viongozi katika masuala yote ya electronics. Samsung sasa hivi anaendana pamoja na iPhone na kampuni nyingine kubwa, Hyundai, ana kampuni nyingi sana, anashindana na Japan. Leo tujiulize tumewekeza kiwango gani katika research and development? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo watu wanafanya research, Oxford wamefanya research, Universities zinafanya research, Imetoka AstraZeneca ndiyo imekuwa vaccine ya COVID-19. Tujiulize Universities zetu research zao zinasaidia nini katika uchumi wa Taifa? Jibu litakuwa hakuna! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba sana Serikali ilitazame suala zima la research and development kwani kama tunataka tuendelee katika dunia hiyo, tusibakie katika ndoto tu, basi lazima tuende na wenzetu katika masuala ya research and development. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kumalizia, jana walikuja wenye viwanda wanaotengeneza biscuit, biscuit viwanda wazalendo wamezidishiwa 500 shillings kwa kilo as excise duty. Wanasema sisi tuna viwanda sote tunafahamu sasa hivi mfumuko wa bei viwanda vinatumia unga, unga wenyewe kupatikana taabu, bei zimepanda, leo tunakuja tunaambiwa tulipe 500 Shillings per kilo as excise duty na wakati watu wa importation hali iko vilevile, sasa hapa tutaishi vipi? Sasa nilikuwa naomba sana kupitia Waziri, Wizara ya Fedha, walitazame hili suala na nyakati zilivyo. Nafahamu tunatafuta mapato ya tofauti katika sehemu na nyanja tofauti, lakini hii biscuit tuitizame wanakula akina nani? Ni watoto wetu wa shule kwenye vishughuli hivyo vya madarasani na sehemu nyingine, kwa hivyo, nilikuwa naomba sana katika sehemu hiziā¦.
NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Turky, mengine andika.
MHE. TOUFIQ SALIM TURKY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana na naunga hoja kwa asilimia zote. (Makofi)